Moshi: Mzazi ampiga na kumjeruhi mwalimu shuleni kwa kosa la kumuadhibu mwanae

Moshi: Mzazi ampiga na kumjeruhi mwalimu shuleni kwa kosa la kumuadhibu mwanae

Yeah hapo ndio kunapoleta shida! Kupiga kichwani na sehemu nyingine !!

Mi mwenyewe mzaziii uchungu naujua vizuri sana mbona!
Juzi mwalimu kanipigia simu mwanao mkorofiiii anapiga watoto wenzie anawapokonya sijui vitu gani anavitupa mara juzi kamsukuma mwenzie hadi jino lilitaka kutoka ananiambia imekua too much namchapa mwili ukasisimkaaa🤠🤠

Nikaumiaa nikamtetea hapana usimchape sana mwalimu hao ni watoto wadogo ukute wanakua kwenye kucheza tu hawaelewi muelekeze taratibuu kesho alivoenda shule ndani nikamvalisha ki jeans kigumu 😁😁😂😂!
Namwambia mwl akikuchapa jikaze usilie !

Lamomy Jr shule ni mkorofi balaa
Natamani ningekuwa mwalimu wa mwanao
 
Mwanafunzi kudeki shule kwani yeye analipwa na serikali hizi kazi za kudeki walimu ndio wafanye wao.
Mwalimu hajasomea kudeki amesomea kufundisha wanafunzi yaani transfer of knowledge. Achaga daharau kabisa . Kwa Tanzania wanafunzi ndio hudeki madarasa.
 
Why anakuwa mkorofi hivo??
Mbona baba yake anasemaga “Mambo yao waachie wenyewe” kwann asiige tabia za mshua wake Jr lakini?!!!
Baba ake mpole hata wampopoe yeye hajali maneno yake, “Binadamu wa siku hizi tatizo wabishi” 😂😂😂
Hebu mwambie aige Miongozo ya baba yake!!!
Jr mbona mkorofi jamani
Mmxieeeeeeeeww!

Umenza bange zako uduguuu!
 
Lkn mwalimu kufanya kazi ya usafi wakati mwanafunzi yupo hiyo naona sio sawa! Tutakua hatujawatendea haki walimu wetu, kikubwa ninachokiona kazi ziwe na kipimo, kazi ziwe za kumfundisha/kumjenga mtoto na sio kumkomoa.

Mimi ninachokipinga ni adhabu za kiuonezi na kikatiri kwa watoto wadogo zinazotolewa na walimu wasiojua maadili ya kazi zao
Ndiyo kielelezo
 
Siku moja nilitoa kichapo kwa mwanafunzi mmoja wa kike wa darasa la kike baada ya kukataa kunipikia chai asubuhi. Baada ya kumchapa viboko kadhaa kwa ubishi wake alikimbia nyumbani kwao kumleta baba yake.

Mzazi alikuja amefura hasira mpaka nyumbani kwa walimu eneo la shule akakosa mwalimu yupi amshambulie kwa kuwa walimu tulichanganyikana huku wengine wakiwa ni watu wazima na wenye miili mikubwa iliyojazia. Mzazi alirudi nyumbani kwake huku akitoa ole wake huyo mwalimu aliyemchapa mtoto wake angepigana naye. Tangu siku hiyo niliona isiwe taabu kuwatumia wanafunzi kwenye shughuli zangu binafsi.

Kuna mkuu mmoja wa shule ni wa kike alikuwa ni mbabe, mzazi akijitia kiherehere kwenda shuleni kuleta fujo alikuwa anamkwida na kumzabatua makofi na ngumi huku akimuambia anampeleka polisi. Wazazi wengine shuleni hawaji ila watatengeneza manuever kumkomoa mwalimu aliyechapa watoto wao. Mwalimu anaweza kujikuta katundikwa juu ya mti kalala huko usiku wote kimazingara. Wengine hufanyiwa vitendo vya kishirikina usiku
waalimu wanapiga sana watoto, hata mimi kuna mtoto alishawai pigwa vibaya sana na mwalimu, na niliwapatia shida sana wale walimu na shule nzima.
 
Back
Top Bottom