Huo ndio Ukweli mchungu kuumeza, lakini usiokwepeka.
Sio ujasiri wala ushujaa kwa viongozi kutembea mkifurahia mikopo na kujipiga kifua mbele ya wananchi majukwaani,kama vile ni jambo la kheri na kishujaa kukopa kopa bila Dira ya kitaifa.
Mnapaswa pia kutoa elimu kwa wananchi, juu ya madhara ya mikopo hiyo kwa uchumi wa nchi.
Ili wananchi waweze kujiandaa kisaikolojia huko mbeleni.
Kwa sababu nyinyi viongozi mnakwenda kukopa huko,lakini walipaji wakuu ni wananchi na vizazi vyao.
Kwa nchi iliyojaaliwa raslimali kama hii ya Tanzania.
Hatukupaswa na hatustahili kushinda mguu na njia kwenda kutembeza mabakuli huko Duniani,sambamba na nchi maskini wa kweli ambazo zipo Africa na kwingineko.
Wakati huo tukiziacha mali zetu zikichotwa kwa mkono mwingine na hao hao wakopeshaji,kwa msaada wa baadhi ya wenzetu wachache kwa manufaa binafsi.
Kwani mifano hai ya mikopo hiyo na madhara yake kwa ushamiri wa taifa tunao.
Mfano wa karibuni kabisa ni huu unaoendelea huko Sri Lanka [emoji1224].
Walikopa hadi wakanyanganywa Bandari yao kuu.
Na sasa wanaelekea kupoteza uhuru wao kama taifa.
Ni baada ya hao hao IMF watalapoitangaza Sri Lanka kama nchi iliyofilisika.
Bado mfano mwingine wa madhara ya mikopo uko Lebanon [emoji1146].
Kwa hiyo CCM wakati mkisifia ukopaji muelewe jinsi mnavyoelekea kulitumbukiza taifa hili tajiri la raslimali,mikononi mwa wakopeshaji.
EeeeNHeeeeee!
Mkuu 'Voicer', you ain't seen nothing yet!
Hiyo mikopo angalau ingetumika ipasavyo na kukamilisha miradi iliyokusudiwa kikamilifu, pengine tungefaidika na matokeo ya mikopo hiyo, na kidogo tukaziba masikio juu ya masharti yake; na hata wakati mwingine kuyakaidi hayo masharti (kwani watatufanya nini tukikaidi)?
Lakini tatizo linakuwa kubwa zaidi wakati miradi yenyewe faida zake haionekani, na juu ya yote masharti ya mikopo ndiyo yanakuwa makali zaidi. Hapa ndipo penye tatizo kubwa na hawa viongozi tulionao wanaoamini njia pekee ni kutembeza bakuli.
Sasa ngoja nikupe jambo jingine linalohimizwa na hao wakubwa wa WB na IMF, pengine ndilo baya zaidi ya hiyo mikopo na masharti yake.
Kama hujatazama vizuri, Samia asha anza wimbo juu ya jambo hili, kinachosubiriwa tu sasa ni kutangaziwa miradi itakayofanywa chini ya mpango wenyewe..
Mpango huu ni hiyo inayoitwa PPP (Private Public Partnership). Tuakuja kujengewa 'Expressway' hapa Dar hadi Morogoro au hata Dodoma. Wenye pesa yao watapewa miaka 30 au zaidi kuzalisha faidi yao juu ya migongo yetu tutakaotoa jasho kuitumia barabara hiyo. Kama wewe ni kabwela huwezi na hutakiwi kusogea karibu na barabara hiyo.
Huo ndio uwekezaji mpya utakaopata nguvu zaidi miaka hii ya Samia.
Baadhi ya watu watauliza, kuna ubaya gani wa kufanya hivyo, lakini hata mimi nitauliza, kuna ubaya gani wa sisi kufanya kazi hiyo wenyewe.
Kwa nini nipende kuishi kwenye nyumba ya kupanga na maudhi ya masharti ya upangaji, kama ninaweza kujenga nyumba yangu mwenyewe? Hilo nalo ni swali linalohitaji majibu kamili.