Baada ya Urusi kuonyesha nia ya dhati kabisa ya kuishambulia Ukraine, mataifa mengi Duniani yalichukua hatua za kuwarudisha raia wake nyumbani.
Wale ambao hawakuwa na nauli Serikali zao ziliwatumia nauli.
Na baadhi ya nchi kama Israel na Germany walituma ndege kabisa kubeba raia wao.
Wakati hayo yakijiri, Tanzania ilikuwa kimya utadhani hakuna mtanzania yoyote Ukraine.
Baada ya Urusi kutangaza kuyatambua majimbo ya Donetsk,Donbass na Lugansk yaliyoasi kutoka Ukraine na kujitangaza Jamhuri,ndipo Serikali ya Tanzania ilipotoa ushauri tu,na siyo msaada kuwataka Watanzania waliopo Ukraine warudi nyumbani.
Yaani ni ushauri tu,na si kwamba Serikali haikujua kwamba ni lazima vita iwepo, hapana, Serikali ilijua yote kuwa vita ipo kwa sababu kila kitu kilikuwa wazi ktk uso wa Dunia.
Ila kwa sababu ya kutokuwa na Desturi ya kupenda watu wake ndo sababu haikuchukua hatua zozote kuokoa watu wake.
Mmoja Kati ya Watanzania wenye majonzi na hili janga la Ukraine ni msanii wa Bongo movie,Monalisa, anadai kwamba amepoteza mawasiliano na Bintiye anayesoma Ukraine na hajui hatima yake hadi sasa hivi.
Kulikuwa na ugumu gani Serikali kuchukua hatua mapema za kuokoa watu wake kwa gharama yoyote ile?
Huwa tukisema kwamba Serikali ya CCM imechoka na imechakaa kifikra na kiutendaji tunaonekana watu wabaya sana.
Tuendako tutaongea lugha moja,sasa hivi mipaka ya Ukraine imefungwa,na anga limefungwa, hairuhusiwi ndege yoyote ya kiraia kuruka kwenye anga la la Ukraine.
Rais wa Ukraine amewataka raia wote kwenda kwenye kambi za kijeshi kuchukua silaha za kujihami.
Hatima ya Watanzania waliopo Ukraine hadi sasa haijulikani itakuwaje.