Mpira wa Ulaya umekuwa wa kizembe sana nowdays kuliko Afrika

Mpira wa Ulaya umekuwa wa kizembe sana nowdays kuliko Afrika

Kwa mtazamo wangu mpira wa Ulaya ulianza kushuka baada ya Italy kuporomoka kisoka, kuanzia ligi na vilabu vyao hadi timu yao ya taifa.

Italy ndiyo ulikuwa muhimili wa soka la Ulaya na ilikuwa hauwezi kuitwa mchezaji bora duniani hadi uwe unachezea moja ya vilabu vya Italy. Ligi za France na Germany zimeshindwa kuziba hilo pengo la Italy kiufasaha pamoja na kwamba timu zao za taifa zimekuwa zinafanya vizuri.

Nasemaga siku zote EPL haijawahi kuwa ligi bora Ulaya, imepandishwa tu na marketing na kwa kiasi naweza kusema inachangia kuvuruga muelekeo wa mpira wa Ulaya.
Watu wengi hua tunabishana sana kuhusu hili swala lakini ukweli usemwe EPL haijawahi kua ligi Bora duniani. Nembo za mpira ni Italy na Spain then ndo tunakuja england...

Ukitaka kuamini taja malegend wa EPL then walinganishe na wale wa Seria A na Laliga ni mbingu na ardhi..
 
Cha kwanza kwangu Mimi hapana.
Kuhusu mafanikio hiyo ni debatable. Kama ni mafanikio ya pesa ni jinsi unavyo bargain mikataba na nguvu ya ushawishi ya management yako kukupandisha hadhi. Mane alikuwa anakula pesa ndogo kuliko bench warmers wengi pale Liverpool.
Makombe aliyonyanyua Messi ni mengi Messi ana UEFA 4 zidane je?
 
Cha kwanza kwangu Mimi hapana.
Kuhusu mafanikio hiyo ni debatable. Kama ni mafanikio ya pesa ni jinsi unavyo bargain mikataba na nguvu ya ushawishi ya management yako kukupandisha hadhi. Mane alikuwa anakula pesa ndogo kuliko bench warmers wengi pale Liverpool.
Kwenye individual achievements Messi ana tuzo nyingi kumzidi zidane

Zidane linganisha tu na XAVI na INIESTA sio kwa messi
 
Nilikuwa siambiwi kitu Kwa Man U
Man U ikifungwa Hata chakula Kilikuwa Hakiliki
Kwasasa Sijui hata Imecheza Lini
Sijui ina points ngap
Nikiambiwa Imefungwa Kama Vile nimeambiwa Kuna Mbuzi kapotea huko Malawi!!
Yaani hata Roho Kustuka hakuna!
Nimebakia na Simba hii ndio Inayo nitesa sana japo Simuda nayo ...
Upokama mimi mpka nikaitwa Manchester kama jina langu ila now hata sijui jezi yao ina mdhamini gani mwisho wangu ni ile AIG
 
Mabadiliko ya kwenye mpira hayajaanza leo, kama kuna mtu amepata nafasi na kuitizama movie ya pele ataelewa lengo la wazungu kwenye soka na wamefanikiwa kwa asilimia ngapi.

Kwa sasa mpira sio kipaji tena ni taaluma kama taaluma nyingine tu, unafundishwa unaelewa kupokea pasi kukaba na kutoa pasi mchezo imeisha.

Maswala ya vyenga ubunifu na talents zimekwisha zama zake sasa ni soka tactics.

Let’s go wanangu wa soka, enjoy tactics.
 
Okay Sasa tumeelewana tumetoka ktk vipaji na mafanikio ya kipesa tuko ktk tunzo Sasa si ndiyo bosi?
Hata kipaji Messi anamzigi mbali mno zidane au kipaji kwako ni Nini? Kupiga kanzu na tobo?

Izo pia Messi kazi piga

Kipaji ni intelligence ya kupiga pass za mwisho ASSIT unamchungulia mtu unaweka icho ni kipaji art

Kuscore pia sio Kila mtu anafunga Messi amefunga mara 5 ya magoli ya zidane career yote je hicho sio kipaji?

Najua ata tukianza hesabu tobo chenga na kanzu I guess Messi kamzidi zidane alio wa humiliate

Au kipaji kwako unaki define vipi?
 
