Mpwayungu yupo sahihi, hii kazi ya ualimu ni ngumu sana

Mpwayungu yupo sahihi, hii kazi ya ualimu ni ngumu sana

Hao private mkuu, walimu wa serikali hasa advanced wana muda mwingi.
Nimesoma shule fulani mwalimu wa geo hafundishi, anafundisha shule provate na ana tuition center, mkitaka awafundishe mnachanga pesa mnamlipa.
Shule inajua lakini wala hakuna anayejali.
Jamaa ana pesa ana hadi ghorofa na ni mashuhuri kwa somo hilo huo mkoa.
Private huwezi kufanya hivyo maana wanataka wakukamue hadi tone lako la mwisho.
Mwalimu wa shule private kutoboa ni ngumu kabisa.
uyo anakula na watu, ukipata mkuu wa shule anakomaa na utendaji wa walimu ,hata serikalini utoboi.

Tena huko serikalini kuna kusimamia mpaka bustani , usafi, mikondo mpaka e, darasa watoto mia, madaftali kusaisha kama mlima
 
Elimu ya SASA sio kama ile ya zamani!

Vitabu hamna wala internet no materials!!KWA sasa kuna topic GANI haina material!!?

Kuna swali GANI halina materials kama sio kutaka kuonyesha u deepness usio na maana!!?

Uwalimu wa leo ni competence based hakuna haja ya kujaza ubao mara tatu kama zamani!!

Wape class activity wajaze wa discuss uone kama wanashindwa vijana!inabaki kutoa muongozo KWA baadhi yasiyoeleweka vizuri!!

Nenda chuo chochote tz kama wanafundisha teacher centred!!

Mambo yamebadilika SASA wanafunzi ndio wenye materials sisi ni wawezeshaji wa mjadala!!!

Chukua hiyo!!
Ukitumia njia hii kwa O level wanafunzi watafeli wengi saana hasa katika masomo ya Physics, biology, chemistry, mathematics and Geography,

Wanafunzi wengi wa o level ubongo unakuwa bado haujakomaa
 
Ukitumia njia hii kwa O level wanafunzi watafeli wengi saana hasa katika masomo ya Physics, biology, chemistry, mathematics and Geography,

Wanafunzi wengi wa o level ubongo unakuwa bado haujakomaa
Ata A level isipokua tu kwa wale brightest kwenye special schools .ila wengi kwenye hizi private schools ni okota okota hamna kitu.
 
Umevuka mipaka mkuu. Sasa ishauri serikali wafute hii kazi isiwepo kabisa maana imelaaniwa kama unavyodai. Mnapenda kuidharau hii kazi na kuwatukana waalimu wakati watoto wenu mnawepeleka huko huko shuleni kwa waalimu.
Siyo watoto wao tu.
Kwani wao wenyewe kabla hawajawa na hizo kazi zao hawakufinyangwa na hao walimu.
Fact ni kazi ngumu lakini huwezi kusema ni kazi ya laana.
 
Advance!?masomo GANI hayo!?

Usi complicate mambo kufundisha simple sana!

TENA advance!unatumia mbinu gani!?au we BADO unatumia teacher centred Ili uwaonyeshe upo deep sio!!?

Mi napiga chemistry na bios ordinary level and never suffocate!!

Ugumu unaufanya wewe mwenyewe!!!

"Easy does it" norman vincent peale!!
Nyie ndio aina ya walimu mnaofundisha organic chemistry kwa siku moja
 
Maskini na watoto wa wakulima ndio wengi wameridhika na Ualimu.

Middle class wengi huwezi waakuta kwenye Ualimu na walioingia huku wengi baada ya muda wanaacha na kufanya mishe zingine.
Mshahara wa 479000 Kwa certificate anaeanza ni kidogo? Bado diploma ni zaid ya 600000 degree kuanzia 770000 Bado mnasema ni kidogo?
Bado ukistaafu mafao zaidi ya mil100
 
Mshahara wa 479000 Kwa certificate anaeanza ni kidogo? Bado diploma ni zaid ya 600000 degree kuanzia 770000 Bado mnasema ni kidogo?
Bado ukistaafu mafao zaidi ya mil100
We ni Mwanasiasa,, ?? Mtumishi au Mkulima ??

TGTS B 479000

TGTS C 636,000

TGTS D 771000

Hapo hakuna extra duty, overtime, perdiem,, on transit,,, Wala posho.

Hiyo pesa ule, uvae, ujitibu, ulipe Kodi, usaidie ndugu na usomeshe !!???

