Moyo wangu umepondeka mno juu ya mahusiano yangu na huyu binti

Moyo wangu umepondeka mno juu ya mahusiano yangu na huyu binti

Habari wanajamii, nielekee kwenye hoja husika moja kwa moja.

Nilikuwa na matarajio mengi sana juu yake lakini imekuwa ndivyo sivyo. Nilifikiria sana baada ya kumfungulia thread/Uzi kwakuwa nilimhada na kumpenda sana ila haikuwa bahati yangu kama wasemavyo wahenga, ng’ombe wa maskini hazai, hili ni kweli kabisa.

Hivyo kwa hali hii baada ya kutambua ukweli nimeazimia kusonga mbele na kuweka akili yangu kwenye majukumu yangu zaidi. Nafahamu ipo siku nitapata mwingine mwenye upendo wa kweli zaidi ya huyu aliyeuponda na kuumiza mtima wangu, nina hakika Mungu atanipa mwongozo mzuri sana juu ya hili na kunisimamia vizuri katika hili.

NB: Wanawake wazuri na wenye hekima bado wapo wengi, sitakata tamaa ya kupenda kabisa, nitampata mzuri zaidi yake naamini.
Yupo humu tupe namba tukulipie kisasi hatuwezi kukubali mwamba ukaumizwa kifala namna hio 😎😎
 
Askofu 😀 kumbe zile story za kuwa makatekista wanakula masista ni za kweli🤣
Jamaa unadhani tunatumia wine ili iweje🤣🤣🤣🤣

Au unadhani tunawekewa mafuta ya taa kwenye msosi 😎
 
🙆🏾‍♀️😁😁😁
Unajua nini?

Unaweza kudhani JF ni mashuhuri sana kumbe sivyo. Data zao zinasema memba tumo karibia laki 7 sijui. Lakini ukiulizia mtaani huko hakuna anayeifahamu JF. Fanya kajaribio tu kesho uanze kuulizia watu huko mtaani, sokoni, kwenye daladala n.k. kama wanaifahamu JF. Hutapata mtu. Na hapa ni Dar. Vipi huko Misungwi na Namtumbo huko?

Kuna memba wachache sana hapa sema tu watu wamejaza mafyekero kibao kumbe ni watu wale wale. Na matokeo yake ndo haya sasa!

Melo inabidi aanzishe kampeni ya kuunganisha IDs zote na kuitangaza JF nchi nzima ili ipate wanachama wa kweli wanaoeleweka...
 
Jamaa unadhani tunatumia wine ili iweje🤣🤣🤣🤣

Au unadhani tunawekewa mafuta ya taa kwenye msosi 😎
haha ukila maharage unajaza protein mwilini unapata shida mvua zikinyesha kidogo😀
aisee waumini wakae chonjo kumbe mnawamezea sana mate wake za watu🤣
 
Back
Top Bottom