Moja ya makosa utafanya ni kuolewa na Mwanaume wa miaka 50+. Walioingia huko wengi wanalia

Moja ya makosa utafanya ni kuolewa na Mwanaume wa miaka 50+. Walioingia huko wengi wanalia


Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

1. Chunguzi zangu za kina zinanionyesha haya. Nitazungumza ukweli mwingi ili kuwaponya ambao wanataka kujaribu kujiingiza huko.

2. Wadada wengi baada ya kuumizwa na mapenzi kutoka kwa vijana wenzao. Hufikiri kwamba suluhisho ni kuolewa na wababa watu wazima wale 50+ huko.

3. Ukweli ni kuwa Hakuna suluhu ya namna hiyo. Mtibeli nikuambie wazi hakuna watu wanaoteswa na mapenzi kama walioolewa na Wababa watu wazima.

4. Katika simu za wanawake kumi nitakazopokea zinazohusu mambo ya ndoa, simu sita ni wanawake walioolewa au wanaoishi kindoa na wanaume watu wazima. Na malalamiko yao yanafanana kwa asilimia 90%.

5. Nilipojaribu kuuliza kwa nini waliolewa na Wanaume watu wazima majibu yao yalikuwa hivi;
a) Watu wazima wanajua kupenda na wanajali.

b) Watu wazima walishavuka ujana hivyo hawana matukio.
c) Watu wazima wanajua thamani ya mwanamke na familia.
d) Watu wazima wanajua kutunza nakuhudumia kwani wengi wao wamejipata.

Hayo ni mawazo yao makuu karibu wote walizungumza mambo yanayoelekeana na hayo.

6. Na mitazamo hiyo ni Kabla ya wao kuishi au kuolewa na Wanaume hao watu wazima.

7. Baada ya kuolewa, mitazamo yao ilibadilika na walikuwa very dissapointed

8. Matokeo na malalamiko yao yako hivi;
a) Watu wazima wanapenda tuu mwanzoni lakini baada ya miezi kadhaa wanabadilika ni bora hata vijana.

b) Watu wazima ni wabinafsi na wanyanyasaji. Maneno kama ya kukusaidia, nilikutoa huna mbele wala nyuma, huna pakwenda ni kawaida.

c) Watu wazima wengi huwazuia Wake zao hawa wadogo kutokufanya kazi kwa kuonyesha wanawivu. Lakini Mtibeli najua hiyo ni njia ya kuwadhibiti na kuwatawala hao mabinti kirahisi.

d) Changamoto za Mke aliyetangulia na Watoto aliowakuta.
Bado mke na watoto aliowakuta ananguvu kubwa kwenye maisha ya Mwanaume mtu mzima.
Hii inafanya binti aliyeolewa na mtu mzima kuwa hana mamlaka wala nguvu yoyote.

e) Watu wazima bado hawajaacha tabia za kutembea na wanawake na wengi Bar na kazi ndio muhimu kuliko mke mpya.

f) Hakuna Kampani wala attension kutoka kwa Baba mtu mzima. Hii inawafanya wadada waishi kwa stresa. Zingatia mwanamke anathamini attention kuliko kula.

g) Mitazamo potofu kutoka kwa Mwanaume na jamii kuwa mwanamke kafuata pesa.
Wadada karibu wote waliniambia moja ya kero zinazowafanya wajute ni kasumba hiyo kwamba mpaka mwanaume anahisi kwamba alimfuata kwa sababu ya pesa.
Ndugu wa mume na majirani wanamtazamo huu jambo ambalo mwanamke hata kama anamapenzi ya kweli anaonekana kaja kuchuma mali.

9. Kwa kifupi, wadada wengi hujikuta katika hali ya stress na majuto baada ya matarajio yao kwenda kombo.

10. Kama Mtibeli, mara nyingi nashauri. Mabinti hakikisha, fanya ufanyavyo uwe na uwezo wa kujihudumia wewe mwenyewe. Kazi ndio Dini yako.
Maana msingi wa matatizo mengi wanayolalamikia wanawake upo kwenye utegemezi.

