Moja ya mambo yanayochangia migogoro kwenye ndoa nyingi ni wanaume kuingia kwenye ndoa wakitarajia wake zao kuwasaidia majukumu yao

Sasa dada angu kwani izo mimba huwa mnabeba maisha yenu yote baada ya kuingia tu kwenye mahusiano. Ofcourse kuna situation ambazo ambazo mwanamke hawezi kujigawa mfano ana mimba au ananyonyesha mtoto mchanga ivyo ivyo kuna situation ambazo mwanaume hawezi kutimiza majukumu yake ipasavyo mfano anaugua nankushindwa kwenda kibaruani ili apate mahitaji ya familia kwaiyo ni suala la kuangalia namna ya kumsaidia mwenza wako hapo. Katika scenerio ya kukutana na uyo dada wa kijapani aliyoongelea jamaa ulikua ni mtoko tu wa kawaida uyo dada hakua na mimba, ulemavu wala tatizo lolote la kumfanya ashindwe kufanya kazi kwa utimilifu hili kupata hela ya mahitaji yake, hiki kitu ni tofauti na wadada wa kibongo ambao mkitoka out watataka mpaka bodaboda uwalipie. Reply yako kwangu umetumia lugha kali kidogo sitokujibu kwa namna ulivyonijibu kuepuka ban maana nipo chini ya uangalizi wa moderators
 
Oohh kwahiyo hata kama wanawake wote duniani wakiamua wafunge vizazi vyao wasizae kwa sababu ni maamuzi yao basi itakuwa sawa tu si ndio, hivi unafahamu kwamba kuna nchi huko ulaya wanawake wameanza kususa kuzaa hadi viongozi wanaingilia kati na kuwabembeleza wazae maana population itapungua, kuhusu mambo ya vita mbona wanawake wengi tu siku hizi wamejaa majeshini na kuhusu huo mfano wako wa kupika misibani kwani hujui kuwa kwenye misiba ya waislam wanaopika ni wanaume au unaishi kwa kukariri tu
 
Very true 👍
 
Wewe nilishakuambia hakuna cha gender instincts wala nini hizo gender roles zilipangwa na wazee wetu wa zamani, na waliziassign kwa jinsia husika kulingana na utashi na upeo wao lakini si kwamba ni nature, ni mentality tu ambayo watu walijengewa vichwani vizazi na vizazi

Kwamba huyu anapendeza akifanya hiki na huyu anapendeza akifanya kile ndio ikawa sehemu ya tamaduni, lakini si kwamba huyu akifanya kile anachofanya mwenzie basi ni vibaya, na ukizingatia mwisho wa siku dunia inabadilika na mitazamo ya watu pia inabadilika toka vizazi hadi vizazi

Kama ambavyo sasa hivi jukumu la kutafuta pesa na kulisha familia limeshaonekana kwamba hata mwanamke anaweza kulifanya, wakati zamani ilionekana hawezi kwanini huo mtazamo usibadilike na kwenye majukumu yanayoitwa ya mwanamke, kwamba sasa mtu yeyote yule anaweza kuyafanya bila kujali jinsia yake
 
NImeshindwa kukuelewesha ili tusipoteze muda tufanye umeshinda. ishi na partner wako kwa namna utavyoona inafaa
 
Umeshindaaaa
 
NImeshindwa kukuelewesha ili tusipoteze muda tufanye umeshinda. ishi na partner wako kwa namna utavyoona inafaa

Umeshindaaaa
Tatizo lako wewe kila mada tunayojadili unakimbilia kusema nimeshinda, humu tunaeleweshana tu hatushindani wala hatutafuti mshindi, sijui kwanini watu wengi mitandaoni huwa mnajadili mada katika mtazamo fulani hivi wa kushindana
 
Tatizo lako wewe kila mada tunayojadili unakimbilia kusema nimeshinda, humu tunaeleweshana tu hatushindani wala hatutafuti mshindi, sijui kwanini watu wengi mitandaoni huwa mnajadili mada katika mtazamo fulani hivi wa kushindana
Sasa mkuu hatufiki hitimisho unataka tujadiliane mpaka lini? Kuna mambo mengine ya kufanya nje ya jf.
 
Baki nyumbani unilee mimi na wanangu sasa.

Tatizo lenu feminist mnashindwaga kubalance mzani.
Acha nikusanue kijana.

Kama mke ana kazi yake, ni kweli Me unapaswa kutimiza kila jukumu lako kama hayo uliyoaijisha na Ke anapaswa kutimiza yake ya nyumbani maana Me huwezi piga miguu yote. Kwamba usake doo na bado home uwajibike wewe(hilo haliwezekani).

Migogoro inaanza pale Ke anashindwa kutimiza majukumu yake ya nyumbani kwa kisingizio cha kazi ambayo haina manufaa kwa familia.
 
Ni kweli
 
Tatizo lako ni wanaume kufua, kupiga deki na kuosha vypmbo? Hivyo hatufanyi, hatutafanya coz mke na msaidizi wapo. In case msaidizi hayupo then kuna nyakati za kusaidiana kazi ndogo hizo. Sijui kwa nini kwako inakuwa big deal wakati kwa wanawake wenzako ni sifa kupika kufanya nyumba iwe safi nk.
Kwa nini kwako ni issue sana?

Nishakuambia, swala la huduma lipo kwa baba, hapo hatupingani, ila mama akiamua kutoka kutafuta, basi anachokipata kionekane, short of that basi aamke asubuhi na kulea familia yake as ndio primary role yake.

Hata wewe ukiingia kwa ndoa, hakikisha jiko is your friend, mpikie mume chakula kitamu, ukishindwa hilo jukumu moja tu basi ndoa itakuwa ngumu. We love to eat food prepared by our wives.
 
Maisha yamebadilika, enzi za wazazi wetu sio sawa na zetu.
Muhimu km wanandoa kusaidiana majukumu pale mwenzi wako anapoanguka, ndiomaana ya kumpa msaidizi. Siwezi kuacha mtoto anarudishwa nyumbani kwa kukosa school fees na mimi ninazo hizo pesa eti nasubiri mume atafute sababu yeye ni mume.

Jukumu la kuhudumia familia ni la wote unless km mke hana chanzo chochote cha mapato.
 
Sasa kazi ya mwanamke ni nini si bora ninunue malaya
Fikra Kama hizi
Ndo zinachangia migogoro
Unaingia kwenye ndoa ukitarajia umhudumie mke wako Kama Malaya wakAti unahitaji tendo ndo unampa mahitaji yake

Hio ndoa lazima migogoro iwepo
 
Hoja yangu mkuu ni vijana wengi wanaingia kwenye ndoa na fikra za kusaidiwa majukumu yao ya kiume

KIJANA anakwambia anataka mwanamke mwenye kazi au ajira
Lengo ili amsaidie majukumu yake
Maanake huyo mwanke akipoteza ajira hiyo ndoa haipo

Naelewa na ni sahihi mwanamke akisema nataka mwenye kazi au ajira
Siyo me
Sikatai kuoa mke mwenye ajira Ila kisiwe kigezo Cha wanaume

Pia suala la mwanamke kukupa kipato chake ni hoja nyingine
Hapo ndipo panatakiwa AKILI IINGIE KAZINI
Ndo kuishi nao kwa akili Sasa utafaidi maana sio lazima
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…