Mnaotumia bidhaa za Apple® Mnapigwa sana. Sijui hata mnavyotoa hela mnafikiriaga nini?

Mnaotumia bidhaa za Apple® Mnapigwa sana. Sijui hata mnavyotoa hela mnafikiriaga nini?

Hahahaa kuanzia iPhone 13 ukitafuta 12 kushuka nasikia wanaziharibu battery maksudi ili mnunue za juu
Ndo ulivyodanganywa 😂 😂
Wanatoa hizo sababu ili zisionekane betri hazina ubora ila ukweli ni kwamba hamna kitu, mi nina marafiki nawaona wanahangaika kubadilisha na sio kwamba wanaziharibu.

Wanasema Ooh sijui iPhone hupaswi kuchezea magemu, sijui hutakiwi sijui kufanya hivi vile 😂 sasa what's the aim of having a phone which is limited??
 
Ndo ulivyodanganywa 😂 😂
Wanatoa hizo sababu ili zisionekane betri hazina ubora ila ukweli ni kwamba hamna kitu, mi nina marafiki nawaona wanahangaika kubadilisha na sio kwamba wanaziharibu.

Wanasema Ooh sijui iPhone hupaswi kuchezea magemu, sijui hutakiwi sijui kufanya hivi vile 😂 sasa what's the aim of having a phone which is limited??
Aaah kumbe majanga tu!!

Cc Depal 🤣🤣🤣
 
Yaan simu unanunua zaidi ya 1 million alaf inazungua kitu kidogo kama chaji(yaan kampuni kubwa vile Apple wanavoisifia pamoja na ma-research yao wanayofanya kila siku na overpriced products wanashindwa kutengeneza simu bora), ukiwauliza utasikia "ooh ni kweli kuanzia iPhone 13 kushuka chini betri zinazingua" like broo wtf?? Mm na Samsung yangu tokea kitambo tushasahau mambo ya chaji na betri 😂 😂
Samsung gani unatumia mkubwa na Mimi nikaipate? Kigezo charge siku nzima.kutembea na USB hapana
 
Kuna kitu kinaitwa product review, kwa mentality yako basi watu wasingekua wanachambua kwa sababu tu ati kila product hua na targeted market. Hata magari yanachambuliwa kila kukicha na people make a fortune out of reviewing products.
Soma kwanza kichwa cha habari cha hii thread, halafu uje usome maoni yangu kisha unijibu upya.

Ova
 
Kampuni la Kimarekani Apple, maarufu kwa kuuza bidhaa za electronics na accessories zake, wanauza ivyo vitu bei ghali sana.

Inawezekana ikawa ni value for money, ila kuna baadhi ya vitu ni wazi wanawaibia "loyal customers" wake, sema ndio ivyo hawaoni au wanajizima data.

Tuachane na iPhone zao kua Million 3 kwenda juu, au Laptop zao za kishua. Ebu Kwa mfano checki izi products:

Mac Pro wheels $700 (Tsh Mil 1.8)

Hii sio computer, ni magurudumu manne ya kuweka kwenye CPU sijui tuiite ya Mac Pro. Hujakosea kusoma.

View attachment 3000624Haya matairi ilibidi wayagawe bure unavyonunua iyo bidhaa yao.

Mac Pro stand $1000 (Tsh Mil 2.6)

Naam. Mil 2.6 tunanunua stendi ya kuiwekea Monitor yetu ya Mac.
View attachment 3000625Hii pia ilitakiwa upewe bure. Kwann walitengeneza computer isio na stendi?

Mikanda ya saa $100 (Tsh Laki 2.6)

Achana na bei ya saa, mkanda tu huu unauzwa laki 2 na nusu na zaidi.
View attachment 3000608

Airpods Max $550 (Tsh Mil 1.4)
Utakua ushakutana na mabishoo wamevaa copy ya aya madude.
View attachment 3000627
Aisee original yake ndio ivo, Mil 1.4 cash.

Apple Pencil $130 (Tsh 340,000/=)
Hii wenzio Samsung ukinunua Tab wanakupa bure sijui kwann wao wanauza.
View attachment 3000606

Mac Pro $7000 (Tsh Mil 18)
Ukiliona kwenye picha kama kidude cha kusugulia nyanya au karoti. Ila ndio ivyo tena, bei ya gari.
View attachment 3000631


Waya type C $30 (Tsh 77,000/=)
Waya tu, wa mita 2 unauzwa hivi. Bila kichwa. Bila protector. Bila kava. Waya.
View attachment 3000614

Cover la Simu la Silicon $50 (Tsh 130,000/=)
Haya makava tunayaona kwa elfu 5 yanauzwa Kariakoo. Wao wanauza bei ya simu.

View attachment 3000609

Mac Pro Display $1500 na Stendi yake inafika hadi $2000 (Tsh Mil 3.9 hadi Mil 5.1)

Hii ni display ya kile kidude cha kusugulia nyanya. Display tu.
View attachment 3000612


Airpods Pro $250 (Tsh 650,000)
Sijawahi tumia kwahiyo sijui mziki wake ila kutoa Laki 6 kisa utu tudude hapana.
View attachment 3000621

Polishing Cloth $20 (Tsh 52,000)
Kitambaa cha kusafishia kioo cha simu au laptop au ipad kinauzwa bei ivo.
View attachment 3000638

Apple Mouse $100 (Tsh 250,000)
Hii ni mouse kama unayoijua sema ya kuchaji.View attachment 3000648Hafu port ya kuchajia ipo chini kwahiyo ikiisha chaji hauwezi kutumia. Kha.View attachment 3000650

Mi labda sina hela, ila kununua bidhaa ya Apple naona kabisa napigwa. Ata iPhone najua ina nguvu ina balaa ila kama wanakuibia kwenye bidhaa zingine kwann wasikuibie kwenye iPhone.

Nimejiandaa kuambiwa nitafute hela.
Ukiona kitu hukielewi, ujue wewe sio mlengwa.

Walengwa wanaelewq
 
Huo ni uongo na wewe unajua, watumiaje wa iPhone ndo mnahangaika sana kutusema, kila siku ni vijembe tuu kuhusu android zetu, ila uzuri ni kwamba moto wa huko mnaujua, kila siku kuhangaika kuchaji visimu vyenu uchwara havikai hata na chaji.

Tuanze hapa, we unaweza kufanya nn kweny iPhone yako mm siwez kufanya kweny android yangu??
kmmko Kama huna uwezo wa kununua iPhone kaa kimya sio kufananisha iPhone na maredio yenu ya kichina.
 
Back
Top Bottom