John Haramba
JF-Expert Member
- Feb 4, 2022
- 365
- 1,374
Muigizaji mkongwe wa Bongo Muvi, Monalisa ameelezea jinsi ambavyo mgogoro wa Urusi na Ukraine unavyompa hofu kwa kuwa mwanaye yupo nchini Ukraine.
Rais wa Urusi, Vladimir Putin alitangaza kuanza oparesheni ya kijeshi katika baadhi ya maeneo ya Ukraine baada ya mvutano wa muda mrefu baina ya mataifa hayo mawili.
Monalisa ameandika: “Tumbo linanicheza kama mzazi. Ukraine! Hakuna ndege, nampataje mwanangu? Mungu wasimamie watoto wetu.”
Ameandika maandishi hayo katika ukurasa wake wa Instagram akiambatanisha na picha moja ikionyesha moto katika moja ya maeneo inayodhaniwa kuwa ni Ukraine.
Binti huyo, Sonia inaelezwa kuwa anasoma katika Chuo Kikuu cha Sumy State kilichopo katika Mji wa Sumy akisomea kozi ya Uhasibu na Ukaguzi (Accounting and Auditing) kwa kipindi cha miaka minne.
Sonia mwenyewe aliwahi kunukuliwa akisema: "Sababu ya kuchagua kwenda kusoma nchi hiyo ni kwanza wametutangulia kiteknolojia kwa hiyo tunapoenda huko kusoma tunaweza hamisha teknolojia kwa njia ya elimu kuja hapa Tanzania.
"Kitu kingine Ukraine na Urusi ni nchi ambazo zina fursa nyingi za utalii hivyo tunavyoenda huko kusoma ni nafasi yetu kuwaambia Tanzania kuna nafasi nyingi za Uwekezaji, kuna Mlima Kilimanjaro, Tanzanite na mengine mengi ambayo Tanzania tunajivunia," amesema Sonia.