Morogoro: Profesa wa SUA afikishwa Mahakamani kwa shitaka la ugoni, mkewe adai fidia ya Milioni 100

Morogoro: Profesa wa SUA afikishwa Mahakamani kwa shitaka la ugoni, mkewe adai fidia ya Milioni 100

Analazimisha kupendwa, ukute yeye ndio chanzo cha mume wake kwenda kuoa mwanamke mwingine. Hakuna mwanaume anaeweza Acha mke mwema. Hadi mwanaume kuoa mke mwingine shida ni kasoro ya mke wa kwanza kashindwa kujua wajibu wake ni nini
Halazimishi kupendwa, anadai haki yake,ndio maana kwenye madai hakuna sehemu anaomba warudiane,anadai fidia ya ugoni sababu Prof kaoa wakati huo bado ana mkataba wa ndoa kwahio anamdhalisha mke halali
 
Serikali haina zuio na idadi ya wake, bali inakupa cheti cha UHALALI wa Ndoa kwa kila Mke uliyeoa.
Ha ha ha; eti inakupa cheti kwa kila mwanamke utakayeoa! Ukisikia mwanaume mateso ndio kama hivyo! Oa upendavyo; muhimu cheti! Dah!
 
Haya makesi watu washayapitiaaa

Ila tuendele kufatilia hii kesi tu

Ova
Hii kesi mama kashashindwa mapeeema, yaan bora angeenda kanisani angesaidiwa angalau km angeshindwa ndio angeenda mahakamani kwa ushauri wa baba paroko kwamba huku tumewashindwa nendeni mahakamani na barua wanapewa, sasa hukurupuki tu kukimbilia mahakamani unaikimbilia Marriage Act je! umefuata procedure ulienda kanisani kupata suluhu mkashindwana na kupewa kibari cha kwenda mahakamani au kalidharau kanisa?
 
Hakimu Mfawidhi Lukumai ameahirisha kesi hiyo baada ya upande wa utetezi kuweka pingamizi la kutaka kesi hiyo isikilizwe faragha na imepangwa kuanza kusikilizwa kwa pingamizi hilo Februari 21, 2023.
Wakili anatakaje kesi isikilizwe faragha anaficha nini wakati tutasoma kila kitu kwenye hukumu pindi itakapotoka?😁😁

"Kwanza ningejua kuna waandishi ningeweka zuio la waandishi kupata taarifa hizi, hivyo kaandikeni mlichopata kwa wakili huyo mwingine,
Kama hataki waandishi si angeyamaliza kwa amani tu nyumbani mara baada ya kupokea madai.

"Kimsingi mteja wangu anadai kulipwa fidia ya shilingi milioni 100 kutokana na madhara ambayo ameyapata," alisema.

Wakili huyo alisema kuwa Oktoba 29, 2022 inadaiwa washitakiwa hao walifunga ndoa huku kukiwa bado kuna ndoa nyingine ya mlalamikaji ambaye ni Matrida na Profesa Kasanga.
Sasa kufunga ndoa kunawezaje kukaitwa UGONI?? Maana ugoni ni ile hali ya mtu aliyeoa au kuolewa kufumaniwa na mwenza wake, akiwa anafanya ngono na mtu mwingine. Kufunga ndoa tayari imekuwa ni ugoni?? Anyways, labda ana ushahidi kuwa hawa watu wamebanjuana, na vipi wakijitetea kuwa walikuwa wanajichunga wakisubiri mpaka NDOA na hata baada ya ndoa hawajabanjua kwa sababu labda mmoja alikuwa mgonjwa nk?


Hivi kumbe ugoni unaweza kudai fidia na ukalipwa
Unaweza kabisa, na kuna mwamba ameweka kesi humu kuonesha mahakama ilivyoamua alipwe fidia, ila sasa lazima uthibitishe kuwa hao unaowadai fidia wamezagamuana. Kama kwenye kesi iliyowekwa, jamaa amempa mimba kabisa yule demu, anarukaje fidia!! Tofauti na mwamba Profesa hapa, haijawekwa wazi kama kuna mizagamuano zaidi ya kusema kuwa kuna ndoa ilifungwa.

Kesi ipo. Na kwamba wamefunga ndoa wakati mkataba wa ndoa ya kwanza ni mke mmoja. Hapo lazima Profesa atakaa na kulipa fidia.
Ugoni uthibitisho wake sio ndoa, bali tendo la ndoa. Kama ishu ilikuwa ni ndoa ya mke mmoja, mke alitakiwa kupinga ndoa ya pili, sio kudai fidia ya ugoni bila kuthibitisha ugoni wenyewe. (Najua ni mapema sana, maana kesi haijaanza kusikilizwa, labda atathibitisha huo ugoni)
 
Back
Top Bottom