MOI watoa tamko kuhusu uvunjifu wa maadali uliofanywa wodini. Mgonjwa aomba radhi

Menejimenti ya Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) imetoa ufafanuzi kuhusu uvunjifu wa maadili uliofanywa na Mgonjwa (jina limehifadhiwa) na anayedaiwa kuwa Mpenzi wake (jina limehifadhiwa) ndani ya wodi (3A) siku ya Jumapili mchana tarehe 9/07/2023 ambapo katika uchunguzi wa awali mgonjwa amekiri kufanya tendo la busu la midomo na ndimi na Mpenzi wake katika mazingira ya kuumwa ndani ya Hospitali kitu ambacho ni kinyume cha maadili ya kitanzania.

“Menejimenti imebaini kwamba Mpenzi wa Mgonjwa huyo si Mtumishi wa Taasisi ya MOl, aidha tukio hilo liligunduliwa na Muuguzi aliyekuwepo wodini ambapo alichukua hatua ya kuzuia Wahusika kuendelea na kitendo hicho, Menejimenti inaendelea kuchukua hatua zaidi kwa Wahusika”

“Uchunguzi zaidi umebaini pia wakati vitendo vinaendelea kuna Mgonjwa jirani (jina linahifadhiwa) ambaye alisharekodi video, Menejimenti ya MOl inalaani kitendo hicho cha uvunjifu wa maadili kilichofanywa na Mgonjwa huyo pamoja na Mpenzi wake, vilevile Menejimenti inalaani na kukemea kitendo cha kurekodi video wodini na kutuma kwenye mitandao ya kijamii kilichofanywa na Mgonjwa jirani”

“Matukio haya yote ni kinyume na mwongozo wa Wizara ya Afya unaozuia kufanya matendo ya uvunjifu wa maadili kwa mgonjwa na kurekodi video wodini, Menejimenti inaendelea kuchunguza zaidi tukio hili ili kujiridhisha kuwa hapakuwa na uzembe katika kusimamia usalama wa Wagonjwa wakati Ndugu wanawatembelea Wagonjwa wodini”

Baada ya Tamko hili Mgonjwa aomba radhi
MGONJWA aliyelazwa katika Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) ambaye video yake imesambaa kwenye mitandao ya kijamii ikionesha akibusu midomo na ndimi na mpenzi wake wodini ameomba radhi kwa kitendo hicho na kuahidi hatorudia tena.

Taarifa iliyotolewa na Afisa Habari wa Moi, Patrick Mvungi inasema kuwa kitendo hicho kimefanyika katika Wodi 3A siku ya Jumapili mchana Julai 9, 2023.

Aidha, amesema katika uchunguzi wa awali mgonjwa amekiri kufanya tendo la busu la midomo na ndimi na mpenzi wake katika mazingira ya kuumwa ndani ya Hospitali kitu ambacho ni kinyume na maadili ya Tanzania.

“Menejimenti imebaini kwamba mpenzi wa mgonjwa huyo si mtumishi wa Moi.”Amesema

Amesema, tukio hilo liligunduliwa na muunguzi aliyekuwepo wodini ambapo alichukua hatua ya kuzuia wahusika kuendelea na kitendo hicho na menejimenti inaendelea kuchukua hatua zaidi kwa wahusika.

𝐀𝐭𝐡𝐚𝐫𝐢 𝐳𝐚 𝐮𝐭𝐚𝐧𝐝𝐚𝐰𝐚𝐳𝐢 𝐡𝐢𝐳𝐨
 
Sasa video ikitumwa mtandao wa kijamii si ndio watu wengine wanajifunza?
Tunataka nini? Falsafa ya "what you see in Las Vegas stays in Las Vegas?"
Au tazama sakata la Muuguzi kuosha vifaa vya hospital in the wrong way. Nadhani watu wote wamepoteana huko katika medical proffession. Wanashindwa kutazamana usoni. Nasikia video ilipokuwa recorded watu walisikika wanasema,"Tazama wanavyotua"

Siku moja nilikuwa natembea mjini,nikapita maeneo ya Kariakoo,nadhani pale pale DDC, I went to the public toilet to piss.

Sasa pale at the urinary for men,alikuwepo huyu mtu ( this most probably uneducated person),and he was standing there pissing at this urinary.

Sasa,dhakari yake ,for some reason,some affliction,ilikuwa inawasha,inamuwasha,kwa hiyo alikuwa anaisugua pale pale kwenye kuta za ile urinary kama kujikuna muasho. It was unthinkable. Ile ehemu chafu,eti anatumia kujikuna.

Nikawa nafikiria tumesikia hadithi za wafalme wa zamani,kama vile Haroun Al Rashid,ambao walikuwa wanatembea in disguise in their kingdom kutazama what is going on. Nikawa nafikiria kuna tatizo hapa:wale watu ambao wana responsibility ya kumueleza huyu mtu kwamba anachofanya ni unhealthy,hajamwambia hivyo.

