Moja ya tukio la kijinga na la kitoto ni kufanya sherehe ya HARUSI, ujinga ujinga mtupu

Moja ya tukio la kijinga na la kitoto ni kufanya sherehe ya HARUSI, ujinga ujinga mtupu

Events za harusi zinaboa sana. Miaka nenda miaka rudi ukumbini mambo ni yaleyale: ​
  • Ingia ukumbini
  • Cheza kidogo
  • Kata keki
  • Tambulisha ndugu
  • Toa zawadi
  • Nenda kwenye msosi
  • Muziki
  • Tuwaage maharusi wetu wakapumzike (wakaichape)

Kweli miezi 3-4 watu wazima wanakaa vikao kwa ajili ya ujinga kama huo! Na pesa zinakusanywa

Katukio ka saa 4 hadi 5 lakini boring and boring 🚮🚮
​
Punguza makasiriko kwenye maisha ya watu. Itakusaidia sana kuongeza umri wa kuishi.
 
Events za harusi zinaboa sana. Miaka nenda miaka rudi ukumbini mambo ni yaleyale: ​
  • Ingia ukumbini
  • Cheza kidogo
  • Kata keki
  • Tambulisha ndugu
  • Toa zawadi
  • Nenda kwenye msosi
  • Muziki
  • Tuwaage maharusi wetu wakapumzike (wakaichape)

Kweli miezi 3-4 watu wazima wanakaa vikao kwa ajili ya ujinga kama huo! Na pesa zinakusanywa

Katukio ka saa 4 hadi 5 lakini boring and boring 🚮🚮
​
Nakubaliana na wewe laikini njoo na mapendekezo. Alternative ways za kusheherekea harusi/ndoa
 
Haina tofauti na kwenda kanisani Jumapili, ujinga ni ule ule..tusimame tukae, kwaya neno sadaka then mnaondoka zenu!
 
Sherehe za harusi ni Sector/Industry za watu. Kuna watu wamewekeza kwenye kumbi, wengine kwenye U-MC na vifaa vya mziki, wengine kwenye chakula etc. Hawa watu ukiwaambia wabadilike au waache hawawezi. Maana ndo kazi yao. Kila wiki wana uhakika wa ku ingiza kipato.

Kinacho ni boa sana kwenye hizi harusi kuwa na watu lukuki ambao hata huwajui. Wanaitwa wageni waalikwa.

Mimi nadhani harusi ni jambo la kifamilia. Inatakiwa uwahusishe ndugu wa karibu na marafiki wachache wa karibu.

Hakuna haja ya kufanya sendoff na harusi ambazo zina fanana from A to Z. Mnanufaisha watu baki huku mkijikamua na oengine kuingia kwenye madeni. I propose the following script.

Day 1. Before ndoa. Introduction dinner. Itahusisha ndugu wa karibu pande zote na marafiki wa karibu kwa ajili ya kufahamiana. Si zaidi ya watu 60. Ndugu wa mke 20, ndugu wa mke 20, marafiki wa kila upande 10. Maharusi wanapata nafasi ya kutambuana na upande wa pili na kupiga story za hapa na pale. Kula kunywa na kucheza mziki wa hapa na pale. Saa 12 jioni hadi saa 4-5 usiku. Tukichulia budget ya juu ya Tsh 40,000 kwa mshiriki ni kama 2.4m. Hapa haukodi ukumbi wa mapambo wala DJ wala MC. Mnaenda kula hotelini, mwenye hotel ana arrange kila kitu mwenyewe.

Day 2. Siku ya kufunga ndoa. Washiriki ni wale 60 wa day 1 plus 40 wa nyongeza (20 kila upande). Ndoa inafungwa asubuhi kati ya saa 3 na saa 4. Then tunaenda kwa kwa ajili ya chakula cha mchana, then show na activity mbalimbali zinaendelea huku watu wakiendelea kula na kunywa hadi saa 4 -5 usiku. Hizi shows na activity zinafanywa na walishiriki wenyewe. Haukodi watu. Kwa mfano
1. Wimbo maalumu wa kumpongeza bi/bw harusi kutoka kwa rafiki zake bi/bw harusi.
2. Shairi kutoka kwa mdogo wa bi/bw harusi
3. Commedy show... etc etc.

