Morogoro: Lori la Mafuta lapata ajali na kulipuka, watu 104 Wapoteza maisha na wengine kujeruhiwa...(Picha zinaogofya)

Morogoro: Lori la Mafuta lapata ajali na kulipuka, watu 104 Wapoteza maisha na wengine kujeruhiwa...(Picha zinaogofya)

Duuh hapa kuwa na askari wa kuwazuia?

Wamesahau ile ajali ya Iringa miaka kadhaa nyuma. Karibu kijiji kizima kiliteketea sababu ya kusombelea mafuta ya bure. Moto ukishika unafata mtiririko wa matone ya mafuta yalipoenda, hivo hadi nyumba ziliungua.

May their soul Rest In Peace.
Hata Mbeya Mkuu,Jeshi la polisi halijawahi kuelimisha bodaboda kuhusu hatari ya malori ya mafuta zaidi ya kuvaa helmet
 
Moro
 
Hata kama mimi ni askari siendi. Kwani askari haungui? Ila nasi binadamu wagumu kuelewa kila mara watu wanaungua halafu lilindondoka lingine wanaenda kuungua tena.

Woow, yaani umesema hivo hadi nimesikia sauti....

Zamani nilikuwa nawaogopa askari, siku hizi am in love with them sababu ya askari mmoja tuu.... Natumai akipita hapa atafahamu ni yeye nimemmaanisha...(He cared for me halafu haifutiki akilini)

Kasie Matata.
 
Hiki ni kipimo sahihi jinsi gani mtaani hali si shwari, wimbi kubwa linaashiria ni ukosefu wa ajira. Laiti wangekua na ajira hapo ungewakuta askari wa usalana tu
Tanker la petrol linaanguka, mtu unaenda kushangaa nini!!! Wazi watanzania wengi hawana ajira

Lakini ukweli lazima usemwe jamii hiyo hiyo ambayo inatatizo la ajira, sehemu kubwa ni wapumbavu na wajinga kiasi cha kwamba anaamini kuanguka kwa hilo tanker hakuna hali ya hatari
Kuiba/kuzoa ayo mafuta ndio kutamaliza shida/umaskini wake


Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa
 
Ahuweni ajali inifuate ila siyo mimi kufuata ajali.
Siwezi kuguswa kwa namna yoyote ile na hili tukio zaidi ya kutaka litumike kama kielelezo kwa wapuuzi wengine wenye akili za kufikia.
Omba msamaha.. Au sema watania!
 
KUNA WAJINGA WENGINE AMBAO HUWA WANAPAKIA ABIRIA NA MADUMU YA PETROL KWENYE MABASI HASA MABASI YA VIJIJINI. NI HATARI SANA
KULE DODOMA KITUO CHA MAFUTA CHA TOTAL PALE IRINGA ROAD KIMULIKWE. NI MADUMU KWA MADUMU HATA WENYE MAGARI HAWAPATI HUDUMA. KIBAYA ZAIDI YANAPAKIWA KWENYE MABASI. IPO SIKU...
 
Hawajifunzi kutokana na matukio ya nyuma?
Hawawezi kujifunza kwasababu TANZANIA tuna watu wengi wasio penda kusoma/kusikiliza radio/kuangalia tv,yawezekana ukimfufua mmoja kati ya waliofariki pale ukamuuliza UMESHAWAHI KUSIKIA LORI LIMELIPUKA NA KUUA WATU TANZANIA HII? atakujibu HAPANA nimeonaga kwenye movie tu.

Wengi wao hapo hawajui hata kama hayo makitu n hatari maana vijiweni story zao kuu ni MADEMU na AINA ZINGINE ila hata siku moja hutokaa uwakute kijiweni wakisimuliana maafa ya kivuko kilichozama kama mv bukoba,nk

SO tunachotakiwa kuhakikisha tunakifanya ili tuokoe vijana wetu walio salia ni elimu na kubadilsha akili zao,kuwaza zaidi ya wanachokiwaza na kuachana na habari nastori za kina messi,na christiano kuna mengi ya kupiga story maana tanzania hii vijiweni stori zao kama sio MPIRA basi MAPENZI kwisha.
 
Sio wote mkuu mbona unahukumu kwa ujumla kenge wewe tukio limetokea kwny shughuli za watu wengine wapita njia tu wamekufa wengine wamekuja kushuhudia ajali kwanini wote useme wezi
Siungi mkono kauli yake lakini hata kusogea kwenda kushangaa nako ni ujinga uliopitiliza. Je, moto unajua huyu amekuja kushangaa tu? Na bado watu wanafanya makosa zaidi... wamejazana kuangalia miili iliyoungua kama wanaangalia sinema nzuri. Wengine wanafikia hata kuwa na ujasiri wa kupiga picha na ku-share. Ujinga ulioje!
 
Ila bodaboda jamani, jana kule Mwanza kama km 2 hivi kutoka nyegezi standi wakasabaisha ajali basi la Abood leo kama masaa 24 hivi yamepita eti Moro nako haohao, hivi baadhi yao huwa wanawaza nini vichwani mwao jama!?
Naipongeza sana Ethiopia kwa kukataza boda boda!! Nadhani Serikali ina haja ya kufungia wendesha boda boda, wengi wao akili haziko njema sana!!
Kwa tanzania bado naamini ajira ya uhakika kwa hawa vijana wetu ni kilimo na ufundi (VETA). Hizi boda boda zinamaliza nguvu kazi ya taifa kila uchwao.
 
Hapo hata ingekuwaje huwezi kusogea hapo ilikuwa ni kuomba kudra tu wachote then waondoke salama maana hata ukisema upige bomu la machozi huwezi ukisema uende uwachape moto ukianza unaanza na wewe unayechapa. Ila yote kwa yote ni mipango ya Mungu maana hujui kifo kitatokea kwa njia gani. Hii ni dunia na kila kitu kinaweza kutokea ndiyo maana hata vita hutokea ambapo binadamu hupambana na binadamu mwenzake ili amuue. Kama binadamu kwa binadamu wanaweza kupambana kuuana basi humu duniani kila kitu kinawezekana juu ya kifo.
Hakuna mpango wa Mungu katika hiyo ajali labda mungu.

Siyo kila kifo ni mpango wa Mungu na siku zote usiamini ya kuwa kila mtu hufa kwa mipango ya Mungu.
 
Hayo ni matukio ya kawaida sana kwa nchi kama Nigeria,mwaka huu tu matukio ninayokumbuka ni mawili...
 
Back
Top Bottom