Baada ya mbili,baada ya siku chache Sarungi akaachishwa kazi. Sarungi ndie alikuwa waziri wa afya.
Sio kama vile mimi nilikwenda kushtaki kwa rais Ali Hassan Mwinyi. Lakini that is what happened.
Hapa umechanganya vitu viwili. Kuna mambo sote tunayafanya na ni halali kama mapenzi japo ni muhimu kujuwa unayafanyia wapi au hali ya kuonesha upendo sote tunafanya shida tu sehemu gani lakini yako mambo hayakubaliki na hayafanwi na watu wote ni kama mfano uliotoa kukojoa hovyo barabarani na mengine.
 
Hanna cha wivu wala nini sema watu mnaendekeza ujinga kila sehemu...hamjui sheria na taratibu za hospitalini? Mnajitoa ufahamu kwa kutetea ujinga. Pumbavu sana hii if ya kizazi hiki
Swala sio sheria na taratibu, toa ujinga wako hapa. Kama sheria na taratibu zinafuatwa nchi hii kusingekuwa na mzozo wa DP World.

Waliotajwa na CAG wote wangekuwa selo. Kwanini sheria ifuatwe kwenye mambo ya kijinga tu yahusuyo raia ila watawala ya kwao yanafumbiwa macho?
 
Aondolewe haraka ni mshenzi. Mtu anapata wapi nguvu ya kufanya umbeya na uzandiki kama anaumwa kweli? 😂 😂 😂
Kibaya zaidi anafanyia uzandiki mgonjwa mwenzake haya ndo machawi sehemu za kazi Sasa mkiwa mmeajiliwa sehemu na mzandiki kama huyu kazi itakuwa shughuli
 
Hahahah yani uchawi full. Bongo kwa uchawi na wivu tuna 100%!!!

Mtu ukionekana una enjoy maisha tu lazma uletewe zengwe yote hio ni wivu tu. Utarogwa tu bila sababu ili tu usiendelee kuinjoy 🤣

Ndio yale yale unagonga mpenzi wako kwenye gari yako anatokea mtu anawagongea vioo.
 
Menejimenti ya Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) imetoa ufafanuzi kuhusu uvunjifu wa maadili uliofanywa na Mgonjwa (jina limehifadhiwa) na anayedaiwa kuwa Mpenzi wake (jina limehifadhiwa) ndani ya wodi (3A) siku ya Jumapili mchana tarehe 9/07/2023 ambapo katika uchunguzi wa awali mgonjwa amekiri kufanya tendo la busu la midomo na ndimi na Mpenzi wake katika mazingira ya kuumwa ndani ya Hospitali kitu ambacho ni kinyume cha maadili ya kitanzania.

“Menejimenti imebaini kwamba Mpenzi wa Mgonjwa huyo si Mtumishi wa Taasisi ya MOl, aidha tukio hilo liligunduliwa na Muuguzi aliyekuwepo wodini ambapo alichukua hatua ya kuzuia Wahusika kuendelea na kitendo hicho, Menejimenti inaendelea kuchukua hatua zaidi kwa Wahusika”

“Uchunguzi zaidi umebaini pia wakati vitendo vinaendelea kuna Mgonjwa jirani (jina linahifadhiwa) ambaye alisharekodi video, Menejimenti ya MOl inalaani kitendo hicho cha uvunjifu wa maadili kilichofanywa na Mgonjwa huyo pamoja na Mpenzi wake, vilevile Menejimenti inalaani na kukemea kitendo cha kurekodi video wodini na kutuma kwenye mitandao ya kijamii kilichofanywa na Mgonjwa jirani”

“Matukio haya yote ni kinyume na mwongozo wa Wizara ya Afya unaozuia kufanya matendo ya uvunjifu wa maadili kwa mgonjwa na kurekodi video wodini, Menejimenti inaendelea kuchunguza zaidi tukio hili ili kujiridhisha kuwa hapakuwa na uzembe katika kusimamia usalama wa Wagonjwa wakati Ndugu wanawatembelea Wagonjwa wodini”

Baada ya Tamko hili Mgonjwa aomba radhi
MGONJWA aliyelazwa katika Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) ambaye video yake imesambaa kwenye mitandao ya kijamii ikionesha akibusu midomo na ndimi na mpenzi wake wodini ameomba radhi kwa kitendo hicho na kuahidi hatorudia tena.

Taarifa iliyotolewa na Afisa Habari wa Moi, Patrick Mvungi inasema kuwa kitendo hicho kimefanyika katika Wodi 3A siku ya Jumapili mchana Julai 9, 2023.

Aidha, amesema katika uchunguzi wa awali mgonjwa amekiri kufanya tendo la busu la midomo na ndimi na mpenzi wake katika mazingira ya kuumwa ndani ya Hospitali kitu ambacho ni kinyume na maadili ya Tanzania.

“Menejimenti imebaini kwamba mpenzi wa mgonjwa huyo si mtumishi wa Moi.”Amesema

Amesema, tukio hilo liligunduliwa na muunguzi aliyekuwepo wodini ambapo alichukua hatua ya kuzuia wahusika kuendelea na kitendo hicho na menejimenti inaendelea kuchukua hatua zaidi kwa wahusika.

Tatizo lipo kwa aliye record video, jinga kabisa. Hayo ni maisha ya watu. Umbea tu usio maana.
 
Back
Top Bottom