Mohammed Shabiby: Namna ya kupunguza bei za mafuta kwa 50% ya bei za sasa

Huu ushauri ni mzuri lkn suala la mafuta hata nchi kubwa zinapata taabu je nao wanauziwa na bandari yetu au
Nchi gani kubwa hizo zinazopata taabu na suala la mafuta?

Na nini hasa maana ya "nchi kubwa" na "nchi ndogo?" na uhusiano wake na hiki tunachojadili hapa?

Kuna nchi kama Luxembourg, Israel, Quatar, Austria nk ni nchi dogo sana lakini ni nchi zenye chumi imara na nchi zenye maisha nafuu sana kwa wananchi wao..!

Na kwa taarifa yako mambo haya hayako hivyo unavyofikiri..

Haya mambo ya uendeshaji wa uchumi wa nchi kwa manufaa nafuu ya maisha kwa wananchi ni suala la SERA na MIPANGO BORA..

Huwezi kuwa na mipango na sera bora bila kuwa na MFUMO BORA wa UTAWALA unaozalisha VIONGOZI BORA wenye kutumia bongo zao vizuri na wasio WABINAFSI (Selfish)..

Tatizo la nchi yetu ya Tanzania wala hata haliko huko unakofikiri wewe..

Tatizo liko kwenye ubinafsi wa viongozi wetu. Na viongozi hawa hutumia matatizo kama haya kujinufaisha kisiasa kwa gharama ya wananchi..!!
 
Ili mafuta yapungue bei tuazimie viongozi wote wanaopata mafuta bure kwa magari yao iondolewe kwani mishahara yao inajitosheleza watumie magari wakiwa kazini na si kwa matembezi binafsi. Kodi za nyumba, umeme maji entertaiment allowance zifutwe wabaki kama wananchi au wafanyakazi wa kawaida. Wastaafu wote wenye marupurupu haya yatolewe kwani wanalipwa pensheni inayojitosheleza. Hakuna haja ya kujengea nyumba viongozi kwani wana mishahara mikubwa waishi kama wafanyakazi wengine. Ikifanyika hivi tutasave hela nyingi sana
 
Bulk procurement faida yake ninayoiona ni control ya kodi.

Ila faida ya kuacha watu waagize wenyewe ni ushindani wa bei hapa ananufaika mlaji wa mwisho.

Sasa ni jambo la kuchagua kati ya hayo mawili.

Kodi kwa serikali au faida ya soko huria.
Hakuna mwagizaji binafsi atakayeweza kukwepa kodi.
 
Tafakari
 
Yaan hao wezi na majambazi ndio huwa wanamtukana JPM.Na pia ndio wanashangilia kifo cha JPM.Kipara na Msoga katika ubora wao.
Huyo unayemwita Kipara ndiye aliyechangia pakubwa ushindi wa Magu. Sasa walishindana wapi wanajuana wenyewe. Magu alivyokuwa mtu wa visa sidhani kama hata ubunge angeupata huyu kama angejua madhambi yake.
 
Tatizo ni wenye dhamana wana maslahi mapana na mifumo iliyopo, Bwana Shabiby ujumbe mzuri ila take it back hakuna wa kukuelewa.
 
Kumbe Russia ni giant
Kabana mafuta kidogo dunia nzima inatetema kama Mayele..
Mafuta ya Russia yanarandaranda bahari kuu hamna wanunuzi- hofu ya kukiuka masharti ya vikwazo iliyowekea urusi inazuia nchi nyingi kununua mafuta ya Vladimir dikteta Putin.
 
Hii itakuwa nzuri sana, bata mimi nitajitoa kwenda kununu mafuta ya urusi maana bei yake iko chini
 
very sensible.
P

Shabiby kuna kitu hajakisema vizuri kuhusu uagizaji wa mafuta wa mtu mmoja mmoja, ubora wa mafuta unakuwa substandard sana, wengi wanafanya mix za uhuni, wanaleta mafuta with low Octane rating, alafu wanatuulia gari zetu.

Shabiby ana point, ila waagizaji binafsi wengi sio waaminifu, wanaleta mafuta with low quality, alafu wanahonga watu wa vipimo, mafuta yanapita alafu yanaua engine zetu

 
Hayo mafuta yaliyowekewa vikwazo na mafuta ya wizi (black market oil) serikali haiwezi kuonekana inahusika kuyanunua maana itawekewa vikwazo. Labda serikali iwaachie wafanyabiashara binafsi wayaingize kama bidhaa za magendo halafu wayauze ndani ya nchi. Na hao wafanyabiashara binafsi sidhani kama watapunguza bei sana, watawalangua na kuwapiga tuu wananchi.
 
Tatizo la watanzania ni ubinafsi. Hivi mtu umeajiriwa una mshahara unakubalije kupokea rushwa? Yani sisi wananchi tunalipa gharama ya watu wachache ambao sio waaminifu. Shabiby yupo sahihi kabisa, watendaji wa mamlaka ndio wenye matatizo.
 
Naunga mkono hoja, kusema ukweli, japo Blaza wangu kuna vitu alisaidia, ila pia kuna vitu aliharibu, sisi wasema kweli, hatukunyamaza, tulisema...
P
 
Ole wako Mmarekani ajue umeenda kununua mafuta Urusi, nakuambia utayarudisha ulikoyatoa mwenyewe,
Hapa ndo namkumbuka Magufuli, angekuja hadharani na kusema hapangiwi na mabeberu tungenunua mafuta Russia kwa bei ya chini
 
kweli , lakini EWURA si wapo? inatakiwa wawadhibiti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…