Moja ya makosa utafanya ni kuolewa na Mwanaume wa miaka 50+. Walioingia huko wengi wanalia

Moja ya makosa utafanya ni kuolewa na Mwanaume wa miaka 50+. Walioingia huko wengi wanalia

Sometimes umasikini huwa unatabia Moja kuu .

Unakunyima best option.

Ni kweli haijakaa sawa Binti mwenye 20s na mzee wa miaka 50.

Ila Sasa unakuta anabidi atumie hiyo ndoa kama survival strategies

Ni sawa na MTU unakuwa umepata A zote badala ya kusomea udaktari unasomea ualimu ili upate ajira .

Au una A zote unaingia Polisi n.k

So ushauri wako ni mzuri ila unawafaa watu wanaotoka stable family ambao wapo na machaguo mengi na preference.

Uko sahihi kabisa
 
Happy life huwezi kuijua kwa mwanamke kama hana uhuru na wewe.

Mwanamke akiwa na uhuru ndio utajua yuko happy au anahuzuni.

Mpaka naandika hapa ni kwamba wanawake wengi hasa walioolewa na wanaume wakubwa wengi wao hawapo happy. Na wanazungumza kwa uhuru kwangu mambo ambayo sidhani waume zao wanajua haya.

Hakunaga furaha bila Uhuru.
Ukisema wanaume wakubwa haimake sense
wewe ungeweka tu age difference
Mwanamke wa miaka 45 unataka aolewe na mwanamme wa umri gani?
 

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

1. Chunguzi zangu za kina zinanionyesha haya. Nitazungumza ukweli mwingi ili kuwaponya ambao wanataka kujaribu kujiingiza huko.

2. Wadada wengi baada ya kuumizwa na mapenzi kutoka kwa vijana wenzao. Hufikiri kwamba suluhisho ni kuolewa na wababa watu wazima wale 50+ huko.

3. Ukweli ni kuwa Hakuna suluhu ya namna hiyo. Mtibeli nikuambie wazi hakuna watu wanaoteswa na mapenzi kama walioolewa na Wababa watu wazima.

4. Katika simu za wanawake kumi nitakazopokea zinazohusu mambo ya ndoa, simu sita ni wanawake walioolewa au wanaoishi kindoa na wanaume watu wazima. Na malalamiko yao yanafanana kwa asilimia 90%.

5. Nilipojaribu kuuliza kwa nini waliolewa na Wanaume watu wazima majibu yao yalikuwa hivi;
a) Watu wazima wanajua kupenda na wanajali.

b) Watu wazima walishavuka ujana hivyo hawana matukio.
c) Watu wazima wanajua thamani ya mwanamke na familia.
d) Watu wazima wanajua kutunza nakuhudumia kwani wengi wao wamejipata.

Hayo ni mawazo yao makuu karibu wote walizungumza mambo yanayoelekeana na hayo.

6. Na mitazamo hiyo ni Kabla ya wao kuishi au kuolewa na Wanaume hao watu wazima.

7. Baada ya kuolewa, mitazamo yao ilibadilika na walikuwa very dissapointed

8. Matokeo na malalamiko yao yako hivi;
a) Watu wazima wanapenda tuu mwanzoni lakini baada ya miezi kadhaa wanabadilika ni bora hata vijana.

b) Watu wazima ni wabinafsi na wanyanyasaji. Maneno kama ya kukusaidia, nilikutoa huna mbele wala nyuma, huna pakwenda ni kawaida.

c) Watu wazima wengi huwazuia Wake zao hawa wadogo kutokufanya kazi kwa kuonyesha wanawivu. Lakini Mtibeli najua hiyo ni njia ya kuwadhibiti na kuwatawala hao mabinti kirahisi.

d) Changamoto za Mke aliyetangulia na Watoto aliowakuta.
Bado mke na watoto aliowakuta ananguvu kubwa kwenye maisha ya Mwanaume mtu mzima.
Hii inafanya binti aliyeolewa na mtu mzima kuwa hana mamlaka wala nguvu yoyote.

e) Watu wazima bado hawajaacha tabia za kutembea na wanawake na wengi Bar na kazi ndio muhimu kuliko mke mpya.

f) Hakuna Kampani wala attension kutoka kwa Baba mtu mzima. Hii inawafanya wadada waishi kwa stresa. Zingatia mwanamke anathamini attention kuliko kula.

g) Mitazamo potofu kutoka kwa Mwanaume na jamii kuwa mwanamke kafuata pesa.
Wadada karibu wote waliniambia moja ya kero zinazowafanya wajute ni kasumba hiyo kwamba mpaka mwanaume anahisi kwamba alimfuata kwa sababu ya pesa.
Ndugu wa mume na majirani wanamtazamo huu jambo ambalo mwanamke hata kama anamapenzi ya kweli anaonekana kaja kuchuma mali.

