Mnatumia njia gani kukabiliana na msongo wa mawazo (stress)?

Mnatumia njia gani kukabiliana na msongo wa mawazo (stress)?

Dah pole sana, Mimi pia huwa napitiaga kipindi kama hicho,huwa sitamani kufanya chochote lkn baada ya muda hali hiyo huwa inaisha,always time heal,jipe muda tu itaisha.
Asante sana ndugu
 
Asante sana ndugu naona nikielezea chanzo cha hayo yote hapa ndo ntazidi kujipa stress kabisa nahitaji faraja sana zaid
Pole mkuu.
Unahitaji faraja lakini hutaki kusema kinachokusibu, sio kila kitu kinacholeta msongo kinatakiwa kufarijiwa vingine inabaidi kuambiwa ukweli. Na hiyo kutaka Faraja pia inachangia hiyo hali unayopitia
 
Nadhani upo kwenye Anxiety ama Depression stage,siyo stress tena.
 
Niko na iyo hali sasa, najitibu kwa kuangalia series mwanzo mwisho. Ratiba yangu iko hivi, nikirudi job saa kumi na mbili nakoga na washa TV naweka series hadi nachukuliwa na usingizi. Movies, series ndio kilevi nikipendacho.

Nimenza na breaking bad, nimemaliza, black list, sasa naangalia shooter. Hii miezi ya mwisho wa mwaka kwangu mara nyingi inakuwa poa ila mara hii msala umeanza oktoba mwazoni hadi sasa. Nimejaribu kusolve na nashukuru njia hii ya kuangalia series imeniondolea stressess na imenipa muda wa kutafakari changamoto zangu nizitatue vipi.

Nashauri tafuta kilevi chako ulewe nacho, naomba unifahamu tafadhali, sikushauri unywe pombe tafuta kilevi chako.

Karibu
Asante sana ntajaribu maana hii hali huwa inaniondelea interest ya vitu vingi naweza nikasema nachek muvi ikifikia nusu natoa ntaingia social network kidogo tu ntazima data yaani nakuwa nusunusu
 
Natamani sikumoja tukutane wote wenye stress ...tusimuliane,tukumbatiane,tulie pamoja ...tukinyamaza tuambiane pole then tukubaliane kuacha mambo kama yalivyo then maisha yaendelee
Inaweza kuwa ni tiba kubwa sana maana hizi changamoto zinakukumba mpaka unahisi ni wew mwenyew tu ndo unakumbana nazo
 
Siku ya jana, leo na sijui hiyo kesho itakwendaje. Napitia msongo mkubwa sana wa mawazo, najaribu kujiliwaza na kujifariji pamoja na kujichanganya na watu ila nikikaa kidogo na kufikiri najikuta na rudi katika huzuni na mfadhaiko wa nafsi. Sio siri nakosa raha na hamu ya vitu vingi naomba mbinu ya kujikwamua.

Kama kuna mtu alishapitia hali hii naomben msaada. Pia mimi sio mlevi wala situmii kileo chochote.
Bakari nondo
 
Kuna stage ya stress ikifika hata mkuyenge hausimami kabisa.
Kweli.
Kuna stress ikikupata hata hamu za mapenzi huzipati. Na unaweza ukalichukia hilo tendo kabisa.
Kila kitu unachopendelea kukifanya huo wakati kinakuwa hakikupi furaha tena.
Hauwezi kusema utoke uende disko au sehemu ya starehe maana hata ukifika huko hata pombe hazipiti na mziki hauusikii.
Kukaa na watu napo unaona ni tabu.

Ilinipata hii hali. Ilikuwa sitoki kitandani na haimaanishi kwamba nilikuwa nina usingizi, hapana. Ni kulia tu, na kumeza antidepressant. Ikafika hatua nazo zikafeli.

Hii hali haitaki ufanye chochote. Kula ni kwa kujilazimisha na hapo kinakukaba. Simu ndio kabisa hautaki hata kuishika maana hamna cha kufurahisha huko. Nisiongelee nilikaa siku ngapi bila kugusa maji (lol). Nilikuwa kama kichaa. Sitoki ndani na siogi. Niliwaza hadi kufanya drugs. Bila kusema mara ngapi nilitamani kufa.

OP, chochote unachopitia, tafuta mtu uongee naye kabla hali haijawa mbaya.
 
Ninakushauri kwamba kama hali hiyo imedumu kwa mada wa zaidi ya siku 5 basi ni vema ukaenda hospitali.

Kuna msongo wa mawazo ambao utaondoka kwa kusaidiwa na dawa(antidepressants)
 
Back
Top Bottom