Moja wapo ya Fungu kwenye Biblia linalotafsiriwa vibaya: Matendo ya Mitume 10:15

Wewe kama huli, sisi wenzako tunakula. Wasabato kuna wakati mnatuonea sana wivu sisi wala Kitimoto.

Mbona Wachina wanakula mbwa, nyoka, chatu, paka, vyura, nk. Lakini hamuwasemi? Hii siyo poa kabisa.
Mimi nmetaja wanyama najisi hayo mambo ya kitimoto wewe ndio umeyaleta.
 
Kinachowaponza watu aina ya mtoa mada ni unafiki. Wao wanafikiri dhambi ni kunywa pombe na kula tu kitimoto. Ila mambo mengine wanaona ni ruksa kufanya! Jambo ambalo siyo sahihi hata kidogo.
Unafiki upi sasa, uzi unahusu wanyama najisi, ulitaka nianzie kuongelea dhambi zote ndio nije nimalizie hilo?

Dhambi ni dhambi, kama kuna mahali popote umeona nazungumza kwamba dhambi zingine ni sawa tu then paoneshe.
 
S
Na hapa je??

Wakolosai 2:16-17
[16]Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato;

[17]mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo.
AfI kabisa ajibu na hili andiko
 
Mimi siyo mtaalam sana kwenye mambo ya dini. Naomba msaada ni kitabu gani na aya ipi kwenye Biblia iliyoelekeza kuwa ibada ni lazima ifanyike JUMAMOSI? Msaada please.
Kutoka 20:8-11 Hiyo ndio siku tuliyoamriwa kupumzika na kufanya ibada, Na huo siyo utaratibu wa Duniani tu hata kwenye mbingu mpya Mungu atakayoifanya bado watu watakwenda mbele zake kuabudi siku ya saba ya Juma, Unaweza kusoma Isaya 66: 23
 
Kila mmoja amepewa utashi wa kung’amua mema na mabaya na kila mtu Mungu anampa muda wa kujirudi usitumie nguvu nyingi kwa ajili ya wengine huku wewe hatma yako huijui.
Kuanguka kupo lakini walau iwe bahati mbaya,

Kuna mambo kwenye bible yamenyooka ila watu mnapenda kuzunguka.

Tukikemea watu wanaopotoka mnaanza kutuona wanafiki, sijui tunawahukumu, hakuna anayekuhukumu maana hiyo ni kazi ya watakatifu,
 
Bold kubwa,tusitumie maandiko matakatifu ku-justify udhaifu wetu na mimi nikikwambia kasome Luka 6:41-45 andiko mahsusi kwa wanaojifanya wasafi kiimani unadhani tutafika?
Kwani wapi mimi nimejitanabaisha kwamba ni msafi kiimani, mbona malalamiko? Mtu akikemea mambo ambayo hayapo sawa ndio anakuwa msafiki kiimani?
 
Kutoka 20:8-11 Hiyo ndio siku tuliyoamriwa kupumzika na kufanya ibada, Na huo siyo utaratibu wa Duniani tu hata kwenye mbingu mpya Mungu atakayoifanya bado watu watakwenda mbele zake kuabudi siku ya saba ya Juma, Unaweza kusoma Isaya 66: 23
🤣🤣🤣🤣Wasabato mna shida sana. Nachowashangaa mnabagua Sheria za torati. Kuna mnazongangana nazo na Kuna zingine mnakataa. Hayo mambo ni mzigo ndugu zangu. Sheria ya kristo ni upendo kwa Mungu na jirani. Hayo mambo mengine yalikua ni tamaduni za kipindi hicho ambazo Mungu alikusudia kuwatenga watu wake na wapagani. Nowadays Mungu habagui Wala hawatengi watu wa jamii yoyote. Achaneni kushupaza vichwa na akili zenu na kujibebesha mizigo isiyo na ulazima.
 
Hujasoma marko 7:19 Yesu alihalalisha vyakula vyote,,,,agano la kale linamapungufu ndio mana likaja agno jipya soma Biblia uelewe
 
Yaani ujumbe tu wa Kumwambia Petrol aongozane na wale wasio wayahudi ilimkazimu kutumia Wanyama?
Kwamba hutaki kuamini kwamba yale yalikuwa maono?

Haya Chukua Biblia yako soma Matendo ya Mitume 10:17 kama unabisha hayo hayakuwa maono,

Na tafsiri ya Maono hayo ni Matendo ya Mitume 10:28.


Maono unayachukulia poa eti ilikuwa maono tu......mbona hakutumia Ng'ombe ambaO hazibishaniwi?
Yaani kusema kwamba yalikuwa maono ndio nayachukulia poa?

