Moja ya tukio la kijinga na la kitoto ni kufanya sherehe ya HARUSI, ujinga ujinga mtupu

Umesema vyema mkuu, hauwezi ukawa na akili timamu ukaenda ukumbini kisa kuna jamaa anaoa

Na wengi wanaopenda hizi mambo za harusi ni wanawake na wanaume wenye tabia za kike
Hapana sikubaliana na wewe,binafsi ndoa yangu haikufanyika ukumbini hilo nililikataa binafsi,kwakuwa sitaki tu zile fujo za ukumbini

Lakini si sahihi kudhihaki watu wanao fanya sherehe zao kwa matakwa yao,kwakuwa wewe hupendi mambo ya ukumbini basi usione wenzako ni wajinga
 
Mbona wachina wanafanyaga Harusi?
 
Dogo Adriz mutu wangu inakuwaje? Unajifanya kucomment kama mtu mzima.

Maarass
 
Kupanga ni kuchagua, binafsi napingana na msherehe hayo.
Wenye jambo lao hasa ni wanawake.
Mkuu wewe haupendi kuburuzwa na MC?
Bila kuwepo Mc kuna uwezekano mkubwa sherehe ingekuwa inanoga sana,kosa kubwa ni Mc kupewa mamlaka yote ya kuendesha sherehe...
Nilisha jiondoa kwenye michango ya harusi tangu 2014.
 
Watu wa dunia ya kwanza hawana michango ya harusi. Wasiokuwa na hela hawafanyi hizo sherehe; otherwise, hulazimika kukopa.

Sisi makapuku wa dunia ya tatu lazima tufanye hizo sherehe ili angalau tupate hata zawadi ya jiko na sufuria za kuanzia maisha!🙈😁
 
Kama nimemuelewa mtoa mada,yeye hazungumzii swala la kufanya sherehe huku huna hela na kuwategemea wengine wamchangie,ila nilivyoelewa yeye shughuli nzima ya kufanya sherehe ukumbini anaona ni Ujinga!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…