Morogoro: Lori la Mafuta lapata ajali na kulipuka, watu 104 Wapoteza maisha na wengine kujeruhiwa...(Picha zinaogofya)

Morogoro: Lori la Mafuta lapata ajali na kulipuka, watu 104 Wapoteza maisha na wengine kujeruhiwa...(Picha zinaogofya)

Afu sijui kwanini kwenye matukio km hayo lazima Kuna mtu anatokea anachomoa betri tu
Kuna mmoja hapo anasikika akisema jamani motooo dah nahisi huyo atakuwa amekufa maana anaonekana alikuwa karibu sana.
 
Umehakikia wapi? Huna hakika, unadhani tu. Inawezekana kulikuwa na wapita njia, wale wanaoshangaa bila kujua madhara n.k hao watu ni wengi sana MUNGU awape wepesi ndugu na familia zao.
Hata kushangaa nako ni kubaya. Na hii tabia tunayo sana Tanzania. Watu kukimbilia eneo la ajali kama kuna karamu. Kwa mtu mwenye akili hata kama nyumba yako iko karibu na eneo la tukio kama hili inabidi ukimbie mabali haraka sana. Kusogea eneo la tukio kama hili eti kwenda kushangaa siyo kisingizio hata kidogo. Ila siungu mkono lughu aliyoitowa jamaa kuwa ni mshahara wa dhambi... Binadamu tunafanya dhambi nyingi sana na yeye anafanya dhambi. Tusichague dhambi moja inastahili adhabu ya moto na nyingine haistahili
 
Sio wote mkuu mbona unahukumu kwa ujumla kenge wewe tukio limetokea kwny shughuli za watu wengine wapita njia tu wamekufa wengine wamekuja kushuhudia ajali kwanini wote useme wezi
mimi nawazungumzia wezi,siwaongelei wasio na hatia,kwa majisi wamepata stahiki yao
 
Inasemekana kuna mmoja alienda kuchomoa betri ya gari ndo likapiga shoti
Hapo kuna mjinga mmoja aliwawashia maana inaonesha baada ya kudondoka watu walienda chota.
Wengi inaonesha ni wa pikipiki
 
Kuna moja ishawahi tokea mbagala usiku sana.wahuni wakaingia kuchota mafuta.sasa kuna mjinga mmoja sijui aliona Giza linamsumbua akaenda kuchukua kibatari na kueka pembeni aone vizuri..kilichofuata!!
Afu sijui kwanini kwenye matukio km hayo lazima Kuna mtu anatokea anachomoa betri tu
 
Na hii ya leo kuna boya alienda kuchomoa betri
Siyo Iringa, ni Mbeya milima ya Uporoto kuelekea Tukuyu ambapo mtanashati John alisababisha moto ulipuke baada ya kujaribu kuiba betri, wenye sufuria hata, wenye vijiko nao wamo, wenye madumu twende, kaburi lao la pamoja lipo kando ya barabara.
 
mimi nawazungumzia wezi,siwaongelei wasio na hatia,kwa majisi wamepata stahiki yao
Kwani wewe hutendi dhambi? Je unastahili kuungua? Japo siungi mkono kuiba au kusogea kwenye ajali kama hiii lakini jaribu kuchunga kauli yako.
 
Haya malori ya mafuta inabidi yaanze kutengeneneza mitungi kama ya gari za natural liquid gas iko very strong kwenye ajali ndogo sio rahisi kupasukaa
 
Hakuwepo mtu mwenye akili ya kuwatandika fimbo hatoke hapo.

Huu ujinga ni mbaya sana.
Hapo hata ingekuwaje huwezi kusogea hapo ilikuwa ni kuomba kudra tu wachote then waondoke salama maana hata ukisema upige bomu la machozi huwezi ukisema uende uwachape moto ukianza unaanza na wewe unayechapa. Ila yote kwa yote ni mipango ya Mungu maana hujui kifo kitatokea kwa njia gani. Hii ni dunia na kila kitu kinaweza kutokea ndiyo maana hata vita hutokea ambapo binadamu hupambana na binadamu mwenzake ili amuue. Kama binadamu kwa binadamu wanaweza kupambana kuuana basi humu duniani kila kitu kinawezekana juu ya kifo.
 
Ghafla tu nimekumbuka ile ajali kama hii iliyotokea miaka ya 94-98 ambayo nayo iliondoka na watu wengi kisa lori la mafuta kudondoka! [emoji24][emoji24][emoji24] Sijui ilikuwa Kagera ile!
 
Back
Top Bottom