Mradi wa Bagamoyo: Hujuma Tanzania na ushindi kwa Kenya na Rwanda

Kama Port ya Dar inapanuliwa kwa kutumia Gharama ya 500mil USD na feasibility zinaonesha kuwa bado inaweza kuongezeka acha iongezwe huku ikiendelea ku buy time kwa ajili ya a better deal la bagamoyo port...sijui kwa nini mkuu alisitisha huu mradi ..ila bado deal linaweza kufanyika hata kama kenya wametangulia na Lamu ..kumbuka berth 3 za kwanza za Lamu zinajengwa na serikali ya kenya na ndo kwanza berth moja imekamika .Bagamoyo ilikuwa ijengewe na wachina na waarabu

Project ya Kupanua Bandari Ya Dar yenye berth 13 mpka sasa...itaifanya Dar port kuwa na capacity ya 28million tonnes by 2025(i think) na bado feasibility study zinaonesha kunaweza kunengwa Berth mpya Mbili au Tatu zenye Quay length ya 1.2km yan 400m per berth ambayo ndo urefu wa meli kubwa duniani kwa sasa..hii inamanisha kwa miaka hata 15 ijayo Dar port inaweza kufanya kazi vizuri kama itapanuliwa na kuwa na cranes za kutosha..

Mtwara port ina Berth mbili kwa sasa zenye urefu wa mita kama 400 jumla..ila wanajenga Berth mpya hivi sasa na kazi inaendelea ..Bei yake ni 285mil usd na urefu wa mita 350 ..hii inaamnisha meli karibia zote duniani zinaweza tia nanga...kwahyo hii ni project muhimu itayosaidia southern zones

Na Tanga port zabuni zimetangazwa ila sijajua specific zake...

So.mimi naona kwa upanuzi unaofanyika bado muda upo...na kama negotiation nzuri zinaweza fanyika kwa maslahi mazur..kwanini tu rush Bagamoyo port...wengi hatujui mkataba ulivyo ila ni serikali gani itakaa kodi ..au hata % flan flan ..
 
Hahaha mkuu una stress sana na Magu

Magu watu hawana tatizo nae sana bali wana tatizo na washauri wake akina Bashite kumshauri awanyanyase wapinzani kwa kuwabambikia kesi, kuwapiga risasi kuwapora ushindi kwenye chaguzi mbalimbali, hii ndiyo kero namba One kero zingine watu wanazivumilia sana
 
Sio tu kutumia, Ethiopia ina hisa kwenye bandari za Djibouti


Bro hawa jamaa wa jukwaa hili (wengi wao) wanapenda kuongea bila ushahidi, wanaongea kwa hisia zaidi. Ukiweza kuongea sana kwa maneno meengi, basi wewe unakuwa ndiye unayejua.
 
Wako mbele kwa kila kitu yaani hadi ufisadi
 
THANK YOU SIR, yaani lapsset ni white elephant project , Ethiopia ndio ilikuwa inalegwa, lakini ethiopia ikapata kiongozi mpya , huyu kiongozi akafanya urafiki urundi kati ya Ethiopia na Eriteria, sasa Ethiopia iko na nafasi ya kutumia bandari ya Massawa hapo Eriteria, na pia Djibouti, na pia hapo somaliland ethiopia imewekeza katika bandari ya bebera port, so Ethiopia will never use lapsset, shinda ya bagamoyo ni conditions zile china inapatia tz, ambazo hatuwezi kaaa taifa kuruhusu
 

Hayo mawazo yako kaa nayo mwenyewe kwani watanzania siyo wajinga kama wewe wanajua mkataba ni majadiliano na kila upande unakuja na mapendekezo yake na si lazima kukubali pendekezo lao na Tanzania si inayo mitizamo yake walipaswa kukaa mezani wajadiliane siyo kupoteza bilion 56 kuwalipa wananchi fidia kisha zinapotea bure kisa Kenya wamemteka Akili mtukufu magufuli, Usawa huu wananchi wanataka kujua hatima yao kwani wengi walihama yale maeneo na wengi wakaacha kuyaendeleza kwa kuishi kwa wasiwasi wakiwa hawajui chochote juu ya Bandari mpya, Tambueni kuwa nyakati hizi siyo za kuwahadaa watu ni vyema kuwambia ukweli.
 
