Uchaguzi 2020 Mnyika: Sakata la Wabunge wa Viti Maalum limehusisha mfumo wa Serikali kufifisha ajenda ya 'Uchaguzi haramu'. Ahoji Nusrat kuteuliwa akiwa gerezani

Walioapishwa waliteuliwa na Chama? Tumia akili ndogo kuelewa na kujibu hoja. Kama hakuna ulazima wa kuteuliwa na Chama basi hakuna sababu ya kutaja kwamba wanatoka chama fulani. Watekeleze wajibu wao kwa namna yao wanayojua lakini siyo hiyo ya sasa
Majina ya wanawake wa viti maalum huchakatwa mapema hata kabla ya uchaguzi mkuu. Hili ni swala la kisheria zaidi na mdee ni lawyer.
 
Hebu tunaomba utupatie kifungu hicho cha sheria.
Katibu mkuu wa chama sio tu anatakiwa apeleke orodha bali anatakiwa apeleke fomu namba 8(d) kwa kila aliyekuwepo kwenye orodha ikiwa imesainiwa na katibu mkuu. Tume ya Taifa ya uchaguzi ilituletea fomu hizi hapa(Anazonyesha) ili tukishateua kama tungeteua, tupeleke orodha ya majina 113 kwa ujumla tukiwa tumejaza hizi fomu.

Mimi kama katibu mkuu, hakuna fomu yoyote ya mtu yoyote niliyowahi kuijaza popote kuthibitisha uteuzi wa yoyote.

Mchakato huo wote haukufatwa, kwa hiyo kwa tafsiri nyepesi, kilichofanyika ni biashara haramu ya kughushi ambayo imehusisha mfumo wa kiserikali, tume ya Taifa ya uchaguzi na kwakweli niseme vilevile imehusisha hao waliokwenda kuapa bila ridhaa ya chama na bila baraka za chama na bila kupishwa kwa mamlaka halali za chama.
 

Acha mishipa

Mbowe anasemaje?
 
Namekuuliza utuletee kifungu cha sheria kinachosema hayo.
Sheria gani inatamka hivyo!?
 
Katiba ipi inasema unamfukuza mtu bila kujitetea ninyi vilaza??
 
Namekuuliza utuletee kifungu cha sheria kinachosema hayo.
Sheria gani inatamka hivyo!?
Kwa katiba ya CHADEMA, mamlaka ya uteuzi wa wabunge yapo kwa kamati kuu ya chama. Kamati kuu ya chama haijawahi kufanya kikao cha kuteua majina ya wabunge wa viti maalum wakati wowote.
 
Niko pamoja nao hao wamama, itoshe kusema kuwa CDM mumeheshimiwa na mumeonekana mna umuhimu kujenga Taifa pamoja na misaada ndo maana wengine wametolewa gerezani ili waungane na familia zao, huo umuhimu wenu ulionekana naomba hao wamama na wadada wasifukuzwe uanachama maana wote wamekipambania chama onesheni kwa vitendo msamaha kwao ili msijigawe bali mjenge.
 
Katiba naSheria za chama changu CHADEMA zifuatwe, wenye kutaka vyeo na pesa, waunge juhudi tu watuachie chama chetu.
Kamati kuu fukuza hao wote waende kwenye pesa wakale raha.

Nakupenda CHADEMA kwa moyo wangu wote✌🏽✌🏽✌🏽
 
Why kama mlijua hana makosa, mkamtesa kwa kumuweka rumande muda wote huo halafu mnakuja kumpa rushwa ya kumpa viti maalum ili kumfunga mdomo, kinyume na taratibu za chama chake..?? Corrupt system
 
maswali mazito haya duuu! haswa kuachiwa na kuapishwa! huu mchongo mzima una baraka zote kutoka juu
 
Acha Chadema Ife ili kizaliwe Chama kingine bhana!!

Imekuwa Chadema, Chadema, Chadema utadhani wimbo wa Taifa bhana!!

Kuna mtu hapa Baba au mama yake anaitwa Chadema?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…