Uchaguzi 2020 Mnyika: Sakata la Wabunge wa Viti Maalum limehusisha mfumo wa Serikali kufifisha ajenda ya 'Uchaguzi haramu'. Ahoji Nusrat kuteuliwa akiwa gerezani

Uchaguzi 2020 Mnyika: Sakata la Wabunge wa Viti Maalum limehusisha mfumo wa Serikali kufifisha ajenda ya 'Uchaguzi haramu'. Ahoji Nusrat kuteuliwa akiwa gerezani

Walioapishwa waliteuliwa na Chama? Tumia akili ndogo kuelewa na kujibu hoja. Kama hakuna ulazima wa kuteuliwa na Chama basi hakuna sababu ya kutaja kwamba wanatoka chama fulani. Watekeleze wajibu wao kwa namna yao wanayojua lakini siyo hiyo ya sasa
Majina ya wanawake wa viti maalum huchakatwa mapema hata kabla ya uchaguzi mkuu. Hili ni swala la kisheria zaidi na mdee ni lawyer.
 
Hebu tunaomba utupatie kifungu hicho cha sheria.
Katibu mkuu wa chama sio tu anatakiwa apeleke orodha bali anatakiwa apeleke fomu namba 8(d) kwa kila aliyekuwepo kwenye orodha ikiwa imesainiwa na katibu mkuu. Tume ya Taifa ya uchaguzi ilituletea fomu hizi hapa(Anazonyesha) ili tukishateua kama tungeteua, tupeleke orodha ya majina 113 kwa ujumla tukiwa tumejaza hizi fomu.

Mimi kama katibu mkuu, hakuna fomu yoyote ya mtu yoyote niliyowahi kuijaza popote kuthibitisha uteuzi wa yoyote.

Mchakato huo wote haukufatwa, kwa hiyo kwa tafsiri nyepesi, kilichofanyika ni biashara haramu ya kughushi ambayo imehusisha mfumo wa kiserikali, tume ya Taifa ya uchaguzi na kwakweli niseme vilevile imehusisha hao waliokwenda kuapa bila ridhaa ya chama na bila baraka za chama na bila kupishwa kwa mamlaka halali za chama.
 
Katibu mkuu wa chama sio tu anatakiwa apeleke orodha bali anatakiwa apeleke fomu namba 8(d) kwa kila aliyekuwepo kwenye orodha ikiwa imesainiwa na katibu mkuu. Tume ya Taifa ya uchaguzi ilituletea fomu hizi hapa(Anazonyesha) ili tukishateua kama tungeteua, tupeleke orodha ya majina 113 kwa ujumla tukiwa tumejaza hizi fomu.....

Acha mishipa

Mbowe anasemaje?
 
Katibu mkuu wa chama sio tu anatakiwa apeleke orodha bali anatakiwa apeleke fomu namba 8(d) kwa kila aliyekuwepo kwenye orodha ikiwa imesainiwa na katibu mkuu. Tume ya Taifa ya uchaguzi ilituletea fomu hizi hapa(Anazonyesha) ili tukishateua kama tungeteua, tupeleke orodha ya majina 113 kwa ujumla tukiwa tumejaza hizi fomu....
Namekuuliza utuletee kifungu cha sheria kinachosema hayo.
Sheria gani inatamka hivyo!?
 
0D2B0E54-B350-46A3-A68E-BA989CC2DECE.jpeg
Katibu Mkuu wa CHADEMA anazungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mchakato wa wabunge wa Viti Maalum ambao wameapisha siku ya jana tarehe Novemba 24, 2020.

Tumewaita kuwaeleza kwamba CHADEMA hakijateua wabunge wa viti maalum wala hakijawasilisha orodha yoyote Tume ya Uchaguzi ya uteuzi wa wabunge wa viti maalum

Mimi kama Katibu Mkuu wa Chama sikuwahi kujaza fomu yoyote, kumthibitisha mtu yeyote mahali popote, kilichofanyika ni biashara haramu ya kugushi iliyohusisha mfumo wa kiserikali.

Mawasiliano yangu ya mwisho na Tume ya Uchaguzi zilikuwa ni barua 2, Nov 9 , niliiandika baada ya Mkurugenzi wa NEC kunukuliwa na vyombo vya habari kwamba CHADEMA imewasilisha orodha ya wabunge wa viti maalum na yeye amekwishaipeleka bungen

Kwa katiba ya CHADEMA mamlaka ya uteuzi wa wabunge yako kwa kamati kuu ya chama, na kamati kuu ya chama haijawahi kufanya kikao cha uteuzi wa majina ya wabunge wa viti maalum na mimi Katibu Mkuu sijawahi kuwasilisha orodha yoyote

Katibu Mkuu, John Mnyika amewataka wabunge wote walioapishwa kuwa wabunge wa Viti Maalum kufika kwenye ofisi za Makao Makuu ya Chama siku ya Novemba 27, saa mbili asubuhi bila kukosa kwa ajili ya utaratibu mwingine.