Kuna Meli gani kubwa duniani kwa sasa ambayo haziwezi kutia nanga kwenye bandari ya Dar?
Sikiliza hiyo video, kina cha bandari ya Dar Ni kikubwa zaidi na kinao uwezo wa kuhudumia meli ya ukubwa wowote duniani
Nyingine hii hapa

 
Zitto nilitaka nikwambie kuwa wewe ni m,s.e.n,g.e lakini nimekumbuka kuwa wana Jf hatutumii lugha chafu.
Usikute wewe ndiyo wale waliolipwa bilion 56 fidia kuhama Bagamoyo kupisha Bandari ndiyo maana una uchungu na Zitto kisa hutaki kuhama na umeuza baadhi ya maeneo yako kwa watu wengine wasiojua ujio wa Bandari.
 
Wako mbele kwa kila kitu yaani hadi ufisadi
Soma vizuri mkuu, kuna maeneo nimekutajia amabayo kenya ipo mbele ya nchi zote za EA.
labda kwa faida yako Kenya ipo mbele katika maeneo yafuatayo:-

kwanza, Mentally,(ina watu ambao ni very smart upstairs),

Pili, Politically( Kenya inathamini sana democrasia kuliko nchi yoyote EA mfano kumbuka kipindi cha uchaguzi wa kenya),

Tatu, economically( uchumi wa kenya ni mkubwa sana kuliko nchi zingine za EA).

Nne, Socially( Kuna huduma nzuri hospitalini na kuna experts wa kutosha mfano ishu na tatizo la ommy dimpoz hospitali iliyogundua tatizo lake ipo nchini Kenya wakati nchini kwake alisema ana cancer wakati siyo kweli, TL alitibiwa nchini kenya kabla ya kwenda Beligium, n. k.)
 
Post ya 2010 lkn alionya vema pengine maoni yake yamezingatiwa
 
Yaani mnamchukulia poa sana Magufuli. Haya na zawadi ya tausi tumewapa
 


Wanasiasa wetu wabinafsi sana hawaangalii vitu beyond their life time. Wamejawa na ubinafsi mwanzo mwisho.
 
Una chuki na Magufuli. Fuatilia harakati za mkinga na ufafanuzi wa mkurugenzi TPA, kisha njoo
 
Nimefika eneo la tukio.
Nasema nimefika.
 
Mkuu nadhani na ww hujamuelewa zitto..... Anachosema hapa Kulikua na competition kati ya TZ na Kenya hivyo kama Bandari ya bagamoyo ingekuwa developed wakati huu tungeliwahi soko la melo kubwa kabla ya Kenya.
Shida anayosema hapa ni kwamba Kenya wamegeuka monopoly hivyo bandari ya TZ itamalizwa nguvu hata bila ya "unyonyaji" wa bagamoyo.

Kwa kusummarise tu anadai Bandari ya bagamoyo hta kama sio viable kwetu ni "better than nothing". Mara 10 hayo mabilioni yaishie bagamoyo tunaponyonywa kuliko yaishie Lamu tukose vyote.

Kingine faida ya bandari haipimwi kwa kodi na mapato ya moja kwa moja ila kuna multiplier effect zinazokuja mfano ajira,tender, makampuni mfano ya logistics,Yard za bandari,warehousing, Tax consultants, taasisi za fedha, real estates, Clearing & forwarding n.k kuweka kambi hapa nchini ambayo yatalipa kodi pia n.k hivyo hta kama tusipopata mapato mwanzoni spillover effect yake inaweza kuwa kubwa kuliko hata mapato ya TPA kwa Dar es salaam.

Ni hayo tu
 
Nina wasi wasi mkubwa Na Zitto kuhusu Bandari ya Bagamoyo! Inaelekea alikuwa Ni Wakala wa kusaidia kuwapumbaza watanzania ili wasione uuzwaji wa nchi kupitia mkataba wa Hivyo wa Bandari ya Bagamoyo Na Inaelekea alikuwa ameahidiwa donge nono! Inamuuma Sana!!!

Hivi Zitto anaamua kufumbia macho masharti magumu yaliyokuwepo kwenye mkataba unadhani Ni bure? Hivi Zitto mshipa wako wa Aibu umeupotezea wapi? Unajidhalilisha!!! Hatukuamini tena!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…