Wanabodi,
Declaration of Interest
Mimi ni Mkatoliki, nimelisoma tamko hili,
News Alert: - Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC): Hatuungi mkono Mkataba wa Bandari. Sauti ya Watu ni sauti ya Mungu naulizia, huku sio kuchanganya dini na siasa?.
Kama Mama Samia ndiye Mkuu wa nchi, ameikubali DPW, ameileta, Bunge ambalo ndio wawakilishi halali wa wananchi wameikubali, CCM ndio chama cha Watanzania, wameikubali DPW, mhimili wa Mahakama umeikubali DPW, who the hell is TEC ikatae DPW?
Kufuatia kila rais wa JMT anapokuwa ni Mkristo ni lazima awe Mkatoliki, Nyerere alikuwa Mkatoliki, Mkapa Mkatoliki na Magufuli Mkatoliki, kuna uwezekano Wakatoliki wamedekezwa na sasa wameota pembe na kuthubutu kumgomea Mama kwasababu sio Mkatoliki?.
Tuambiane ukweli, angekuwa ni Magufuli ameileta DPW, TEC wangetoa waraka huu?.
Kuna mabaya mangapi yamefanywa na marais Wakatoliki lakini TEC wamenyamaza?. Kuna kosa kubwa zaidi ya rais wa JMT kukiuka katiba?. Mbona rais Mkatoliki alikiuka katiba na TEC walikuwepo, mbona sikuona waraka?.
Paskali