Mnawachukuliaje watu wa GNLD na Forever Living Products?

Swali langu kwao ambalo hawajawahi kunijibu ni kuwa kwa kuwa wanasema bidhaa zao zinatokana na mimea, mbegu na vitu asilia, kwa nini wasifanye kampeni ya kutumia mazao asilia badala ya kutengeneza "products"? Kweli mimi wamekula laki moja yangu ya kiingilio, lakini baada ya kutafakari kwa kina nimesema hakuna biashara ya aina hiyo zaidi ya utapeli kama wa DECI. Wamehangaika kuniita kwenye training mara mikutano, lakini nimeona ni upuuzi.
 
Yani wewe ndo fal.a kweli...Nyani haoni kundule...Hiyo "silly" ni kiswahili cha wapi..? Nilitegemea uwe mfano....

Cc to LIKUD

Hahaha na wewe umerudia kwa walewale sasa hiyo "pum.bavu" mbona na wewe umeirudia kwa kiingereza?
 
Last edited by a moderator:
Huwa siwaelewi kwa miaka yote ambayo nimekutana nayo.
 

Inasikitisha kusikia haya. Networking marketing, watu wamekuwa wapofu sana kiasa cha kushindwa kuona jinsi ambavyo wanapoteza mda na kuwapotezea watu muda kwa vitu visivyo na tija. Anakufuata mtu akidhani una level nae sawa ya ufikiri, kwa kweli si jambo la kuomba likukute. They will come in many forms, atleast dubbed them nicely....LOOSERS
 
Yote yaliyosemwa na wakuu hapo juu ni kweli kabisa, mimi yaliwahi kunikuta, rafiki yangu tuliyepoteana kwa muda mrefu siku moja tulikutana maeneo ya Bamaga canteen ya mzalendo.

Kama kawaida ya marafiki kuulizana habari za maisha na maendeleo huwa ni kawaida. Basi jamaa akaanza kunishawishi kwa kuniambia kuna mafanikio zaidi ya haya niliyonayo pindi tu nikijiunga na kampani yao ya Forever Living ambayo anataka kuni-nitambulisha kwa wahusika.

Nilikaribishwa siku ya jumanne jengo la Millenium Tower ghorofa ile ile ya Mzalendo pub, nilichokikuta huko ni mbwembwe zile zile za ushuhuda pamoja na video za watu waliofanikiwa na kuwa mabilionea wa kutisha lakini mwisho wa siku wakaniomba nijiunge na kundi lao.

Na ili niweze kutambullika wka uongozi wa juu lazima nitoe kiingilio cha shs. 500,000/= ili niweze kupata product zangu ambazo nitaziuza kwa muda wangu baada ya saa za kazi. Hata hivyo nilishtuka nikaingia mitini pamoja na jitihada za rafiki yangu kunishawishi ziligonga mwamba baada ya mimi kuona usumbufu na kubadili laini yangu ya simu.

Leo hii ninapoandika hivi jamaa kachoka ile mbaya maana hata nikimpita njiani naogopa kumsalimia asije nisumbua tena. Ila nimesikia kwa watu kwamba jamaa yangu alishindwa kuendelea na Forever Living sasa hivi yupo na kampuni moja mpya inaitwa GREEN...
 
Hahaha na wewe umerudia kwa walewale sasa hiyo "pum.bavu" mbona na wewe umeirudia kwa kiingereza?

Sikiliza wewe kichwa maji...Mimi sijajifunga na matumizi ya lugha umenielewa.... Sasa huyo -------- mwenzako yeye anajifanya kwamba lugha moja ndo inayotakiwa wakati hata yeye ana-mix....
 
