Mnaotumia bidhaa za Apple® Mnapigwa sana. Sijui hata mnavyotoa hela mnafikiriaga nini?

Nikiwa na fuba sitaona shida kuvinunua hivyo, ila kwa uchumi huu wa kati hapana kwakweli.

Acha tukomae na Samsung tu.
Yaani ununue simu, ununue usb, ununue kichwa cha chaji, ununue cover alooo yaani unakamilisha simu mdogomdogo kama unajenga vile
Haiwezekani mtu ananunua simu ambayo ikipata clack kidogo. Anapata plessure, au ana kaa months bila ku lipear.

Apple wako njema. Ila kuna wabongo wengi wanaforce.
 
Ujinga ni mara moja, ukiurejea ujinga mara ya pili maana yake umeamua kwa hiari yako kuwa mpumbavu.

Ni waafrika tu ambao huwa tunaona fahari kumiliki mavitu ya gharama ili tuonekane nasisi tumo au tuna hela wakati mambo ya msingi mengi tu yanatushinda. Umaskini hauondoki kwa kumiliki iphone ya million 3 😂 tubadilike maana wengi wanatumia nguvu kubwa kuonekana matajiri wakati kimsingi hawana huo utajiri.
 
Hawatakaa wakakuelewa aisee. Kamwe. Na watumiaji Wengi wa simu tunatumia chini ya 30%
 
Kwanza nakubaliana na hoja kwamba hizi bidhaa zina ubora.ILA NA UHUNI UPO,
mfano wengi wamesema material inayotumika kutengeneza bidhaa za Apple ni "next level"
Fafanua tofauti ya malighafi iliyotengeneza iphone na Samsung ili tone huo uexceptional

Wengine wanaongelea security features,eleza in details tofauti ya hizo apple na abdroids ili tuone.

Kikubwa zaidi mimi naona hizi bidhaa zimekaa kimashindano zaidi.zinasambaza aura ya taifa la marekani na ziko more hyped.

Wapuuzi utawasikia "tafuta hela"
Ndo maana tunakufa masikini kwa kuendekeza prestigious badala ya prosperity.
Jamaa dunia imeanza kuwastukia
 
Jiulize kwanini marekani anapiga vita electric cars toka china nchini mwake?

Kama watu wanalipwa mshahara mzuri kwanini wasinunue hayo ma tesla na badala yake wanakimbilia EVs za mchina?
Maana yake hata wamarekani wenyewe na pesa zao wameona wanaibiwa
 
chai
 
Bidhaa nyingi, tunanunua kwa show off sio kwa kujua au kuhitaji matumizi yake.
 
Nilitaka kuandika chochote lakini naona umemaliza kila kitu mwenye uelewa ataelewa.
 
Zina ubora, mimi natumia MacBook Pro, nina Smart Watch ya Apple, nina IiPhone 14 Pro Max ila kwenye Tablet bado natumia ya Samsung
Mm nina samsung hata sikumbuki nilinunua lini ila ni kama miaka 4 imepita, Tsh 500,000/= na ninavyoiona ina miaka mingine kama 4 au 5. Naona ni simu bora sana samsung. Jaribu.
 
Kila bidhaa duniani ina mlengwa wake, ambaye akiiona tu wala hajiulizi mara mbili au kuanzisha thread ya kulalamika.

Wasio walengwa ndiyo hivi ukiona hizo bei unaziwaza tofali na mifuko ya sementi, lakini walengwa wanaona tu hiyo Apple.

So waachie walengwa waishi maisha yao.

Ova
 
Ili nalo neno. Nimelipokea mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…