Acha utani ndugu hiyo hela kuna watu ndio posho yao ya siku moja tuu...

WANAOFANYA KAZI YA UALIMU NI MASKINI WASIO NA MITAJI AU WATU WA KUWABEBA FULL STOP [emoji611][emoji611][emoji611]..

UALIMU sio kazi ya kujivunia ni vile tu watu hawana namna.
 
Kazi ya ualimu ni wito. Patakuja kutokea kiongozi mmoja ambaye atasababisha kila mtu kuipenda kazi ya ualimu kwa malipo mazuri na mazingira mazuri ya kufanyia kazi.

tuombe Mungu na wote wanaodharau kazi ya ualimu ni watu wasiokuwa na shukurani kwani nikikumbuka nilivyokuwa sijui kusoma na sasa najua kusoma nawashukuru walimu wote walionifundisha na kunifanya niwe hapa nilipo.
 
Sasa mkiacha kazi nani atafundisha vijana ! Tunawaheshimu na tunawapenda !
Msikate tamaa humo humo kwenye ugumu wa kazi tafuteni upenyo wa kutokea iwe kwa michongo yako ya nje au humo humo kwenye kazi yako!
Pambana, kote ni kugumu labda wanaopata nafasi za kupiga rushwa au kuhujumu ugumu wa huko unatokana na kwamba unachokula ni kile unachopangiwa tu.
Wasanii si wapo

Watawaafundisha tu

Ova
 
Kazi ya ualimu ni wito. Patakuja kutokea kiongozi mmoja ambaye atasababisha kila mtu kuipenda kazi ya ualimu kwa malipo mazuri na mazingira mazuri ya kufanyia kazi.

tuombe Mungu na wote wanaodharau kazi ya ualimu ni watu wasiokuwa na shukurani kwani nikikumbuka nilivyokuwa sijui kusoma na sasa najua kusoma nawashukuru walimu wote walionifundisha na kunifanya niwe hapa nilipo.
Shida sio kazi bali maslahi na mazingira ya kazi yenyewe.

Huwezi kukuta watoto wa viongozi au Wana siasa kwenye kazi ya UALIMU ndio ujue sio kazi ya kufanya.

Kazi nzuri ni ile yenye maslahi Bora na mazingira mazuri ya kazi. UALIMU unakosa hayo yote mawili.

Kwa nini wito uwe kwa maskini tu na wakulima waliokosa ada za kada zingine.
 
Kama ni kazi ngumu iache. Mimi nilishawahi kuwa mwalimu kwa mwaka mmoja kupitia crash program enzi za Kikwete. Niliacha sababu kuu ikiwa kwenda kujiongezea elimu zaidi na pia niliona sina wito nayo. Nilikuwa sieleweki kabisa kwa wanafunzi. Nikiingia class mimi mwenyewe ndo nilikuwa naelewa. Nikaona niache nikasome.

Kuhusu kwamba unatakiwa ujisomee sana ni kweli na inaweza kukusumbua tu mwanzoni lakini baada ya muda mfupi unakuwa fit. Na hii ya kujisomea ni rahisi zaidi kama ulienda kuwa mwalimu ukiwa ulifanya vizuri kwenye masomo unayofundisha na sio umeenda ualimu kisa ulifeli na kutopata admission ya kitu unachopenda chuo.

Mshahara kweli ni mdogo ila ukiwa na akili plus nidhamu ya fedha unachomoka tu kirahisi na wewe kuwa mwalimu tajiri. Tatizo ni kuwa waalimu wengi wanatoka familia duni kwahiyo kuanzia ule mshahara wa kwanza lazima agawie familia yake. Changamoto ya waalimu wengi ni roho ya unyonge waliyo nayo. Wengi wana ndoto ndogondogo.
 
Ukimchukua leo mtoto wa tajiri mmoja ambae alikua anapewa 500k kwaajili ya matumizi yake madogo madogo ya shuleni, ukimpa ajira ya mshahara wa 700k ni lazima ataitukana hiyo kazi na ataiacha haraka sana.

Ila ukimchukua mtoto wa masikin aliekua anapewa matumaini tu kuwa nenda shule nikipata ntakutumia hela ya matumizi na anaondoka akiwa hana kitu ukimpa kazi ya mshahara wa 700k ni lazima ataithamini sana.

Unajua kwanini? Maisha magumu ndo yanatufundisha kuthamani vitu, hakuna anaependa kufanya kazi ngumu.
Ndio. Upo sahihi. Hao maskini ndio wapo tele kwenye kada ya Ualimu ikifuatiwa na majeshi yetu yote.
 
Back
Top Bottom