zwangandaba
JF-Expert Member
- Jan 31, 2023
- 747
- 1,404
Ndugu sangu meku.Marehemu Happiness kasmiry kutoka kijiji cha Usari wilaya ya Moshi. Alishikwa na ugonjwa wa tumbo wa kuhara na kutapika kwa siku kadhaa kabla ya kufariki dunia akiwa nyumbani kwake kutokana na Kukosekana kwa fedha ya matibabu.
Mume wa marehemu huyo ajulikanae kwa jina la John alihakangaika kutafuta pesa ya kumpeleka Hospital kwa siku kadhaa bila mafanikio.
Mume wa marehemu amesema alikuwa anakabiliwa na ukata mkubwa kutokana na kumuhudumia mama yake mzazi ambae amepooza upande mmoja wa mwili.
Marehemu ameacha watoto watatu wadogo.
Mwenyekiti wa kijiji hicho amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kusema ni kweli familia ilikosa namna ya kumpeleka kupata matibabu kutokana na ukata hivyo mama huyo kufariki dunia akiwa nyumbani kwake
Kwenye msiba wa marehemu najua mtanunua vyakula na kununua pombe watu kula na kuywa na kulewa.
Gharama ya sanduku la marehemu laki 5.
Gharama za msiba na mzishi milioni 3.
Marehemu kafariki kwa kukosa 20,000 tu ya kufika hospitali.
RIP ddangu Manka