Uchaguzi 2020 Mr. Much know na Kachero waamsha wenge upinzani: Vurugu zimeanza tayari

Uchaguzi 2020 Mr. Much know na Kachero waamsha wenge upinzani: Vurugu zimeanza tayari

Presha presha, vishuga vya kubipi, viwedingi vya hapa na pale pamoja na vipandauso ni miongoni mwa maradhi hatari yanayoweza kumshambulia mwanamume mtu mzima Kama atasukwasukwa na kiyumbushwa na siasa za maji taka za watoto wadogo. Usituumizie wazee wetu, wanelotumikia hili taifa, ebooooo.

Hasira, visasi, miropoko na kauli chafu zinazoonesha kukosa mafuta ya matumaini, mpauko wa moyo pamoja na harara za Kisiasa ni miongoni mwa pancha za Kisiasa ambazo zinaweza kumpata mwanamume wa makamo mjuaji ambaye hasikilizi viongozi wake wa kisiasa.
 
Baadhi ya binadamu wa JF wabaya sana....!Nikikumbuka namna hao binadamu walivyokuwa wana'mpaka mafuta kwa mgongo wa chupa' ndugu Membe hapa jukwaani yaani hata siamini ninachokisoma hapa jukwaani. Wengine, walibadiri hadi Avatars zao hapa JF na kuweka avatar za picha za ndugu B. 'Camillus', huku wakikoleza na hash-tags za #Twende na 'Jamaa' 2020. Hizo avatar sioni hata moja!

Mshana Jr , Mkuu, upo?

Kwa heshima kubwa naomba utoe tathmini ni nini kimetokea juu ya Mtanzania mwenzetu Ndugu Benard kisiasa.

Muda ukikutosha tufafanulie zaidi juu ya huyu ndugu yetu amekwama wapi; wakati juzi kati tuliambiwa anaadaa baraza la mawaziri.

Karibu
Kazi na Bata.

😂😂😂😂😂😂
 
Ukweli ni kwamba Membe hata akigoma kumwunga mkono Lissu hao wanachama wa ACT wanapigia kura mgombea wa urais chadema .Kwahiyo Membe awaunge mkono chadema au asiwaunge haisaidii ,zamu hii hawa viongozi wanaohama vyama hamna anayewaamini kama walivyofanya lowasa na sumaye .


ACT inahitaji chadema lakini chadema haihitaji ACT huku bara
 
Ati alijifanya kwenda kuchukua mpunga ili arudi kwa kishindo matokeo yake amenyong'onyea. Imekula kwake.
 
Wanabodi,

Tujiandae kusikia chochote kutoka kwenye viunga vya siasa za Upinzani. Bundi ametua kwenye mti wa mzambarau halafu akaruka na kwenda kutua mti wa msumbawanga (taja kabila)...
Kaa Kigamboni huko, utuambie alienda kumuambia nini Pengo maana wote wale wale tu. Haya mengine acha wafu wazikane
 
Kaa Kigamboni huko, utuambie alienda kumuambia nini Pengo maana wote wale wale tu. Haya mengine acha wafu wazikane
Hawezi kunieleza. Mi ni salamu tuu halafu huyoo naelekea mikadi na malaika kuogelea
 
Back
Top Bottom