Wakipekee
JF-Expert Member
- Aug 21, 2019
- 6,194
- 10,711
Watu wengi hua tunabishana sana kuhusu hili swala lakini ukweli usemwe EPL haijawahi kua ligi Bora duniani. Nembo za mpira ni Italy na Spain then ndo tunakuja england...Kwa mtazamo wangu mpira wa Ulaya ulianza kushuka baada ya Italy kuporomoka kisoka, kuanzia ligi na vilabu vyao hadi timu yao ya taifa.
Italy ndiyo ulikuwa muhimili wa soka la Ulaya na ilikuwa hauwezi kuitwa mchezaji bora duniani hadi uwe unachezea moja ya vilabu vya Italy. Ligi za France na Germany zimeshindwa kuziba hilo pengo la Italy kiufasaha pamoja na kwamba timu zao za taifa zimekuwa zinafanya vizuri.
Nasemaga siku zote EPL haijawahi kuwa ligi bora Ulaya, imepandishwa tu na marketing na kwa kiasi naweza kusema inachangia kuvuruga muelekeo wa mpira wa Ulaya.
Ukitaka kuamini taja malegend wa EPL then walinganishe na wale wa Seria A na Laliga ni mbingu na ardhi..