21 April 2022
Moshi, Kilimanjaro
Tanzania
Madiwani 41 mkoani Kilimanjaro waandika barua ya kumkataa mkurugenzi
Madiwani 41wa Halmashauri ya Wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro, wameandika barua ya kumkataa mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Kastory Msigala wakimtuhumu kutumia maamizi binafsi kupitisha baadhi ya miradi ya maendeleo katika Halmashauri hiyo. Madiwani hao ambao waliandamana hadi ofisi ya Mkuu wa Mkoa kuwasilisha barua yao, wanalalamikia ukusanyaji wa mapato hafifu kutokana na utendaji usio shirikishi wa Mkurugenzi huyo pamoja, utolewaji wa maamuzi ya utekelezaji wa miradi bila kushirikisha kamati ya fedha na baraza la madiwani.
Source : mwananchi digital