Mwanachama wetu aliyekuwa na kesi ya jinai ya kubambikiwa kwa muda mrefu Nusrat Hanje alitolewa gerezani tarehe 23 Novemba na mfumo ili watimize adhma yao.

Katibu Mkuu amesema kwamba wabunge wote walioapishwa Novemba 24 wamewekwa na mfumo na hawana baraka za chama cha Demokrasia na Maendeleo.

Kauli iliyotolewa jana na kumhusisha Mwenyekiti, Freeman Mbowe haina ukweli. Mbowe ataongoza kamati kuu na itawasikiliza wahusika. Kati ya walioapishwa kuna wajumbe wa kamati kuu wanafahamu uteuzi haukufanyika na wanajua wameshiriki biashara haramu

==========

JOHN MREMA: Mbele yetu katibu mkuu wa chama, John John Mnyika akiwa na mkurugenzi wa Itikadi, Uenezi na mahusiano ya mambo ya nje na msemaji mkuu kwa siku ya leo atakuwa katibu mkuu wa chama.

JOHN MNYIKA: Tarehe 28 Oktoba kulifanyika uchafuzi ulioitwa uchaguzi mkuu ambapo mtakumbuka kati ya mambo yaliyofanyika ni hujuma za wazi za mfumo wa kiserikali ukihusisha tume ya Taifa ya uchaguzi kupika matokeo ya uchaguzi.

Chama cha demokrasia na maendeleo hakijateua wabunge wa viti maalum au wagombe ubunge viti maalum wala hakijawasilisha orodha yoyote tume ya Taifa ya uchaguzi ya uteuzi wa wabunge wa viti maalum.

Kwa katiba ya CHADEMA, mamlaka ya uteuzi wa wabunge yapo kwa kamati kuu ya chama. Kamati kuu ya chama haijawahi kufanya kikao cha kuteua majina ya wabunge wa viti maalum wakati wowote.

Pili katibu mkuu wa chama ambae ndie mwenye mamlaka ya kimawasiliano ya kuwasiliana na tume ya Taifa ya uchaguzi, katibu mkuu wa chama sijawahi kuwasilisha orodha yoyote tume ya Taifa ya uchaguzi ya wanaoitwa waliopendekezwa wabunge wa viti maalum.

Katibu mkuu wa chama sio tu anatakiwa apeleke orodha bali anatakiwa apeleke fomu namba 8(d) kwa kila aliyekuwepo kwenye orodha ikiwa imesainiwa na katibu mkuu. Tume ya Taifa ya uchaguzi ilituletea fomu hizi hapa(Anazonyesha) ili tukishateua kama tungeteua, tupeleke orodha ya majina 113 kwa ujumla tukiwa tumejaza hizi fomu.

Mimi kama katibu mkuu, hakuna fomu yoyote ya mtu yoyote niliyowahi kuijaza popote kuthibitisha uteuzi wa yoyote.

Mchakato huo wote haukufatwa, kwa hiyo kwa tafsiri nyepesi, kilichofanyika ni biashara haramu ya kughushi ambayo imehusisha mfumo wa kiserikali, tume ya Taifa ya uchaguzi na kwakweli niseme vilevile imehusisha hao waliokwenda kuapa bila ridhaa ya chama na bila baraka za chama na bila kupishwa kwa mamlaka halali za chama.

Chama inabidi kichukue hatua, katiba yetu inasema hatua zozote zisichukuliwe bila ya wahusika kuitwa, kujieleza. Sasa kwa kuwa hili jambo ni la dharula, chama kitatumia utaratibu wa dharula katika kushughulika na jambo hili na tutaongozwa na kanuni za chama.

Kwa kuwa mamlaka ya jambo hili ni kamati kuu ya chama, naomba kuwatangazi kwamba tumeitisha kikao cha kamati kuu ya chama maalum, kitafanyika siku ya Ijumaa tarehe 27 hapa jijini Dar es Salaam.

Pamoja na kuwa tutawaandikia wahusika, ili kusitokee kisingizio kwa yeyote kwamba hakuitwa, hakupata taarifa ya kuitwa naomba kutangaza 'Public notice' kupitia vyombo vya habari kwa wanachama wetu 19 walioshiriki kwenda kula kiapo jana tarehe 24 kufika makao makuu ya chama bila kukosa.

Kuna tukio la mwanachama wetu ambae ni kiongozi wa baraza la baraza la vijana la CHADEMA, Nusrat Hanje ambae amesota ndani kwa kesi ya kubambikiziwa kwa siku 133 akiwa mahabusu na leo tarehe 25 mahakama kuu ndio ilikuwa inakutana kutoa uamuzi juu ya rufaa ambayo amekata baada ya kusota ndani kwa muda mrefu.

Kituko kinachoashiria mfumo kuhusika katika huu mchezo, tarehe 23 usiku alikwenda kutolewa gerezani ili kesho yake apelekwe kuapa na alitolewa na mfumo bila hata kuzingatia masharti ya kisheria. Tunashkuru kwamba mwanachama wetu na kiongozi wetu ametoka baada ya kusota ndani kwa muda mrefu lakini mfumo ulimtoa ili kutekeleza malengo yao.