11. Mwanamke ukishakuwa unauwezo wa kujihudumia mapenzi hayawezi kukusumbua. Utasumbuliwa na mwanaume mmoja tuu. Yule uliyempenda kwa moyo wako wote. Wanaofuata ni kitonga.

12. Moja ya dalili huna kazi za kufanya ni kuteswa na kila anayekuja kuwa mpenzi wako. Ni kiashiria huna kazi za kufanya.

Nimemaliza.

TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
wanawake wa jamii forum wengi wao wana uchumi ulio very stable
wapo wachache sana ambao ndio hawa tunaiwata TANZANIA.
 
Wanawake wanaolewa na watu wenye miaka hata 60 na wana happy life... na wapo vijana wengi wameona kwenye 30th lakini Kila kukicha ngumi mkononoi na kulalaia bar na mwishowe talaka.....
Mambo mengine ni maisha binafsi ya watu

Happy life huwezi kuijua kwa mwanamke kama hana uhuru na wewe.

Mwanamke akiwa na uhuru ndio utajua yuko happy au anahuzuni.

Mpaka naandika hapa ni kwamba wanawake wengi hasa walioolewa na wanaume wakubwa wengi wao hawapo happy. Na wanazungumza kwa uhuru kwangu mambo ambayo sidhani waume zao wanajua haya.

Hakunaga furaha bila Uhuru.
 
Sisemi ila vipo vingi😅😅
Sana sana utulivu mie sitaki kufokewa 🏃‍♀️🏃‍♀️🏃‍♀️(jokes
Wee mamilo mi sinaga tabia ya kufoka,kama ni mikasi ndo balaa,au unaogopa vile nakula Bia ntaacha kwaajili yako☺️
 
Mwanamke ukiolewa na mtu mzima awe na mali na hakikisha unatumia akili sio mihemko

kama ana mke ama alikufa jitahidi upate kwako ...... hata km ni single room

Kingine wacha kukodolea mali ulizozikuta macho jitahid akuwezeshe upate mtaji

Acha kupokea hati za nyumba na mali bila kujua uhakika wa Mali hizo kisheria utaangukia pua

Ukiwa na wababa tumia akili tafuta connection umri wako sio wa showoff ni w majukumu
 
Hakuna jibu la moja kwa moja, mikikimikiki ya haya mambo yanaendelea kuwepo na walikuwepo, mpaka anaolewa na mtu mzima tayari wewe unachangamoto kwa hiyo isionekana mtu mzima ana tatizo

Changamoto nimeshaisema Mkuu.
Mwanamke mwenye kazi na anayejimudu kimaisha hawezi kuolewa na mzee dunia iende irudi
 
Sio wote acha kuwapaka mafuta na mgongo wa chupa mzee
mimi nipo nao wamama na wadada wa JF kwenye ma group kadhaa ya watsap.
wengi nilionao kule ni wanawake wa uchumi wa kati na wajuu.
hakuna mwanamke wa JF anaomba omba hela za kijinga
sijui hela ya vocha, sijui hela ya kucha na ujinga ujinga
mwingine kama huo.
 
Mwanamke ukiolewa na mtu mzima awe na mali na hakikisha unatumia akili sio mihemko

kama ana mke ama alikufa jitahidi upate kwako ...... hata km ni single room

Kingine wacha kukodolea mali ulizozikuta macho jitahid akuwezeshe upate mtaji

Acha kupokea hati za nyumba na mali bila kujua uhakika wa Mali hizo kisheria utaangukia pua

Ukiwa na wababa tumia akili tafuta connection umri wako sio wa showoff ni w majukumu

Changamoto nyingine Mwanaume ikitokea amekufa kwa tatizo jingije lolote, binti hupewa kashfa ya kumuua mumewe na chuki inakuwa kati ya watoto wakubwa na watoto wa mke mdogo
 
Basi isije kuonekana kwa sababu Mwanamke amelewa kutokana na changamoto za Kiuchumi sasa anapokuta Yule Mwanaume uchumi hauko kama alivyotarajia isionekana Mwanaume ana shida

Shida zipo Mkuu😃😀😀

Watu msiolingana na kufanana shida zenu pia hazitalingana wala kufanana.

Ni kama single mother tuu. Shida inakuja pale ambapo hamfanani
 
Back
Top Bottom