Kwenye familia zetu kuna watu wana vipaji mbalimbali na huu ndo wakati wa wao kuburudisha familia.

Hapa budget ni 10,000,000.

Haya matukio yote yatakuwa ndo sendoff na harusi humo humo. So with budget isiyo zidi 15,000,000 ambayo familia mbili zote zinaweza kujichanga bila kuhitaji michango ya watu baki mnakuwa mme mme enjoy sana.
 
Sherehe ni asili ya mwanadamu,kukataaa sherehe unaikataa asili yako.
Ndoa haihitaji sherehe iwe ndogo au kubwa kuthibitisha upendo na commitment havitegemei ukubwa wa sherehe. Wapo watu wengi wenye ndoa imara bila kufanya harusi
 
Kabisa.

Wanaonikera zaidi ni wale vijana wa huku vijijini wanaolazimisha kufunga ndoa huku hana chochote.

Baada ya siku mbili za ndoa kile chakula na michango kuisha wanalala njaa na mke wake huku akidaiwa na fundi aliemshonea suti ya harusi.
Hao ni wale hujikita sana kwenye siku ya harusi kuliko maandalizi ya maisha ya ndoa yenyewe kama vile mipango ya kifedha na maisha

Wanashindwa kutofautisha kati ya harusi na ndoa
 
Lakini si sahihi kudhihaki watu wanao fanya sherehe zao kwa matakwa yao,kwakuwa wewe hupendi mambo ya ukumbini basi usione wenzako ni wajinga
Mwisho wa yote, upendo wa kweli haihitaji gharama kubwa kuthibitishwa. Kama sio ujinha ni nini kuteketeza mamilioni ukumbini na huku baadhi ya vipengele vya harusi vinaweza kuonekana ni vya kitoto na vinavyoonyesha immaturity kama kulishana keki kwa mdomo mbele ya hadhara
 
Hizo ni perception zako kila mmoja Ana utashi wake wa kufanya mambo
Kipaumbele cha harusi ni mwonekano kuliko uhalisia wa maisha. Katika baadhi ya harusi, msisitizo mkubwa huwa kwenye mapambo, mavazi, picha na show, badala ya maandalizi ya maisha ya ndoa. Hii inaweza kufanana na mtazamo wa kitoto wa kuthamini muonekano
 
Tangu nijitambue nimehudhuria harusi za ndugu zangu wa damu wawili tu,
Michango natao ila kama nna budget hiyo, nje na hapo mikausho
Hata nikitoa mchango kwenye harusi siendi
Kiufupi sipendi sherehe naonaga kama ku-fake happiness
Sahihi harusi ni ujinga sana
 
Ujinga utauona wewe unayetaka vitu tofauti, kwa wanaotaka routine hii huu si ujinga.

This is exactly what they want.

Na kwenye maisha hatupangiani, wengine tunaona soka ni ujinga, wengine ndiyo furaha yao.
 
Mwisho wa yote, upendo wa kweli haihitaji gharama kubwa kuthibitishwa. Kama sio ujinha ni nini kuteketeza mamilioni ukumbini na huku baadhi ya vipengele vya harusi vinaweza kuonekana ni vya kitoto na vinavyoonyesha immaturity kama kulishana keki kwa mdomo mbele ya hadhara
Nakubaliana na wewe kwa watu ambao wanafanya mambo nje ya uwezo wao,kuna watu harusi au sherehe ikiisha unakuta wana madeni mpaka 30,000,000/= kama sio ujinga ni nini?
 
Back
Top Bottom