Moja wapo ya Fungu kwenye Biblia linalotafsiriwa vibaya: Matendo ya Mitume 10:15

Soma vizuri hayo yalikuwa ni maono tu na nimeweka na tafsiri yake ambayo ipo katika sura hiyohiyo. Nyie mnasomaje Biblia mbona mambo mengine yapo wazi tu-?
 
Ni kwanini Petro alimkatalia Mungu mara tatu kuchinja na kula wanyama wale aliokuwa ameletewa? na hakula mpaka chombo kikaondolewa,

Hayo mafundisho yeye aliyapata wapi?
 
Petro alimkatalia Mungu mara tatu kwamba hawezi kula Najisi, na huyu alikuwa mfuasi wa Yesu, Je mafundisho hayo aliyatoa wapi? Na kwanini alikataa ikiwa Mungu ameruhusu tule kila kilicho mbele yetu?
petro ni kutoka katika taifa hilo hilo lililozishika sheria za tolati,enzi na enzi.

hata aliotembea nao Yesu na kulala nao haina maana walimuelewa 100% bado wengi iliwachukua muda,kama mtume paulo.
 
Na hapa je??

Wakolosai 2:16-17
[16]Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato;

[17]mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo.
Naaaaam Naaaaam
 
Barikiwaa sanaaa.
 
Lete Andiko linalosema agano la Kale lilifutwa...
Soma waebrani 6,7 na 8. Hayo yote ni kivuli tu kumuelezea kristo. Ndio maana hatuna kuhani mkuu, sadaka za kuteketeza, au hema ambalo ndiko pekee Mungu alipatikana. Cha ajabu reality iliyokuja ndio Yesu ila watu bado mnajifichia kwenye kivuli.
 
Soma waebrani 6,7 na 8. Hayo yote ni kivuli tu kumuelezea kristo. Ndio maana hatuna kuhani mkuu, sadaka za kuteketeza, au hema ambalo ndiko pekee Mungu alipatikana. Cha ajabu reality iliyokuja ndio Yesu ila watu bado mnajifichia kwenye kivuli.
God bless you
[emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]
 
Chakula ni utamaduni,
Yesu alisema ya kuwa "..amri iliyokuu kuliko zote ni upendo..."

"..Mpende jirani yako kama nafsi yako.."

Mambo ya kitimoto yalikuwa katika torati ya Musa, kwa maana watu waliishi katika sheria.

Kwa sasa tunaishi katika Amri za Mungu ( hakuna amri inayoongelea chakula)

Mnajipa mzigo mzito kiimani ilihali hamuwezi kutenda hata yaliyo ya kawaida katika maisha? Chakula huingia kinywani kisha tumboni na huenda chooni.

Imani yako ndiyo msingi wa hukumu.
Mnajihesabia haki kwa kuwa tu hamli kitimoto!?
 
Fine tunatenda dhambi na hata Biblia imeandika tukisema hatuna dhambi tunajidanganya na tunamfanya Yesu Kristo kuwa Muongo kasome Yohana 1:8–10,

Je kutenda kwetu dhambi (maana hata kuwaza ni dhambi) Kutufunge midomo tusiwaseme watu wengine wanaopotoka?
 
Wakolosai 2:16-17
[16]Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato;
Kuhukumu ni kazi ya Mungu kazi yetu sisi ni kusema ukweli pale tunapoona mtu anapotoka, Ni fungu hilohilo watu huwa wanalitumia kuisema sabato ila wanasahau kwamba watu ambao paulo alikuwa anawambia hapo walikuwa wanaishika sabato pamoja na paulo mwenyewe. Soma matendo ya Mitume 17:2 Inasema "Paulo alijiunga nao kama ilivyokuwa desturi yake, akajadiliana nao Sabato tatu mfululizo, akitumia Maandiko Matakatifu."
 
Mbinguni hatuingii Kwa kipimo Cha kula chakula, tutaingia Kwa kufanya matendo mema na ROHO nyeupe ambayo sio ya visasi wala husda
 
Yaani ujumbe tu wa Kumwambia Petrol aongozane na wale wasio wayahudi ilimkazimu kutumia Wanyama?

Maono unayachukulia poa eti ilikuwa maono tu......mbona hakutumia Ng'ombe ambaO hazibishaniwi?
 
Bold kubwa,tusitumie maandiko matakatifu ku-justify udhaifu wetu na mimi nikikwambia kasome Luka 6:41-45 andiko mahsusi kwa wanaojifanya wasafi kiimani unadhani tutafika?

Kila mmoja amepewa utashi wa kung’amua mema na mabaya na kila mtu Mungu anampa muda wa kujirudi usitumie nguvu nyingi kwa ajili ya wengine huku wewe hatma yako huijui.
 
Hili una uhakika nalo? Unajua ibada ya jumapili imekuja siku gani?
Mimi siyo mtaalam sana kwenye mambo ya dini. Naomba msaada ni kitabu gani na aya ipi kwenye Biblia iliyoelekeza kuwa ibada ni lazima ifanyike JUMAMOSI? Msaada please.
 
Kimwingiacho mtu hakimtii unajisi kwani hicho hutoka na kuingia chooni, bali unajisi ni Yale yatokayo moyoni mwake... Wivu, chuki nk........

Sent from my Infinix X6517 using JamiiForums mobile app
 
Wewe kama huli, sisi wenzako tunakula. Wasabato kuna wakati mnatuonea sana wivu sisi wala Kitimoto.

Mbona Wachina wanakula mbwa, nyoka, chatu, paka, vyura, nk. Lakini hamuwasemi? Hii siyo poa kabisa.
 
Kinachowaponza watu aina ya mtoa mada ni unafiki. Wao wanafikiri dhambi ni kunywa pombe na kula tu kitimoto. Ila mambo mengine wanaona ni ruksa kufanya! Jambo ambalo siyo sahihi hata kidogo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…