Mabadiliko ya kwenye mpira hayajaanza leo, kama kuna mtu amepata nafasi na kuitizama movie ya pele ataelewa lengo la wazungu kwenye soka na wamefanikiwa kwa asilimia ngapi.

Kwa sasa mpira sio kipaji tena ni taaluma kama taaluma nyingine tu, unafundishwa unaelewa kupokea pasi kukaba na kutoa pasi mchezo imeisha.

Maswala ya vyenga ubunifu na talents zimekwisha zama zake sasa ni soka tactics.

Let’s go wanangu wa soka, enjoy tactics.
Chukua Usain bolt si ana mbio talent mfundishe kukaba na kutoa pass then uone kama atafanya chochote
 
I salute you kinsmen.
Binafsi nimeanza kufuatilia soka la ulaya muda kidogo Liverpool die hard fans.

Lakini tuseme ukweli ligi za ulaya kwa sasa uwezo wa wachezaji umekuwa mdogo sana na hakuna vipaji kabisa asilia yaani ile pure talent hakuna kabisa.

Hasa hasa EPL nowdays huwa nafuatilia game za Liverpool basi tu sababu ya kuipenda team ila kwa sasa sioni zile pure talent kama zama zile ..

Tulikuwaga na Xabi alonso anazima pale na mascherano kati halafu Steven Gerald. Lakini leo tuna wataru Hendo,

Tukikuwaga na watu wa kazi Denis Bergkamp pale arsenal lakini leo tuna Gabriel jesus, na taka taka zingine kama Halaand pale Man City.

Hebu fikiria watu kazi kama Vidic,Rio ferdinand, Ashley Cole, patrice Evra,dirk kuyt, hawapo tena,

hebu wazia pale Qpl ya moto enzi zile yaani full kuenjoy.

Binafsi ukiniuliza nitakwambia kwa sasa CAF champions league ni bora kuliko Uefa ya sasa hivi . UEFA ya mwisho kuwa nzuri zaidi ni ile 2015/2016! Baada ya hapo ni maigizo matupu na ujinga ujinga.

Wachezaji nowdays wamekariri mifumo kutoka kwa makocha kama maroboti yaani hatuoni zile extra talent kutoka kwao .

Sikuhizi mchezaji kufunga goli la uwezo binafsi ni ngumu sana sana zaidi ya kufuata mfumo kama robot..

Naamini Neymar ndiyo talent ya mwisho ambayo ilibaki na ilitegemewa kufanya makubwa lakini ndio vile mnamuona tena mwenyewe kijana umri umesogea..

Nadhani ligi ya EPL ndiyo imeshakuwa ya kidwanzi sana kufuatilia hakuna tena soka la burudani kama zamani zaidi mifumo mipya ya hovyo wachezaji waifuate kama robot.

No wonder wachezaji kama Halaand wanacheza na wanaonekana bora sana, na wanafikia mpka kugombania tuzo kubwa kubwa ni ujinga.

Marefa wa epl ndio kituko kabisa hawana tofauti na huku Bongo wana VAR lakini bado maamuzi ni kichekesho.

Angalau Spain bado wana mpira wao asili kidogo unafurahia kuenjoy.

Afadhali hata ligi ya Tanzania kuna magoli yanafungwa unaona kabisa huu ni uwezo binafsi kabisa kuliko EPL ya sasa aseeh
Nilishaacha kufuatilia mpira baada ya kuelewa hilo. Tena enzi hizi za kubet ndio kabisaa unaona mechi zinapangwa
 
Hata kipaji Messi anamzigi mbali mno zidane au kipaji kwako ni Nini? Kupiga kanzu na tobo?

Izo pia Messi kazi piga

Kipaji ni intelligence ya kupiga pass za mwisho ASSIT unamchungulia mtu unaweka icho ni kipaji art

Kuscore pia sio Kila mtu anafunga Messi amefunga mara 5 ya magoli ya zidane career yote je hicho sio kipaji?