9. Kwa kifupi, wadada wengi hujikuta katika hali ya stress na majuto baada ya matarajio yao kwenda kombo.

10. Kama Mtibeli, mara nyingi nashauri. Mabinti hakikisha, fanya ufanyavyo uwe na uwezo wa kujihudumia wewe mwenyewe. Kazi ndio Dini yako.
Maana msingi wa matatizo mengi wanayolalamikia wanawake upo kwenye utegemezi.

11. Mwanamke ukishakuwa unauwezo wa kujihudumia mapenzi hayawezi kukusumbua. Utasumbuliwa na mwanaume mmoja tuu. Yule uliyempenda kwa moyo wako wote. Wanaofuata ni kitonga.

12. Moja ya dalili huna kazi za kufanya ni kuteswa na kila anayekuja kuwa mpenzi wako. Ni kiashiria huna kazi za kufanya.

Nimemaliza.

TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
Utafiti uchwara huu ..tatizo siyo umri labda kugombea mali na familia iliyo kuwepo kabla
 
Wanaume tunatakiwa umakini sana, ukiwa 50+ tafuta mwanamke 40+ and you'll enjoy. Hiyo gape ya 20yrs, 50+ vs 20+ itakuuwa kwa stress.
Siyo kweli wanaume wa umri huo waowapo wengi wao uwapa uhuru sana wake zao ..hivyo hakuna stress yoyote ....wao awaangalii maswala ya kuchunga papuchi ya mke bali malengo ya familia
 
Utafiti uchwara huu ..tatizo siyo umri labda kugombea mali na familia iliyo kuwepo kabla

Anagombeaje mali wakati yeye ni sehemu ya familia? Yupo ndani ya familia. Ni mali za familia. Yeye ni mke halali. Anagombeaje kitu ambacho naye ni mali zake?
 
Wanaume tunatakiwa umakini sana, ukiwa 50+ tafuta mwanamke 40+ and you'll enjoy. Hiyo gape ya 20yrs, 50+ vs 20+ itakuuwa kwa stress.

😃😄😀
Hilo gao linaongeza wingi wa tofauti ambao ni tatizo kwenye mahusiano
 
Ukisema wanaume wakubwa haimake sense
wewe ungeweka tu age difference
Mwanamke wa miaka 45 unataka aolewe na mwanamme wa umri gani?

Mbona inaeleweka Mkuu.
Sasa mwanaume 50+ akioa mwanamke 40+ unafikiri hiyo ni habari?

Mada ipo wazi
 
Siyo kweli wanaume wa umri huo waowapo wengi wao uwapa uhuru sana wake zao ..hivyo hakuna stress yoyote ....wao awaangalii maswala ya kuchunga papuchi ya mke bali malengo ya familia
Gape kubwa ya umri inafanya wawili washindwe kuishi pamoja, namna ya kufikiri, mambo ya kufikiri, mnakuwa hamuendani...lazima stress zikuuwe.
 
Mwana ume mwenyewe miaka 50 mara nyingi atakuwa tayari na watoto alio wapata kwa wanawake wengine ...tatizo lipo hapo

Anawatoto wakubwa. Wanasehemu ya maamuzi ndani ya familia.

Mwanaume mtu mzima age 50+ hawezi mfanya mkewe mwenye miaka 20+ au 30+ ati amuombe ushauri. Atamshauri kitu gani?
Wanaume wengi wanakuwa wana mifumo tayari inayojiendesha mpaka mifumo ya ushauri.

Kibinti kikifika kinajiona kama hakina umuhimu wowote. Kumbuka wanawake nao wanatabia ya kujifanya ati wanashauri au wachangiaji ndani ya nyumba ili uwepo wao uonekane.
Sasa hilo linakuwa gumu kutokea anapoolewa na mtu mzima
 
Back
Top Bottom