Kuna kipindi nilifanya kazi sehemu, nikiwa nyumbani kila nikifikiria kesho natakiwa kwenda kazini natamani kulia, ile kazi nilikuwa naichukia ilifika mahali natamani hata niumwe ili nisiende kazini ila sikuacha kwa sababu nilikuwa sina namna nyingine ya kupata kipato. Hadi nilipopata mbadala ndio nikaondoka.... Unaweza kuwa uko mahali kwa sababu tu huna option ambayo ni bora zaidi kuliko pale ulipo, naamini ndoa ni tamu lakini sio kila ndoa iko hivyo, zingine ni chungu
Ndoa chungu zipo lakini sio nyingi kama zinavyotangazwa.
Asilimia kubwa ya ndoa watu wanaishi kwa furaha na wanaenjoy maisha. Na wengi wanaotoka kwenye ndoa ambao waliziona chungu hujuta. Ingawaje wapo wachache ambao hufurahia uamuzi wao.
Kingine, unapoona mtu yupo sehemu kwa sababu hana pakwenda ujue yeye ndiye tatizo.
Mfano wa kazi,
Mtu anapofanya kazi ya mshahara anaouona mdogo au mazingira hatarishi lakini akajilazimisha kufanya kazi basi ujue hiyo kazi ni muhimu kwake kuliko akiacha.
Ikitokea amehama kwa kupata nyingine labda yenye mapato makubwa hivyohivyo tunasema ni muhimu kwake.
Kwenye furaha kunakitu kinaitwa kuridhika. Kukubaliana na hali. Na kuishi ndani ya baraka ulizonazo.
Furaha ni mindset kwa sehemu kubwa
Kuna wanawake na wanaume wanawenza wenye sifa zinazotamaniwa na wengi lakini hawaridhiki nao. Na hawana furaha.
Kutosheka na kuridhika. Ni tabia ambayo ukiikosa hata mtu apewe nini hawezi kufurahia maisha.
Kuna mtu analipwa laki moja anaishi vizuri kwa furaha. Kuna mtu analipwa milioni moja haishi kwa furaha kwa sababu ya kutoridhika.
Wakati fulani nilifikiri kuvaa vizuri, kula vizuri ndio kuwa na furaha lakini haikuwa hivyo. Furaha inaanzia kwenye mindset then inatoka nje.
Kwenye ndoa, watu wengi waliowahi kuwasiliana na mimi, asilimia 80% tatizo lao ni mindset.
Kugombana wanagombana mara chache sana lakini hiyohiyo mara chache wanazitumia kama fimbo
Yaani mtu ulimkosea mwezi uliopita. Mkikorofishana kidogo anakumbushia. Ni suala la mtazamo, kukosa kusameheana. Kutoridhika.
Kwamba mtu kaoa au kaolewe lakini bado anatamani zaidi au anaona hakufanya uamuzi sahihi.