Najua ata tukianza hesabu tobo chenga na kanzu I guess Messi kamzidi zidane alio wa humiliate

Au kipaji kwako unaki define vipi?
Wakati ukiendelea kumsifia Messi kumzidi Zinedine kumbuka Zidane kafanya kipindi gani na akina nani na Messi kafanya kipindi gani na akina nani. Sipingi Messi kuwa na kipaji ila sijakiona kikimzidi Zidane au hata Ronadinho.
Kwahiyo, we endelea kuamini unavyoamini na Mimi niendelee kuamini hivi.
 
Kwamba Zidane ana kipaji kumzidi Messi? Yaani Zidane ni goat mbele ya Messi. Sawa ni mtizamo wako.
 
Wakati ukiendelea kumsifia Messi kumzidi Zinedine kumbuka Zidane kafanya kipindi gani na akina nani na Messi kafanya kipindi gani na akina nani. Sipingi Messi kuwa na kipaji ila sijakiona kikimzidi Zidane au hata Ronadinho.
Kwahiyo, we endelea kuamini unavyoamini na Mimi niendelee kuamini hivi.
Kipaji kipi alichonacho zidane Messi hana?

Nikuulize kitu kitu Gani zidane kafanya na RONALDINHO kuhusu Mpira Neymar hajafanya?

Taja KIKOSI full Cha Madrid ya zidane na Barca ya Ronaldinho na Mimi nitaje team zenye wachezaji wanaolingana na hao wa vikosi vya sasa
 
Watu wengi hua tunabishana sana kuhusu hili swala lakini ukweli usemwe EPL haijawahi kua ligi Bora duniani. Nembo za mpira ni Italy na Spain then ndo tunakuja england...

Ukitaka kuamini taja malegend wa EPL then walinganishe na wale wa Seria A na Laliga ni mbingu na ardhi..
Eti Ganacho, Gabriel Jesus au Gakpo apige chenga halafu akafunge hapa 🤣
 
Attachments

  • images (97).jpeg
    images (97).jpeg
    32.2 KB · Views: 2
Chukua Usain bolt si ana mbio talent mfundishe kukaba na kutoa pass then uone kama atafanya chochote
We nae hufuatilii vitu usain bolt ni Mchezaji wa mpira wa miguu na kuna kipindi alitaka kujiunga na man united kocha ndiyo hakuwa na matumizi nae hakukubali kumpa kandarasi
 
Chukua Usain bolt si ana mbio talent mfundishe kukaba na kutoa pass then uone kama atafanya chochote
Usain bolt amecheza ligi ya Australia kwenye timu inayoitwa central coast mariners 2018, bado akafanya majaribio Borusia Dortmund, na akawa anataka asajili Man U.

Fuatilia mambo, mpira umebadilika mno mambo ya talent yameisha, saivi ni curiosity ya mtu na uwezo wa kuelewa mifumo then unacheza, usitegemee kuja kuona vipaji kama vya kina samuel etoo, Ronaldinho Gaucho, Ronaldo de Lima, Raul, Puyol, Reuben Arjen, Frank Ribery, Iniesta, Xavi Alonso, Xabi alonso, kina Thiery Hendry, Didie drogba, Kaka, Yaya Toure, zinadine Zidane, Thuram, Mario Baloteli, Diego Armando Maradona, Lionel Messi, Christiano Ronaldo na wengine wengi.

Ukipata nafasi angalia movie ya Pele, utajifunza mengi kwenye mpira hutoshangaa hiki unachokiona sasa mana ilikuwa ni kampeni tangu zaman kupiga vita mpira unaotegemea vipaji na uwezo binafsi kwa kulazimisha mifumo.

Pele mwenyewe alilitia wakati mgumu kupata nafasi kwenye timu za wazungu hadi ilipoaminika kuwa uwezo wake binafsi kuna muda unahitajika ili timu kupata matokeo.
 
DROGBA alikuwa na kipaji?

Acheni basi
 
Messi na Ronaldo hao pia ni vipaji vya zamani vinavyoishia sema tu wamechelewa kustaafu soka kama wenzao kina Rooney,Terry,na wengineo. Vipaji vya zamani vilikuwa vinaleta raha kutizama tofauti na sasa tunaenda kutizama mbinu za mwalimu tu na mwenye mbinu bora ndo anayeshinda mechi kama ilivyo kwa Pep wa Barca, Bayern Munich na sasa Man City
 
Back
Top Bottom