Na mimi nikuulize kwanini aliletewa wanyama wote najisi? Kwanini mara tatu zote alikataa kwenda kuchinja ale na alimkatalia Mungu? Mbona Mungu hakumuadhibu?
 
Hujasoma marko 7:19 Yesu alihalalisha vyakula vyote,,,,agano la kale linamapungufu ndio mana likaja agno jipya soma Biblia uelewe
Ni stori hiyohiyo iko Mathayo 15 na ukisoma lile fungu la 17 linaelezea hichohicho kitu ila ule mstari unaosema alihalalisha vyakula vyote haupo.

Hilo fungu unalolieleza hapa soma version zaidi ya moja ya biblia utapata majibu, kuna article nyingi sana zinaelezea nini kilifanyika mpaka hilo fungu likawepo
 
Sijawahi kuwa na imani na kitabu cha matendo ya Mitume.

Baada ya Gospel 4 sina imani na vitabu na barua za Paulo.

Sina mashaka na vitabu vya Wahebrania
 
Mbinguni hatuingii Kwa kipimo Cha kula chakula, tutaingia Kwa kufanya matendo mema na ROHO nyeupe ambayo sio ya visasi wala husda
Ufunuo 14:12 imewataja watakatifu kama watu wazishikao amri za Mungu na Imani ya Yesu,

Kutenda matendo mema peke yake huku umeacha yale Mungu aliyoagiza hakukupeleki popote.
 
Mnyama akiitwa ' najisi' maana yake ni nini ?.... Kwenye hiyo mistari ya mambo ya walawi nguruwe ametajwa kama 'najisi' na tena mtu akila atakuwa 'najisi' mpaka jioni.

Mambo ya Walawi 11 7
Na nguruwe, kwa sababu yeye anazo kwato, ni mwenye miguu iliyopasuka kati, lakini hacheui, yeye ni najisi kwenu.

Mambo ya Walawi 11 24
Nanyi mtakuwa najisi kwa wanyama hao; kila atakayegusa mzoga wao atakuwa ni najisi hata jioni;

Mambo ya Walawi 11 25
na mtu awaye yote atakayechukua cho chote cha mizoga yao atafua nguo zake, naye atakuwa najisi hata jioni.


Kwa maelezo hapo juu ni kwamba ukila nguruwe mchana utakuwa najisi siku nzima mpaka jioni tu au nimekosea ?

Tofautisha maneno najisi na haramu

"Najisi" na "haramu" ni misamiati inayotumika katika muktadha tofauti, hasa katika lugha za kidini kama vile Kiislamu.

1. Najisi:
- Ni muktadha wa kitu kuwa na uchafu au unajisi, mara nyingi kutokana na mambo kama vile uchafu wa kimwili au kitu kuhusishwa na kitu kinachokataliwa kulingana na imani au desturi.
- Mara nyingine, katika lugha za kidini, "najisi" inaweza kutumika kumaanisha kitu kinachotakiwa kuepukwa au kutakaswa.

2. Haramu:
- Ni kitu au tendo ambacho kimeharamishwa au kisichoruhusiwa kufanywa, kwa kawaida kulingana na mafundisho ya dini au sheria.
- Mara nyingine, "haramu" inaweza kutumika kumaanisha jambo lisiloruhusiwa kufanywa na inaweza kuhusisha mambo ya kisheria au ya kidini.

Kwa kifupi, "najisi" ni zaidi kuhusu uchafu au kitu kinachokataliwa kutokana na sababu fulani, wakati "haramu" ni kuhusu kitu au tendo ambalo limepigwa marufuku kufanywa kwa mujibu wa mafundisho au sheria.



zitto junior Mathanzua FaizaFoxy
 
Watu wanachukua vifungu kidogo ambavyo vinafavor vitu vyao ambavyo kwa macho yao vinawavutia ila hawasemu ukweli.
Naona hata wewe mwenyewe umechukua kifungu kidogo ukaanzishia mjadala mfupi japo sijaelewa hitimisho li wapi
 
Nikiona mkristo anakimbilia agano la kale kuclarify imani yake namuona hajaelewa imani yake bado.
Kabisa mkuu, agano la kale ni kivuli cha agano jipya tena mtume Paulo aliwaambia waebrania

Waebrania 8:13
Kwa kule kusema, Agano jipya, amelifanya lile la kwanza kuwa kuukuu. Lakini kitu kianzacho kuwa kikuukuu na kuchakaa ki karibu na kutoweka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…