Uchaguzi 2020 Mnyika: Sakata la Wabunge wa Viti Maalum limehusisha mfumo wa Serikali kufifisha ajenda ya 'Uchaguzi haramu'. Ahoji Nusrat kuteuliwa akiwa gerezani

Wanasiasa wote wa Tz iwe opposition or chama tawala wanapambania matumbo yao,huwa nashangaa watu humu mishipa inawatoka kisa hayo mavyama lakini wananufaika wengine,jinga kabisa......poleni mliovuliwa nguo......hata Shangazi anayejifanya mwanaharakati,leo akiteuliwa kuwa DC au RC atakubali na mtaishia kushangaa tu
 
Haki kuifadhiwa haizuii haki hiyo kuendelea kupiganiwa.Hata wakoloni waliifadhi haki za waafrika ila mwisho wa siku waliziachia.
 
Kweli wazazi waliuza ng'ombe ili wapeleke ng'ombe Shule. Hivi wewe huoni kinyaa serikali nzima inashiriki uhalifu wa kugusbi nyaraka na kudanganya umma?
Yote haya juu ya nini?
Ndugu yangu tumia akili angalau kidogo...jifunze kupambanua mambo...usikariri tu mambo...kwa mawazo yako serikali imefoji...hivi Mdee na wenzake wanaweza kukubali serikali ifoji halafu wao waapishwe?

Kama ni kufoji kwanini usifikirie kuwa pengine baadhi ndani ya Chadema wamefoji saini za kiongozi wao na kuwasilisha majina bungeni?!

Halafu hivi unadhani Mdee na wenzake wanaweza kwenda kuapishwa Bila baraka za uongozi wa juu wa Chadema? Mimi nawasikitia Sana Chadema kwa kweli...mkiaminishwa kuwa kulikuwa na wizi kwenye uchaguzi na nyie mnaimba hivyo hivyo...Lissu akiimba huu siyo uchaguzi Bali ni uchafuzi na nyie mnakuja na msamiati huo huo..yaani mnachezewa Kama mazezeta...hamuwezi kutumia akili zenu na kuchambua mambo...mnapelekeshwa tu...uchaguzi huu ulikuwa ni uchaguzi halali.

Kibaraka na msaliti alishindwa kihalali kabisa...hakukuwa na wizi wa kura..nyie mitandaoni na kwenye vichwa vyenu ndio mnaoamini kuwa ulikuwepo wizi. Sasa akina Mdee happy bungeni wamewaacha na wamekwenda kupata milioni tano kwa mwezi.

Lissu amekwenda kwa mabwana zake ulaya...mtaaminishwa sijui ICC, nakuthibitishia hakutakuwa na ICC Wala mjomba wake...Tanzania pia haitakatiwa misaada...endeleeni kuteseka na kusononeka kwa mawazo...Na hakuna Mtanzania atakayeandamana.
 
Kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi na kanuni zake orodha ya wabunge watarajiwa wa viti maalumu yanapaswa kupelekwa lini NEC na vyama vya siasa?

Je, ni kabla ya tarehe ya uchaguzi mkuu au baada?

Nakumbuka uchaguzi wa 2015 Esther Bulaya alikuwa kwenye orodha ya wabunge wa viti maalumu watarajiwa kabla hajamshinda mzee Wassira jimboni Bunda.

Tusimlaumu Dobi kaniki ni rangi yake.

Maendeleo hayana vyama!
 
Hongera kwa kuandika pepa. Sijasoma chochote humo.
 
chadema ilipitisha wanawake 68 kugombea majimboni hebu tuambie hao wanawake nani aliwadhalilisha kingono na wapi mpaka kuwapa hizo nafasi?
Unaujua mchakato wake?Kaa kimya kama hujui,dada zetu wanadhalilishwa
 
Sio uongozi wa chama....
Nchi hii inaendeshwa ki dikteta.. Unafikiri hao Covid 19 wameapa kwa hiari?
Kuna mwingine alikua jela Uhuru wake unatakana na kukubali ubunge
Halima baada ya kukubali kesi Zake zote zimefutwa.. Kama nchi taasisi zote kubwa zipo kisiasa unategemea nini
Mahakama..TRA.JESHI LOTE.. TAKUKURU.. USALAMA WA TAIFA
Hizi idara zote zipo kisiasa sana... Sasa unategemea maajabu gani?
 
Punguza stress mkuu utakufa bure kunywa maji kidogo. Hebu angalia mwenye chama alivyo tweet hapa chini!!

 
Wewe bongo yako hamna kitu kabisa. Unafikiri hayo ya ngono na mambo mengine hayapo kwa CCM?
Yaani watu wengine mnatia aibu, kama hujui siasa kaa kimyaaa.
 
Punguza stress mkuu utakufa bure kunywa maji kidogo. Hebu angalia mwenye chama alivyo tweet hapa chini!!

View attachment 1634586
Halima hana jinsi tangu jiwe kaingia madarakani Leo Ndio mara ya kwanza kalala bila kesi
Sina ubaya nao pia naamini alikua hana jinsi
If you can't fight them just join them
Huyu bint kweli kateseka sana
Kuanzia leo hutamuona tena mahakama ya kisutu
 
Chadema wasikurupuke.

Kuna jambo wanapaswa kufikiria sana kabla ya kwenda hatua anazosema Mnyika...

Nimeona kule twitter Heche anasema atashiriki Kamati Kuu. Ni vizuri wakikaa kama kamati kuu waangalie mahala pa kurekebisha kabla hawajatimuana kwani ot will be loong battle from to within.

HIVI LILE TAMKO LA KUTOTAMBUA MATOKEO YA UCHAGUZI LILITOKANA NA UAMUZI WA KAMATI KUU?
 
Shetani akisisitiza ufanye jambo fulani, jiulize mara mbili.

Waliosema wapinzani ni wa kuwafutilia mbali, leo wanalalamika kwanini hawaendi Bungeni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…