Mpwayungu yupo sahihi, hii kazi ya ualimu ni ngumu sana

uyo anakula na watu, ukipata mkuu wa shule anakomaa na utendaji wa walimu ,hata serikalini utoboi.

Tena huko serikalini kuna kusimamia mpaka bustani , usafi, mikondo mpaka e, darasa watoto mia, madaftali kusaisha kama mlima
 
Ukitumia njia hii kwa O level wanafunzi watafeli wengi saana hasa katika masomo ya Physics, biology, chemistry, mathematics and Geography,

Wanafunzi wengi wa o level ubongo unakuwa bado haujakomaa
 
Ukitumia njia hii kwa O level wanafunzi watafeli wengi saana hasa katika masomo ya Physics, biology, chemistry, mathematics and Geography,

Wanafunzi wengi wa o level ubongo unakuwa bado haujakomaa
Ata A level isipokua tu kwa wale brightest kwenye special schools .ila wengi kwenye hizi private schools ni okota okota hamna kitu.
 
Umevuka mipaka mkuu. Sasa ishauri serikali wafute hii kazi isiwepo kabisa maana imelaaniwa kama unavyodai. Mnapenda kuidharau hii kazi na kuwatukana waalimu wakati watoto wenu mnawepeleka huko huko shuleni kwa waalimu.
Siyo watoto wao tu.
Kwani wao wenyewe kabla hawajawa na hizo kazi zao hawakufinyangwa na hao walimu.
Fact ni kazi ngumu lakini huwezi kusema ni kazi ya laana.
 
Nyie ndio aina ya walimu mnaofundisha organic chemistry kwa siku moja
 
Maskini na watoto wa wakulima ndio wengi wameridhika na Ualimu.

Middle class wengi huwezi waakuta kwenye Ualimu na walioingia huku wengi baada ya muda wanaacha na kufanya mishe zingine.
Mshahara wa 479000 Kwa certificate anaeanza ni kidogo? Bado diploma ni zaid ya 600000 degree kuanzia 770000 Bado mnasema ni kidogo?
Bado ukistaafu mafao zaidi ya mil100
 
Mshahara wa 479000 Kwa certificate anaeanza ni kidogo? Bado diploma ni zaid ya 600000 degree kuanzia 770000 Bado mnasema ni kidogo?
Bado ukistaafu mafao zaidi ya mil100
We ni Mwanasiasa,, ?? Mtumishi au Mkulima ??

TGTS B 479000

TGTS C 636,000

TGTS D 771000

Hapo hakuna extra duty, overtime, perdiem,, on transit,,, Wala posho.

Hiyo pesa ule, uvae, ujitibu, ulipe Kodi, usaidie ndugu na usomeshe !!???

Acha utani ndugu hiyo hela kuna watu ndio posho yao ya siku moja tuu...

WANAOFANYA KAZI YA UALIMU NI MASKINI WASIO NA MITAJI AU WATU WA KUWABEBA FULL STOP [emoji611][emoji611][emoji611]..

UALIMU sio kazi ya kujivunia ni vile tu watu hawana namna.
 
Kazi ya ualimu ni wito. Patakuja kutokea kiongozi mmoja ambaye atasababisha kila mtu kuipenda kazi ya ualimu kwa malipo mazuri na mazingira mazuri ya kufanyia kazi.

tuombe Mungu na wote wanaodharau kazi ya ualimu ni watu wasiokuwa na shukurani kwani nikikumbuka nilivyokuwa sijui kusoma na sasa najua kusoma nawashukuru walimu wote walionifundisha na kunifanya niwe hapa nilipo.
 
Wasanii si wapo

Watawaafundisha tu

Ova
 
Shida sio kazi bali maslahi na mazingira ya kazi yenyewe.

Huwezi kukuta watoto wa viongozi au Wana siasa kwenye kazi ya UALIMU ndio ujue sio kazi ya kufanya.

Kazi nzuri ni ile yenye maslahi Bora na mazingira mazuri ya kazi. UALIMU unakosa hayo yote mawili.

Kwa nini wito uwe kwa maskini tu na wakulima waliokosa ada za kada zingine.
 
Kama ni kazi ngumu iache. Mimi nilishawahi kuwa mwalimu kwa mwaka mmoja kupitia crash program enzi za Kikwete. Niliacha sababu kuu ikiwa kwenda kujiongezea elimu zaidi na pia niliona sina wito nayo. Nilikuwa sieleweki kabisa kwa wanafunzi. Nikiingia class mimi mwenyewe ndo nilikuwa naelewa. Nikaona niache nikasome.

Kuhusu kwamba unatakiwa ujisomee sana ni kweli na inaweza kukusumbua tu mwanzoni lakini baada ya muda mfupi unakuwa fit. Na hii ya kujisomea ni rahisi zaidi kama ulienda kuwa mwalimu ukiwa ulifanya vizuri kwenye masomo unayofundisha na sio umeenda ualimu kisa ulifeli na kutopata admission ya kitu unachopenda chuo.

Mshahara kweli ni mdogo ila ukiwa na akili plus nidhamu ya fedha unachomoka tu kirahisi na wewe kuwa mwalimu tajiri. Tatizo ni kuwa waalimu wengi wanatoka familia duni kwahiyo kuanzia ule mshahara wa kwanza lazima agawie familia yake. Changamoto ya waalimu wengi ni roho ya unyonge waliyo nayo. Wengi wana ndoto ndogondogo.
 
Ndio. Upo sahihi. Hao maskini ndio wapo tele kwenye kada ya Ualimu ikifuatiwa na majeshi yetu yote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…