Mpenzi wangu anasita kujenga juu ya kiwanja changu

Mpenzi wangu anasita kujenga juu ya kiwanja changu

Hii ilitakiwa tumshauri yeye huyo mpenzi wako.

Lakini ktk hiyo asijaribu kujenga kwenye hicho kiwanja chako. Nyie wanawake hamuelewekagi. Mkishikwa kidogo akili na kupangwa,unageuka kabisa. Leo unajiona huwezi kufanya chochote ikitokea lolote huko mbele,lakini amini huko mbele hautakuwa wewe tena, shetani amekaa katikati yenu wanawake. Akijenga kwenye hicho kiwanja ahesabu amepoteza. Anunue tu uwanja mwingine sio huo wako. Kama amesita kujenga kwenye huo uwanja jua kabisa umepata mwanaume. Na asisite,akatae kabisa wala fikra zisiwepo.
Na usimshawishi tena kujenga hapo. Baadae uzeni hicho kiwanja ingizeni kwenye mambo yenu mengine mchanganyiko
Mmh okay sawa
 
Mimi nashauri kila mmoja awe na uwanja wake na nyumba yake.

Hapo hata mimi nayaona matatizo. Kwanza oaneni wacheni uzinzi na uasherati.


Uislam raha sana, hata mke na mume kila mmoja ana mali yake, hakuna ujinga wa sijuwi tulijenga nae.

Fateni sheria ya kila mtu kumiliki chake. Lakini mnaofanya haramu sijuwi kama mtanielewa.
Sawa Dada nimempa room ya kuangalia namna bora kama ataafiki sawa
 
Tulianza mahusiano amenikuta na kiwanja kikubwa tu, nikamshauri pesa aingize kwenye ujenzi haina haja ya kununua kiwanja, ila amekuwa mzito kujenga juu ya ardhi ile, anadai siku mambo yakienda ndivyo sivyo atapoteza property. [emoji848]

Sio ubinafsi huo? Na why muwaze kuachana mpaka ugomvi wa mali kuhusishwa? Anyways nimemshauri aangalie namna itakayofaa.
Sasa tuseme amejenga kwenye kiwanja chako, ikaja tokea siku mkagombana na kuachana utamwambia achukue nyumba yake na akuachie kiwanja chako? Ushauri wangu ni aidha umuuzie hichi kiwanja, au muandikiane kisheria kuwa unampa yeye hicho kiwanja na hutomdai mkifarikiana (hakuna anaeweza kutabiri kitakachotokea kesha), au muingie ubia akulipe nusu ya pesa ulizonunua kiwanja na halafu muanze kujenga pamoja kwa pesa zenu nyote wawili, hapo ikitokea mtafaruku itakuwa ni rahisi kugawana/kulipana mali.
 
Tambua mwanaume mwenye akili timamu hawezi kufanya unachotaka ni hali tu ya kiuanaume kwanza akijenga hapo hatakua na amani atakua anahisi udhaifu fulani , kwanza hata hicho kiwanja chako hatakiwi kukuuliza una mipango nacho gani.... Wanaume hata tukikwama ni ngumu kuomba msaada kwenu labda sasa ujongeze wewe kuona mumeo anahitaji support yako na mwambie ongezea nguvu pale kwa mwanamke anaejitambua, kwa mwanaume ukianza kuegemea kwenye vitu vya mwanamke hilo ni anguko, mwanamke afanye vitu kwa mapenzi yake mwenyewe sio kuombwa
Mh sawa hakuna tatizo nilishauri tu
 
Tulianza mahusiano amenikuta na kiwanja kikubwa tu, nikamshauri pesa aingize kwenye ujenzi haina haja ya kununua kiwanja, ila amekuwa mzito kujenga juu ya ardhi ile, anadai siku mambo yakienda ndivyo sivyo atapoteza property. [emoji848]

Sio ubinafsi huo? Na why muwaze kuachana mpaka ugomvi wa mali kuhusishwa? Anyways nimemshauri aangalie namna itakayofaa.
Badilisha hati ya uwanja iwe jina la mmewe Kama Ni unajua Mana ya mke labda utakuwa unajua Mana ya mwanamke na sio mke
 
Back
Top Bottom