Acheni kudharau kazi za watu kwani nyie mnafanya kazi gani zaidi ya kuonyesha madharau humu kama hutaki kitu kaa kimya maana kinaweza kuwa kina tija kwa mwingine sio lazima upende kila kitu kwenye hii dunia kuna watu wanafaidika sana tu.
 
hii ni kudanganya wazi wazi na kutumika vibaya ili kuingiza watanzania wenzako kwenye matatizo...uache kazi BOT au BARICK tena mhasibu, ukauze lotion au juice na food supplements. haniingii akilini :coffee: Sitaki kusikia kabisa hawo wanaojiita sijui forever. :A S thumbs_down:
 
Acheni kudharau kazi za watu kwani nyie mnafanya kazi gani zaidi ya kuonyesha madharau humu kama hutaki kitu kaa kimya maana kinaweza kuwa kina tija kwa mwingine sio lazima upende kila kitu kwenye hii dunia kuna watu wanafaidika sana tu.

wao ndio wana dharau, unajua kumfuata mtu mzima na heshima zake na kumueleza upu.thread kama huo ni dharau ya hali ya juu sana!
 
Wakuu hii biashara ya hawa jamaa ni sawa zile zinazoitwa pyramid schemes ambazo zimepigwa marufuku nchi nyingi, na sasa kwa kuzihalalisha wamezipa majina ya kutumia kama business networking. Mfumo wake ni ule ule wa pyramid kunakuwa na ncha na base pana. Mtu ambaye yuko kwenye ncha kupata faida kutokana na watu chini yake aliowaingiza kwenye biashara na manunuzi yao ya bidhaa. Kadiri base inavyopanuka ndio mapato yake huongezeka. Products za FLP ni supplements tu na si za tiba ni wizi na udanganyifu tu unaofanyika na bei zake ni za kinyonyaji. Kwanza hazitambuliki na WHO. WHO huratibu madawa ya tiba mbali mbali na kuhakikisha zinapatikana kwa bei zisizonyonya watu. Kwa pande wa FLP miongoni mwa wanzilishi wa hiyo biashara tz ni dada mmoja aishie UK ambaye ni shemeji na aliyewahi kuwa waziri mkuu mmoja wa tz, kwa nafasi ya shemeji yake aliweza kufanya biashara nzuri kwa vigogo wengi wenye fedha akaweza kuongeza watu wengi akanufaika na kuendelea kunufaika kwa kuwa na base kubwa kwenye hiyo pyramid
 
Hahahaha nimecheka sana na baadhi ya comment za members, ila hawa jamaa uwa wanaongea sana
 
Kuna DECI ambayo imekuwepo humu nchini mda mrefu tu (Forever Living Products).., ipo disguised as a Multi level marketing sijui nini.., eti una nunua dawa kwa shillingi laki saba then unaenda kuziuza sijui.., alafu eti ukimshawishi mwenzako kwenda kukunua hayo madawa eti ile pesa yake mnagawana.

Yaani dawa ambazo kiu halisia zina-gharimu elfu 20 we una-nunua kwa laki saba..!!!, then huyo unae-mleta na yeye akiweza kupata maboya wenzake wa kwenda kununua basi ile pesa yao mnagawana nyie up-liners wale and the pyramid goes on and on! huu si wizi kabisa..! kwanini hawapigwi mnyororo hawa.., kwanza hata sijui kama wana-mashine za EFD hawa!


 
Du iyo issue walinisomesha lkn nikachomoa kabisa
 
Toka niisikie hii kitu, imewabeba wengi lakini sijasikia wakilalamika kufirisika labda kama wanafanya siri.

Maana hawa jamaa kwa mbwembwe...wanataka mpaka mashuka yawe ya forever living.

Siwatofautishi sana na alovera maana nayo dah....wana mpaka malapa ya alovera kwendea bafuni eti wadudu wasichanganyike na sabuni.
 
Du iyo issue walinisomesha lkn nikachomoa kabisa

Kwa kweli hata mimi nilichomoa tena nilimchomolea rafiki yangu wa karibu kiaina kwani sababu ya kumheshimu nilimpa lugha ya kumdanganya ili asinielewe vby. Lakini kiukweli ile ni DECI nyingine hapa nchini
 

jamani msitukane vitu msivyojua. kama walikushauri ukakataa ni uamuzi wako lakini usiwatukane kuwa ni wizi wa ki-mbwa. najua watu wengi wanaouza hizi products na wanapata hela nzuri sana huwezi amini. wananunua na kuuza hizi products,wengine hadi wana maduka. jaribu kuuliza upate ukweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…