Hiyo Ballot paper jinsi ilivyo:
1. Itawachosha wapiga kura kutafuta jina la Lissu, maana watu wana tabia ya kuscan vitu top- bottom
2. Kutakuwa na confusion kati ya CHADEMA na CHAUMA, maana CHAUMA inaanza kutokea kabla ya CHADEMA
3. Kwenye column za majina wameweka majina ya Wagombea wenza kwanza kabla ya mgombea urais, hii itawaconfuse wale wasiotake time kuscan paper nzima. Kwa upande wa CCM itakuwa ni rahisi kumtambua mama Samia kuwa ndiye mwenza wa Magufuli, ila kwa wale wanaomjua Lissu tu kabla ya Salum Mwalimu wanaweza kushindwa kumlink Salum na Lissu. Ilitakiwa majina ya wagombea urais yawe Column ya kwanza na wagombea wenza Column ya pili
4. Kwa mpiga kura process ya utafutaji mtu wa kumpigia kwenye hiyo karatasi, iwapo watu wasipojua in advance mtu wamtakaye alipo, inaweza kuchukua muda mrefu kwa mpiga kura mmoja mmoja kukaa ndani ya kile chumba cha kupigia kura . Kwa hiyo hizo ballot paper zilivyotengenezwa zitapelekea muda wa kupiga kura uishe kabla ya watu wengi hawajapiga.
Hii ni advantage kwa CCM kama watahamasisha watu wao wapige mapema, yaani watakuwa mbele kwenye queue na kumaximize time ya upigaji Yaani kama ikichukua sekunde 2 kwa mpiga kura wa CCM kuweka tiki kwenye jina la JPM, itamchukua sekunde si chini ya 8 kwa mpiga kura wa Lissu kusearch jina la Lissu(kama hajui lilipo). Hii itapelekea wapiga kura wengi wa CCM kufanya yao huku wapiga kura wa CHADEMA wakiwa nyuma huko kwenye queue na matokeo yake muda umeisha halafu wamepiga kura kiduchu.
Solution ya hii ni kuelimisha wapiga kura, sasa sijajua kama muda wa kuelimisha wapiga kura nchi nzima kwa sasa ni wa kutosha maana nchi ni kubwa sana hii, na watu wengi huenda ujumbe ukachelewa kuwafikia
Lakini kuneutralize hilo ni kuwahi kwenda kupiga kura ikitokea randomness ya kutosha kwenye queue za kupiga kura, basi advantage hiyo ya juu hapo haitokuwepo sana, Ila wakiwahi wa CCM na kupiga mapema, Upinzani itakula kwao.
Kwa hiyo kiufupi solution ya hilo suala ni kama ifuatavyo:.
1. Elimu kwa wapiga kura, juu ya hiyo karatasi ilivyokaa
2. Kutumia nembo ya chama ya vidole viwili kama search method, yaani wapiga kura waambiwe, ilinkumtafuta Lissu alipo tafuta nembo ya vidole viwili, hapo utaliona jina la Lissu
3. Kuhakikisha wapiga kura wa Lissu wanawahi vituoni ili kuwaondolea CCM advantage ya kupiga kura zao nyingi mapema
4. Kuanzia sasa kila mkutano atakaopiga Lissu hasa kwenye maeneo na mikoa yenye Literacy level ndogo awahimize wananchi kutafuta jina lake (asiwaambie liko mwisho, isije ikatokea liko katikati) kwa kutumia alama ya vidole vya nembo ya Chama cha Chadema, Kauli ya Lissu itasambaa kwa haraka, na pia wabunge na madiwani wa Chadema waelezwe kutoa elimu hii ya kutafuta mgombea kwa kutumia nembo ya chama kwenye mikutano yao ya kampeni!