Chukwu emeka
JF-Expert Member
- Jan 12, 2018
- 25,299
- 40,929
😱😱😱😱 daah Inasikitisha sanaAjali imetokea eneo la Mzambarauni (Nje kidogo ya Mji wa Morogoro). Inadaiwa kuwa waendesha Bodaboda waliojaribu kuchota mafuta wameteketea ktk moto huo
> Mpaka sasa chanzo cha Lori hilo kupinduka na hatimaye kushika bado haijafahamika
======
Morogoro. “Inasikitisha”. Ndivyo unavyoweza kusema baada ya lori la mafuta ya petroli kupinduka eneo la Msamvu mkoani Morogoro na kuwaka moto muda mfupi baada ya watu kuanza kuchota mafuta hayo.
Tukio hilo limetokea leo Jumamosi Agosti 10, 2019 ambapo Mwananchi limefika eneo hilo na kushuhudia miili iliyoungua ikiwa imelazwa pembeni ya barabara ya Dar es Salaam-Morogoro wengi wakiwa ni madereva bodaboda na mamalishe wanaofanya shughuli zao hapo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa amesema karibu watu 57 wamepoteza maisha katika ajali hiyo iliyotokea saa mbili asubuhi.
Ajali hiyo imetokea umbali wa mita 200 kutoka kituo kikuu cha mabasi Msamvu ukitokea Dar es Salaam.
Baadhi ya mashuhuda wamelieleza Mwananchi kuwa baada ya lori hilo kupinduka, watu walianza kuchota mafuta hayo.
Wamesema mmoja wa waliokuwa wakichota mafuta hayo alikuwa akivuta sigara, kwamba ndio chanzo cha mlipuko huo.
Chanzo: Mwananchi