Mnawakumbuka watuma salamu maarufu redioni wa enzi hizo? Tujikumbushe kwa kuwataja...

Mnawakumbuka watuma salamu maarufu redioni wa enzi hizo? Tujikumbushe kwa kuwataja...

Huko Kenya walikuwepo Sura Mbili Kiango Momanya...bila kumsahau mtangazaji maarufu wa Salaam wa KBC idhaa ya Taifa Omuga Kabisae.

Vipindi vya salamu vya Kenya Broadcasting Cooparation idhaa ya kiswahili,hasa kuanzia saa kumi jioni baada ya taarifa ya habari vipindi hivyo vilikuwa vinaendeshwa na mtagazaji Omuga Kabisae... nilikuwa nafurahia jinsi mtuma salamu maarufu wa Kenya "Sura Mbili Kiyango Mumanyi" alivyokuwa akitajwa mara nyingi katika vipindi hivyo.
Source:https://www.jamiiforums.com/enterta...-kinakukumbusha-mbali-sana-3.html#post5133471
 
wapi Sita wa Sita, Mohamedi Kiyaiyai, Kung'ombe Chacha Morema Sokare Mohiri Obare (ukipenda Mohiri Obare bwaaana!), Chesco Mzee wa Mtanda, Mzee Lawena Nsonda (ee babaaaaa!), Dismas Chabela, etc.?
 
nimewakumbuka manka mushi na chesco mzee wa matunda. sijui wapo hai awa viumbe
 
Mi nakumbuka kipindi cha salam chapuchapu rfa by Godwine Gondwe
 
Jumanne Sebarua Tingisha, Mbago Mohammed Mbago kitu ya Mbeya, kulikuwa na jamaa wanajiita wataalamu wa kulima ming'oko (mpaka leo sijui ming'oko ni nini)

mihogo iliyokaushwa.............
angedizzle usichanganye na makopa. Ming'oko ni mizizi fulani ya porini inapatikana sana maeneo ya kusini mwa Tanzania ambayo huliwa baada ya kuchemshwa. Ukifika Lindi na kuendelea huko mbele utaiona watu wanachuuza kwenye masinia
 
Last edited by a moderator:
Umetukumbusha mbali lakini unawakumbuka ZAKARIA NDENFO MWINDA TEMBO,KONDO ALI KONDO,CHIVALAVALA CHIVALAVALA WA MAHUTA NEWALA NA MANASE NKAMBAKO WA ARIA C DODOMA.Sebarua tingisha mara ya mwisho nilonana nae magomeni mapipa akaniambia sasa yeye sio tingisha tena bali anatingishwa baada ya kuzulumiwa basi aina ya fuso alilo nunua kwa kiinua mgongo alichopewa tanesco kwa sasa yuko kwao Gologolo Lushoto

"Maliki Lumaliza wa misugusugu kibaha" yupo magomeni mapipa shibamu anauza mihogo!
 
Zamani kila vipindi
vya salam kwa njia ya simu redioni majina haya yalikua maarufu sana.
Charles imalaya kama simba, kung'ombe chacha sukari muhilo obaré, basu
basanga basu,baba dula one, chesco mzee wa matunda, imma kulaya, suzy
ngodoki, manka mushi, jumane sebarua tingisha. Dah siku hizi majina haya
yamefunikwa sana redion.

Mkubwa umewasahau watu kama Maalimu litumbi, Papa Osama.
 
Jumanne Sebarua Tingisha, Mbago Mohammed Mbago kitu ya Mbeya, kulikuwa na jamaa wanajiita wataalamu wa kulima ming'oko (mpaka leo sijui ming'oko ni nini)

Ming'oko kwa wakazi wa LIndi,Masasi Mtwara watailelewa ni chakula maaarufu humo like mihogo midoooogo
 
angedizzle usichanganye na makopa. Ming'oko ni mizizi fulani ya porini inapatikana sana maeneo ya kusini mwa Tanzania ambayo huliwa baada ya kuchemshwa. Ukifika Lindi na kuendelea huko mbele utaiona watu wanachuuza kwenye masinia



Kweli Mkuu usemacho

Pia Dar soko la Tmk Stereo huwa inapatikana.
 
Last edited by a moderator:
Zakaria Ndemfoo, wapi utamkosa ? kuanzia RTD, DW, Afrika kusini, Radio Japan, KBC, ILIHALI KUNA IDHAA YA KISWAHILI YEYE ni kwake,
Kuna kunguru Muoga, Isa Hassan Majeshi,
 
wapi Sita wa Sita, Mohamedi Kiyaiyai, Kung'ombe Chacha Morema Sokare Mohiri Obare (ukipenda Mohiri Obare bwaaana!), Chesco Mzee wa Mtanda, Mzee Lawena Nsonda (ee babaaaaa!), Dismas Chabela, etc.?

hao kina Chesco ni kizazi cha Dot com !
 
Back
Top Bottom