Moja ya tukio la kijinga na la kitoto ni kufanya sherehe ya HARUSI, ujinga ujinga mtupu

Moja ya tukio la kijinga na la kitoto ni kufanya sherehe ya HARUSI, ujinga ujinga mtupu

Kamati za nini mnajadiliana ujinga tu, basi wanunulieni zawadi wanandoa wakaanze maisha yao

Wanakamati wanahangaikia harusi kuwa na li KEKI kubwa afu la ngazi, huku nyama zikiwa chache hio ndoa haiwezi kudumu
Duuu
Kumbe wewe unataka nyama nyingi

Halafu wao badala ya kuweka nyama nyingi wanaleta keki kubwa lenye ngazi ngazi.....
 
Huyu jamaa kilichomkela ni zile kadi za michango zilizojazana mezani kwake.

Ila yuko sahihi kabisa
Kweli ila alichangiwa sasa yeye hataki kuchangia sio vizuri angekataa basi hivi ukiweka 30 kwa kila kadi na zawadi ya vikombe viwili vya chai kwa kila kadi shida iko wapi
 
Events za harusi zinaboa sana. Miaka nenda miaka rudi ukumbini mambo ni yaleyale: ​
  • Ingia ukumbini
  • Cheza kidogo
  • Kata keki
  • Tambulisha ndugu
  • Toa zawadi
  • Nenda kwenye msosi
  • Muziki
  • Tuwaage maharusi wetu wakapumzike (wakaichape)

Kweli miezi 3-4 watu wazima wanakaa vikao kwa ajili ya ujinga kama huo! Na pesa zinakusanywa

Katukio ka saa 4 hadi 5 lakini boring and boring 🚮🚮
​
Na upumbavu zaidi, sherehe inafanyika ukumbini huko mbali. Saa 6 ikiisha ndugu mnahangaika kurudi kwenu. Kwanini sherehe isiwe mchana ikaisha jioni. Ungese mtupu.
Matako yenu wote mnaofanya upuuzi huo.
 
Wewe hukuchangiwa
Frankly speaking, tangu nimeanza ajira 2014 mwishoni nilikua mchangaji sana wa harusi na nimechangia nyingi sana na nyingine nilikua wale wavaa sare sjui ndio mnaita maids. Harusi yangu kuchangia ilikua Oct 2024 ambapo mimi ndio nilikua mpambe wa bwana harusi. Gari ya maharusi niliendesha mimi, licha ya kuwa ndio mpambe. Aliyeoa ni mshikaji wangu wa karibu sana.

Ajabu ni kwamba nilipopata mchumba, nilimwambia naandaa mazingira nikuoe. Yeye akawa anapush haraka, tena nilivyomwambia nimehamia kampuni nyingine kikazi na wamenipeleka Dodoma akawa anahofu ndoa itayeyuka. Nikamwambia natuma washenga kwenu na baada ya mwezi mmoja kupita naoa. Nahitaji watu 10 tu toka kwenu wengine mtawakuta kwetu tukishatoka kufunga ndoa. Kwetu kuna bonge la uwanja-thanks to my dad alijiwekea sehemu ya wazi. Pale panatosha tents 3, pakapikwa, pakaliwa, pakapambwa. Ni familia na marafiki zangu 5 tu ndio waliohudhuria pamoja na wale ndugu 10 wa mke wangu. Bajeti yangu ilikua 1.5m tu, familia ikajazia.
Game over

Hii hapa short budget (apart from 1.5m)
Gauni la kukodi laki 2
Kiatu chake cha 35k Kariakoo
Nywele na mapambo 150k
Suti yangu 160k
Kiatu cha 40k
Nilikuwa nimetoka kunyoa like 2 days ago, sikuhitaji more dids on my hair.
Nilikodi gari 1 ya hao ndugu wa mke.
Gari ya maharusi alitoa mwanangu wa damu tangu tunasoma O level hata mafuta sikuweka.
Wanafamilia walijitafutia wenyewe usafiri wao. Kikao kilikua kimoja tu mimi na baba ajenda TUPANGE RATIBA YA KESHO.
 
Acha hiyo, kuna ile utasikia watu wanakutana kujadiliana, kujifunza step za harusini 😀

Alooo, Mm harusi yangu tutishia Kwa mwanasheria/Kanisani.

Ila hyo honeymoon lazima iwe ya kibabe.
 
Back
Top Bottom