Hakimu Mfawidhi Lukumai ameahirisha kesi hiyo baada ya upande wa utetezi kuweka pingamizi la kutaka kesi hiyo isikilizwe faragha na imepangwa kuanza kusikilizwa kwa pingamizi hilo Februari 21, 2023.
Wakili anatakaje kesi isikilizwe faragha anaficha nini wakati tutasoma kila kitu kwenye hukumu pindi itakapotoka?😁😁
"Kwanza ningejua kuna waandishi ningeweka zuio la waandishi kupata taarifa hizi, hivyo kaandikeni mlichopata kwa wakili huyo mwingine,
Kama hataki waandishi si angeyamaliza kwa amani tu nyumbani mara baada ya kupokea madai.
"Kimsingi mteja wangu anadai kulipwa fidia ya shilingi milioni 100 kutokana na madhara ambayo ameyapata," alisema.
Wakili huyo alisema kuwa Oktoba 29, 2022 inadaiwa washitakiwa hao walifunga ndoa huku kukiwa bado kuna ndoa nyingine ya mlalamikaji ambaye ni Matrida na Profesa Kasanga.
Sasa kufunga ndoa kunawezaje kukaitwa UGONI?? Maana ugoni ni ile hali ya mtu aliyeoa au kuolewa kufumaniwa na mwenza wake, akiwa anafanya ngono na mtu mwingine. Kufunga ndoa tayari imekuwa ni ugoni?? Anyways, labda ana ushahidi kuwa hawa watu wamebanjuana, na vipi wakijitetea kuwa walikuwa wanajichunga wakisubiri mpaka NDOA na hata baada ya ndoa hawajabanjua kwa sababu labda mmoja alikuwa mgonjwa nk?
Hivi kumbe ugoni unaweza kudai fidia na ukalipwa
Unaweza kabisa, na kuna mwamba ameweka kesi humu kuonesha mahakama ilivyoamua alipwe fidia, ila sasa lazima uthibitishe kuwa hao unaowadai fidia wamezagamuana. Kama kwenye kesi iliyowekwa, jamaa amempa mimba kabisa yule demu, anarukaje fidia!! Tofauti na mwamba Profesa hapa, haijawekwa wazi kama kuna mizagamuano zaidi ya kusema kuwa kuna ndoa ilifungwa.
Kesi ipo. Na kwamba wamefunga ndoa wakati mkataba wa ndoa ya kwanza ni mke mmoja. Hapo lazima Profesa atakaa na kulipa fidia.
Ugoni uthibitisho wake sio ndoa, bali tendo la ndoa. Kama ishu ilikuwa ni ndoa ya mke mmoja, mke alitakiwa kupinga ndoa ya pili, sio kudai fidia ya ugoni bila kuthibitisha ugoni wenyewe. (Najua ni mapema sana, maana kesi haijaanza kusikilizwa, labda atathibitisha huo ugoni)