Mkuu baada ya Nyerere kutoka Uchina alianza mahaba nao ya ghafla sana, aliiga hadi mifumo yao ya ulinzi. Kule Uchina wana The Guoanbu (Foreign Intelligence) ambayo iko chini ya The Ministry of State Security, yenyewe kila kitengo kinakuwa na wakurugenzi wawili, yani mmoja ni wa kisiasia (Political Commissar) na mwingine ni wa kitaalamu (Technical Director).
Sasa kazi ya huyu Mkurugenzi wa kisiasa ni (Political Director) ni kuhakikisha kwamba taasisi ya ujasusi (The Guoanbu) inafuata matakwa ya chama cha kikomunisti cha Uchina wakati huyu mwingine ni kusimamia shughuli za kila siku za taasisi.
Hapa pana Checks and Balances kwasababu huyu mkuregenzi mmoja (Hasa yule wa siasa) kama akitoa amri ikakataliwa na mwingine (Yule wa kitaalamu) basi lazima atoe sababu za msingi kabisa kwanini amri yake ni muhimu na mwisho kabisa chama ndicho chenye usemi wa mwisho.
Mara ya kwanza Zhou Enlai anaanzisha shirika hili la Ujasusi la Uchina kipindi hicho likiitwa The Chinese Communist Party Central Investigation Department (Zhongyang Diaochabu) mwaka 1927 kule Shanghai. Watu walioajiriwa walikuwa ni vijana kutoka chama cha kikomunisti cha Uchina ambacho ndiyo kilikuwa kinaanza harakati zake.
Utaratibu huu ulikuwepo hata Ujerumani kipindi cha Mfalme Kaiza William ambapo Jeshi la Ujerumani lilikuwa na majemedari wawili kwenye nafasi moja ambapo moja ndiyo mwenye amri (Commanding Officer) na mwingine ni mtaalamu wa mikakati (Technical Expert) ambaye alitoka kwenye The Germany Generals Staff chombo ambacho kilikuwa kina watu wenye akili kupita kiasi.
Hapa napo pana Checks and Balances kama Jemedari moja (Commanding Officer) akikataa ushauri wa kitaalamu basi yule Technical Expert anaruhusiwa kuvunja itifaki na kwenda moja kwa moja kwa mfalme ili kutoa sababu kwanini ushauri wake ni muhimu kufuatwa na mfalme ndiyo anaamua.
Sasa mfumo huu tulioiga kutoka kwa Wachina siyo mbaya kivile, lakini ungekuwa na maana kama bado tungekuwa kwenye mfumo wa chama kimoja na Uchumi wa Kijama. Lakini pia kadiri siku zinavyoenda watu wanaoingia kwenye Idara ya Usalama wa Taifa ni watu wenye akili ndogo mno wasioweza kuchambua mambo mazito kwa kina, wasioweza kutunza siri, wachumia matumbo na walafi wa vyeo . This is a national crisis, believe me.