Mpangaji agoma kuhama baada ya mkataba kuisha. Nitumie mbinu gani kumtoa kwenye nyumba yangu?

Atathibisha vipi kuwa kaibiwa? hizo hela wakati mashahidi walikuwepo wakati vyombo vinatolewa?
Unaongea kihisia mwenzako naongea kiuzoefu kwa sababu nilishawahi kushuhudia.
Haihitaji kuthibitisha kwa sababu ni ndani kwake ndio sehemu salama kuhifadhi kitu chochote cha gharama anachojisikia kwa hiyo wewe ambae utakuwa umemuingilia faragha yake ndio utatakiwa uthibitishe kwamba hukuondoka na pesa zake,mchezo wa sheria sio jambo la kukariri huwa zinageukageuka kulingana na ujanja wa mtaalamu uliyesimama naye mahakamani.
Au kama hauniamini wewe fanya hivyo unavyowaza halafu mwisho wa kesi uje utupe mrejesho
 
Mpe hela yako akatafute chumba na akipata, mpe hela ya kusafirishia vyombo vyake kwenda kwenye makazi yake mapya, akigoma hapo ujue anatembea na mkeo.
 
Ungekuwa landlord ungeelewa mapungufu ya wapangaji ; sio wote!!! Shida iko kwa wabangaizaji 🤷🏻‍♂️🤷🏻‍♂️
Sema na wewe unakejeli mno, una shida mahali, mara unamuita single mother, mara hapa unasema mbangaizaji..Aisee wewe si unapaswa kujali pesa yako tu, hayo mengine mapungufu ya mtu yanahusu nini??Unafikir na wewe ungekuwa zipo za kutosha ungekuwa unampigia kelele mpangaji kisa hajalipa miezi mitatu???
Mtu kaingia hata miaka miwili hana tayari unafanya ukaratabati??Hii kama sio mtafutano ni nini aisee au kuna kitu ulirequest - access ikawa denied..ndo unataka kutumia umwamba??
 
Hata mimi nimemshangaa hiyo kodi anayolipwa ni ya kazi gani?
Hivi dereva wa taxi au uber anavyotukodisha gari yake ikitokea uchakavu au breakdown naye atulipishe hela nyingine ya ziada ya kununua vipuri ina make sense?
 
Huyo jamaa ni aina fulani ya wenye nyumba wanaopenda kuvimba yaani anyenyekewe muda wote kisa ana nyumba as if mpangaji anakaa bure,ni aina ya watu wanaodhani kila mtu aliyepanga ni maskini.
 
Kama hajafanya kosa lolote la kuvunja vipengele vya mkataba, huna haki ya kumuondoa kwenye nyumbani. The best you can do ni kumpangishia nyumbani sehemu nyingine while the repair is on-going.
 
Mamndenyi

Baadhi ya __"kipato huleta majivuno"
 
Mtoa mada badili kitasa akirudi akute ufunguo mpya kuliko utoe vitu Kwa force lazima polis utaenda so short way badili kitasa ili asiingie kama utaki atumie iyo nyumba
 
Unajua wafanyabiashara wanaokwenda Dubai na China wanakata miezi mitatu huko alafu wanarudi na mzigo? Unafikiri wanakwenda kufanya biashara gani? Ni hatari kuomba access kwa watu kama hao🤷🏻‍♂️
 
Tafuta Njagu mpange mum bambike kesi ya kuhifadhi bange nyumbani kwako
 
Na wewe weka kufuli lako juu ya mlango,siku akija mlipishe gharama aliyozidisha kwa kumuhifadhia vitu vyake,akigoma unafidia kwa vitu vyake,ubaya ubwela
 
Njoo na elf 35 mkuu tumtupie jin liwe limamchapa bakora kila akisinzia tu ndam ya nyumba
 
Umempata mpangaji boya mm ningepita na shingo yako huwa sipendag unyonyaji
 
Hiyo security deposit ilitakiwa kama mpangaji haja fanya uharibifu arudishiwe mpangaji, ila kama mpangaji kafanya uharibifu wa Vitasa, mlango au Dirisha kumtaka inakua sahii.
 
Wakati mwingine huruma na uungwana unahitqjika
Hela yake mpe tu na maisha yasonge hujui alikoipata

Wakati mwingine unaepusha usumbufu na pia utu
Unaweza kwenda kushitaki ukaliwa hela zaidi ya hiyo deposit

Mpe na kama ana shida muongezee aende kwa amani
 
Mtupie jini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…