Moshi: Mama afariki Dunia akiwa nyumbani kwa kukosa pesa ya matibabu, aacha watoto wadogo

Moshi: Mama afariki Dunia akiwa nyumbani kwa kukosa pesa ya matibabu, aacha watoto wadogo

Marehemu Happiness kasmiry kutoka kijiji cha Usari wilaya ya Moshi. Alishikwa na ugonjwa wa tumbo wa kuhara na kutapika kwa siku kadhaa kabla ya kufariki dunia akiwa nyumbani kwake kutokana na Kukosekana kwa fedha ya matibabu.

Mume wa marehemu huyo ajulikanae kwa jina la John alihakangaika kutafuta pesa ya kumpeleka Hospital kwa siku kadhaa bila mafanikio.

Mume wa marehemu amesema alikuwa anakabiliwa na ukata mkubwa kutokana na kumuhudumia mama yake mzazi ambae amepooza upande mmoja wa mwili.

Marehemu ameacha watoto watatu wadogo.
Mwenyekiti wa kijiji hicho amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kusema ni kweli familia ilikosa namna ya kumpeleka kupata matibabu kutokana na ukata hivyo mama huyo kufariki dunia akiwa nyumbani kwake
Ndugu sangu meku.

Kwenye msiba wa marehemu najua mtanunua vyakula na kununua pombe watu kula na kuywa na kulewa.

Gharama ya sanduku la marehemu laki 5.

Gharama za msiba na mzishi milioni 3.

Marehemu kafariki kwa kukosa 20,000 tu ya kufika hospitali.

RIP ddangu Manka
 
Binafsi sitakubali kufia home, naenda hospital hata kama sina hela naenda kulala kwenye mabenchi ya mapokezi wasinitibu nifie hapo
Una kufa kweli mkuu hakuna atakaye hangaika nawe hii ndio Africa.
 
Watu Wana roho mbaya, majirani wote wameshindwa kumpa msaada hata wa laki akaanze matibabu, mpaka mtu anakufa

Wala usilaumu watu, yamkini umezungukwa na wenye matatizo pia na huwasaidii aidha kwa kutowajua au vinginevyo..
 
Wachaga wabinafsi aisee yaani Kuna kitu hawana Ile social interaction Yao ni shida kusadiana kwenye shida
 
Marehemu Happiness Kasmiry kutoka kijiji cha Usari wilaya ya Moshi. Alishikwa na ugonjwa wa tumbo wa kuhara na kutapika kwa siku kadhaa kabla ya kufariki dunia akiwa nyumbani kwake kutokana na Kukosekana kwa fedha ya matibabu.

Mume wa marehemu huyo ajulikanae kwa jina la John alihakangaika kutafuta pesa ya kumpeleka Hospital kwa siku kadhaa bila mafanikio.

Mume wa marehemu amesema alikuwa anakabiliwa na ukata mkubwa kutokana na kumuhudumia mama yake mzazi ambae amepooza upande mmoja wa mwili.

Marehemu ameacha watoto watatu wadogo.

Mwenyekiti wa kijiji hicho amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kusema ni kweli familia ilikosa namna ya kumpeleka kupata matibabu kutokana na ukata hivyo mama huyo kufariki dunia akiwa nyumbani kwake
Adui wetu bado wako kazini, umasikini, ujinga na maradhi!
Kama angepelekwa hospitali wasingemtibu?
Vipi aliweza kupewa angalau maji mengi ya kunywa au nayo ni gharama? Kuhara na kutapika, kinapunguza maji mwilini, sasa sijui hawa ndugu walikuwa na uelewa wa kunywa maji?
 
Mwenyekiti wa kijiji hicho amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kusema ni kweli familia ilikosa namna ya kumpeleka kupata matibabu kutokana na ukata hivyo mama huyo kufariki dunia akiwa nyumbani kwake
R.I.P

Hata Mimi nilirudishwa hospital sababu bima yangu ya afya imefungiwa hivyo nikaambiwa niende makao makuu sababu za kufungiwa sikuirenew tangu nianze kunitumia wakaifunga sababu imexpire ukiangalia ugonjwa umenikamata na bima nnayo nngekufa pale hospital angelaumiwa nani?
 
