Uchaguzi 2020 Mr. Much know na Kachero waamsha wenge upinzani: Vurugu zimeanza tayari

Uchaguzi 2020 Mr. Much know na Kachero waamsha wenge upinzani: Vurugu zimeanza tayari

Moja , mbili , tatu paaa kimbiaaaa,aliyezaliwa mbali na ardhi ya nusu jangwa ndiye mshindi
 
Uasi uliopo ndani ya ccm ni mkubwa kuliko tunavyoaminishwa...!!
Hadi imfikie hatua mgombea anamlilia marehemu...
CCM ukileta uasi unaletewa nyasi. Nadhani wote tunajua jinsi nyasi zilivyo "good conductor" wa moto. Kuungua, utaungua tuu
 
Hadi nione watu wanadeki barabara ndio nitaamini kuwa anakubalika chamani
 
Mr No everything mwache apambane na hali yake ila kumbuka wasumbawanga wakija hapa watakupiga juju, spinach tembele na nsasa tunapeleka ulaya mambo si mabaya.
 
Mr No everything mwache apambane na hali yake ila kumbuka wasumbawanga wakija hapa watakupiga juju, spinach tembele na nsasa tunapeleka ulaya mambo si mabaya.
Aisee umesema. Au Nikimbilie gamboshi kujikinga nini?
 
Wanabodi,

Tujiandae kusikia chochote kutoka kwenye viunga vya siasa za Upinzani. Bundi ametua kwenye mti wa mzambarau halafu akaruka na kwenda kutua mti wa msumbawanga (taja kabila).

Kule kwenye mti wa mzambarau, kachero hashikiki hatamaniki. Unaambiwa amevimba Kama koboko. Kasema Kama mbwai na iwe mbwai yeye ndie mpeperusha fulagi. Nyepesi anahahasa kutaka suluhu ila kachero hataki kusikia ukizingatia keshaingiza pensheni yake huko kununua mbolea na viatilifu vingine vya kuukuza mti wa mzambarau.

Kule kwenye mti wa msumbawanga, unaambiwa Mr. Know Ol hafuati maelekezo Wala utaratibu. Amesema yeye ni alwatan almaarufu. Yeye ndio kajiweka juu ya kila kitu na ndio maana inasemekana cheamani na KM wamesusa kimtindo. Mr No Everithingi anaonekana kuwa mzoefu wa mapambano ya kipontio Pilato ila n mwepesi mithili ya unyoya wa kuku yanapokuja masuala ya kikaisari. Cheamani alisikika akisema "mwaka huu Kama nitapata wabunge 20 itakuwa muujiza".

Haya jogoo ameshawika, upande wa pili wazee wa mchicha, matembele, sukumawiki na spinachi nasikia mambo yao kwatu. Wanateleza Kama wako kwenye mgongo wa ngisi. Sasa hivi wamekodisha mwewe wanampanda na amewaongezea umaarufu.

Tusubiri
[emoji23][emoji23][emoji23]huu uandishi ni burudani
 
muda si mrefu watu wanagawana mbao pale mzambarauni!! 🤣
Kachero amechachamaa anasema hawezi kupandishwa presha, kishuga na kiwedingi kwa wakati mmoja. Amesema yeye atachanja mbuga na kimbunga kumba kumba
 
Back
Top Bottom