Nakupa mfano wa kazi inamfanya mtu awe online muda wote,
Kwa mfano mlengaji wa magari yaliyotumika Tanzania na mostly makazi yake ni Dar au mwanza, huyu kitendea kazi kikubwa ni simu, yaani madalali wakipost gari ukiielewa kazi ni kwenda kukagua wewe na fundi wako na mnaenda na gari, pale mtabargain bei utaangalia ina vipengele gani, gari utaichukua labda kuna marekebisho ya gearbox, kumwaga oil, kubadili bonet au mwamba, kufunga shockup mpya au kufunga android radio, au kunyoosha bodi na kupiga mkono mmoja rangi smart na put isiwe nyingi, kuweka tairi mpya, au kurekebisha engine hapa wewe unakua pembeni unakula nyama choma huku ukiwa online, labda ulinunua hiyo gari kwa kulenga kwa milioni tano plus marekebisho ubaoni unaiweka kwa milioni 8 hapo labda unafukuzia hata milioni moja unusu, sasa unawapa kazi madalalari waipost mitandaoni huko labda vijiwe vya kinondoni vijana, chipolopolo, mlimani, mikumi, lumumba kote huko utasikia simu tu zinaita watu wanakuja kukagua gari ataefika bei basi anapewa gari na faili anakuwekea pesa kwenye akaunti yako, hasa mtu wa namna hii asiwe online ili iweje wakati anategemea biashara awe hewani ili afanye business,