Sasa Ndugai amesema alipelekewa majina tarehe 20 Novemba na tume, Nusrat Hanje alietolewa gerezani tarehe 23 Novemba, uteuzi wa tume unasema umefanyika tarehe 20, fomu yake aliijaza lini, hakimu aliemuapisha alikuwa wapi kabla ya tarehe 20 tume ilipomteua mambo ambayo yanadhihirisha wazi kwamba hili jambo ni kazi ya mfumo.

Lengo la wazi la mfumo ni kutaka kufifisha ajenda ya kwamba Tanzania ilifanya uchaguzi haramu tarehe 28 Oktoba ulioitwa uchafuzi wakati umma ukishinikiza, jamii ya kimataifa ikishinikiza, bunge likionekana la chama kimoja ili kujaribu kulipa uhalali serikali ya illegitimate president Magufuli ikaamua kushiriki huu mchezo haramu wa kuhusisha tume, spika wa bunge na hatimaye tumefika hapa tulipofika.

Nitoe rai kwa watanzania, jambo hili lisitutoe watanzania kwenye mjadala mkubwa na muhimu zaidi kwamba tarehe 28 Oktoba kulifanyika uchafuzi na kwamba sisi tunataka uchaguzi ufanyika upya chini ya tume huru ya uchaguzi.

Sisi tunaotaka hilo tunatengenezewa mazingira ya mjadala kuhama, umma wa watanzania usikubali kuingizwa kwenye mtego wa dola wa kuhamisha mjadala na kufifisha hasira za wananchi.

Kauli iliyotolewa jana wakati wa kuapishwa iliyotaka kujenga ishara kama mwenyekiti wa chama, Freeman Mbowe alihalalisha hili linaloendelea, hii kauli sio ya kweli na mwenyekiti wa chama ndie atakaeongoza kikao cha kamati kuu ya chama kitakachofanyika tarehe 27.
Katiba ipi inasema unamfukuza mtu bila kujitetea ninyi vilaza??
 
Namekuuliza utuletee kifungu cha sheria kinachosema hayo.
Sheria gani inatamka hivyo!?
Kwa katiba ya CHADEMA, mamlaka ya uteuzi wa wabunge yapo kwa kamati kuu ya chama. Kamati kuu ya chama haijawahi kufanya kikao cha kuteua majina ya wabunge wa viti maalum wakati wowote.
 
Niko pamoja nao hao wamama, itoshe kusema kuwa CDM mumeheshimiwa na mumeonekana mna umuhimu kujenga Taifa pamoja na misaada ndo maana wengine wametolewa gerezani ili waungane na familia zao, huo umuhimu wenu ulionekana naomba hao wamama na wadada wasifukuzwe uanachama maana wote wamekipambania chama onesheni kwa vitendo msamaha kwao ili msijigawe bali mjenge.
 
Katiba naSheria za chama changu CHADEMA zifuatwe, wenye kutaka vyeo na pesa, waunge juhudi tu watuachie chama chetu.
Kamati kuu fukuza hao wote waende kwenye pesa wakale raha.

Nakupenda CHADEMA kwa moyo wangu wote✌🏽✌🏽✌🏽
 
Niko pamoja nao hao wamama, itoshe kusema kuwa CDM mumeheshimiwa na mumeonekana mna umuhimu kujenga Taifa pamoja na misaada ndo maana wengine wametolewa gerezani ili waungane na familia zao, huo umuhimu wenu ulionekana naomba hao wamama na wadada wasifukuzwe uanachama maana wote wamekipambania chama onesheni kwa vitendo msamaha kwao ili msijigawe bali mjenge.
Why kama mlijua hana makosa, mkamtesa kwa kumuweka rumande muda wote huo halafu mnakuja kumpa rushwa ya kumpa viti maalum ili kumfunga mdomo, kinyume na taratibu za chama chake..?? Corrupt system
 
Maswali yafuatayo yanapaswa kujibiwa na Mbowe/Mnyika:

1. Nani amepeleka Orodha ya Majina ya Wabunge wa Viti Maalum NEC?
2. Orodha hiyo imepelekwa kwa njia gani?
3. Kama msimamo wa chama na wa Katibu Mkuu ni kuwa Orodha haikupelekwa, walioapishwa jana walipatikanaje?
4. Hatua gani zinachukuliwa na CHADEMA ikiwa usaliti umetokea?
5. Ilikuwaje Nusrat Hanje aachiwe tu kutoka mahabusu na asubuhi yake aapishwe kuwa Mbunge wa Viti Maalum?
6. Nani yuko nyuma ya suitafahamu hii nzima ndani ya CHADEMA na anashughulikiwaje?
maswali mazito haya duuu! haswa kuachiwa na kuapishwa! huu mchongo mzima una baraka zote kutoka juu
 
Acha Chadema Ife ili kizaliwe Chama kingine bhana!!

Imekuwa Chadema, Chadema, Chadema utadhani wimbo wa Taifa bhana!!

Kuna mtu hapa Baba au mama yake anaitwa Chadema?
 
Back
Top Bottom