Dunia ilivyo ya ajabu, kwenye msiba watu wamekula na kushiba
 
Ningepata nafasi, ningejibana nimsaidie marehemu. Inasikitisha Sana.
 
Kungekuwa na ile bima ya wote,huyu mama angepona aisee
 
Watu wote walozunguka pale walishindwa msaidie aende hospital ,?mwenyekit anashindwa changisha watu huku mgonjwa yupo hospital mbona wanachangisha pesa za mlinzi mara sijui nin ,🙆🏼‍♂️🙆🏼‍♂️
Sometimes akili/fahamu huwa zinakuwa zimefungwa. Hapo pia unakuta alikosekana mchangishaji /mhamasishaji, maana nayo ni talanta fulani.
 
Hii yote ni sababu watu tupo dunia ya tatu...

Kwa wenzetu hata kama huna pesa, unakimbia chap ER, unatibiwa ila deni lako utakutana nalo baadaye...

Wao kwao uhai kwanza
 
Halafu kuna watu wanaona Bima ya Afya kwa wote ni hasara kwa Taifa.
Bima ya Afya kwa wote SIYO BURE wewe MBUZI.

NI Tsh340,000 kwa MWAKA.

Kila mtu anayo??

Maana kibima Cha Tsh 30,000 kwa mwaka kwa kaya ya watu 6 chenyewe kimewashinda.
 
Watu wote walozunguka pale walishindwa msaidie aende hospital ,?mwenyekit anashindwa changisha watu huku mgonjwa yupo hospital mbona wanachangisha pesa za mlinzi mara sijui nin ,🙆🏼‍♂️🙆🏼‍♂️
Hata maendeleo ya mitaa, unakuta hayaji kwa sababu ya watu kufungwa fahamu na kuwa wajinga. Unakuta barabara inachimbika sababu ya kukosekana mtaro, watu wanapita hapo palipochimbika kwa miaka chungu nzima wakisubiri serikali ije kupaziba na kuwatengenezea mtaro. Unapiga hesabu unaona kama kila kaya ingetoa shilingi laki 1 kwa mwaka, mtaa wenye kaya 100 hiyo barabara ingekuwa imetengenezeka fresh. Au basi hiyo laki 1 ichangwe kwa miaka 3, lakini watu hawataki, wapo radhi kununua mabampa na bush kila baada ya miezi 6 ila kujitengenezea barabara hawataki, na huko waendako wana majumba ya mamilioni.

Magari yao yanakwanguka mabampa lakini wapo tu wanasubiri serikali ije kuwatengenezea. Fahamu zikishikiliwa ni ngumu sana kupata maendeleo.
 
Marehemu Happiness Kasmiry kutoka kijiji cha Usari wilaya ya Moshi. Alishikwa na ugonjwa wa tumbo wa kuhara na kutapika kwa siku kadhaa kabla ya kufariki dunia akiwa nyumbani kwake kutokana na Kukosekana kwa fedha ya matibabu.

Mume wa marehemu huyo ajulikanae kwa jina la John alihakangaika kutafuta pesa ya kumpeleka Hospital kwa siku kadhaa bila mafanikio.

Mume wa marehemu amesema alikuwa anakabiliwa na ukata mkubwa kutokana na kumuhudumia mama yake mzazi ambae amepooza upande mmoja wa mwili.

Marehemu ameacha watoto watatu wadogo.

Mwenyekiti wa kijiji hicho amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kusema ni kweli familia ilikosa namna ya kumpeleka kupata matibabu kutokana na ukata hivyo mama huyo kufariki dunia akiwa nyumbani kwake
Pole sana! Vipi wachaga wenzake wanaovimba humu kuwa wana hela walishindwa kumsaidia?
 
Back
Top Bottom