Mradi wa Bagamoyo: Hujuma Tanzania na ushindi kwa Kenya na Rwanda

Mradi wa Bagamoyo: Hujuma Tanzania na ushindi kwa Kenya na Rwanda

Kama Port ya Dar inapanuliwa kwa kutumia Gharama ya 500mil USD na feasibility zinaonesha kuwa bado inaweza kuongezeka acha iongezwe huku ikiendelea ku buy time kwa ajili ya a better deal la bagamoyo port...sijui kwa nini mkuu alisitisha huu mradi ..ila bado deal linaweza kufanyika hata kama kenya wametangulia na Lamu ..kumbuka berth 3 za kwanza za Lamu zinajengwa na serikali ya kenya na ndo kwanza berth moja imekamika .Bagamoyo ilikuwa ijengewe na wachina na waarabu

Project ya Kupanua Bandari Ya Dar yenye berth 13 mpka sasa...itaifanya Dar port kuwa na capacity ya 28million tonnes by 2025(i think) na bado feasibility study zinaonesha kunaweza kunengwa Berth mpya Mbili au Tatu zenye Quay length ya 1.2km yan 400m per berth ambayo ndo urefu wa meli kubwa duniani kwa sasa..hii inamanisha kwa miaka hata 15 ijayo Dar port inaweza kufanya kazi vizuri kama itapanuliwa na kuwa na cranes za kutosha..

Mtwara port ina Berth mbili kwa sasa zenye urefu wa mita kama 400 jumla..ila wanajenga Berth mpya hivi sasa na kazi inaendelea ..Bei yake ni 285mil usd na urefu wa mita 350 ..hii inaamnisha meli karibia zote duniani zinaweza tia nanga...kwahyo hii ni project muhimu itayosaidia southern zones

Na Tanga port zabuni zimetangazwa ila sijajua specific zake...

So.mimi naona kwa upanuzi unaofanyika bado muda upo...na kama negotiation nzuri zinaweza fanyika kwa maslahi mazur..kwanini tu rush Bagamoyo port...wengi hatujui mkataba ulivyo ila ni serikali gani itakaa kodi ..au hata % flan flan ..
 
Hahaha mkuu una stress sana na Magu

Magu watu hawana tatizo nae sana bali wana tatizo na washauri wake akina Bashite kumshauri awanyanyase wapinzani kwa kuwabambikia kesi, kuwapiga risasi kuwapora ushindi kwenye chaguzi mbalimbali, hii ndiyo kero namba One kero zingine watu wanazivumilia sana
 
Sio tu kutumia, Ethiopia ina hisa kwenye bandari za Djibouti



Bro hawa jamaa wa jukwaa hili (wengi wao) wanapenda kuongea bila ushahidi, wanaongea kwa hisia zaidi. Ukiweza kuongea sana kwa maneno meengi, basi wewe unakuwa ndiye unayejua.
 
MH. ZITO KABWE, hongera sana kwa ufafanuzi wako japo usiwe na wivu kwa sababu Kenya inazidi kutusua kiuchumi kwa kuanzisha miradi mikubwa yenye tija kwa wananchi na taifa kwa ujumla.

Kuna siku nilisema kwamba Kenya ni nchi yenye rasilimali chache ila inaoongozwa na watu wenye akili kubwa sana. Natumai kupitia huu uzi wako umewathibitishia watanzania kwamba Kenya iko mbele ya Tanzania kwa kila kitu i.e mentally, economically, politically and socially.
Wako mbele kwa kila kitu yaani hadi ufisadi
 
Kwanza hiyo bandari ni white elephant, waliijenga ili kuhudumia shehena ya Ethiopia na Sudan ndio maana mradi unaitwa lapsset lakini cha kushangaza Ethiopia imejenga railway to Djibouti

Wangefaidi kama kipindi kile Ethiopia ilivyokua haina mahusiano mazuri na Djibouti lakini baada ya kusameeana na kuungana mpaka Rais wa Ethiopia kapewa nobel maana yake hiyo Lamu haitapata hata container moja la Ethiopia

Bandari Ya Mombasa ni kubwa na haijatumika yote kiasi cha kuhitaji bandari nyingine ya ziada
THANK YOU SIR, yaani lapsset ni white elephant project , Ethiopia ndio ilikuwa inalegwa, lakini ethiopia ikapata kiongozi mpya , huyu kiongozi akafanya urafiki urundi kati ya Ethiopia na Eriteria, sasa Ethiopia iko na nafasi ya kutumia bandari ya Massawa hapo Eriteria, na pia Djibouti, na pia hapo somaliland ethiopia imewekeza katika bandari ya bebera port, so Ethiopia will never use lapsset, shinda ya bagamoyo ni conditions zile china inapatia tz, ambazo hatuwezi kaaa taifa kuruhusu
 
Dah hapa ndo naamini watanzania tuna minyoo kichwani.

1. Hivi wachina wajenge afu wasilipe kodi hata cent lakini wawe huru kufanya biashara.
2. Wakae kwenye ardhi yetu miaka 99
3. Haturuhusiwi kuendeleza bandari yeyote zilizopo
4. Wasimamie wao for the whole period kweli. Ndugu zangu hawa hawa


Wanapinga miradi kama
1. Stiglers gorge
2. Reli
3. Ndege
I ambayo hii unakwenda kwa mwananchi wa kawaida moja kwa moja.
Sijui watanzania tunataka nini


Sisi hatukuwa tayari kupata uhuru au tunatakiwa kutawaliwa kidikteta for while hadi hadi tupate akili

Hayo mawazo yako kaa nayo mwenyewe kwani watanzania siyo wajinga kama wewe wanajua mkataba ni majadiliano na kila upande unakuja na mapendekezo yake na si lazima kukubali pendekezo lao na Tanzania si inayo mitizamo yake walipaswa kukaa mezani wajadiliane siyo kupoteza bilion 56 kuwalipa wananchi fidia kisha zinapotea bure kisa Kenya wamemteka Akili mtukufu magufuli, Usawa huu wananchi wanataka kujua hatima yao kwani wengi walihama yale maeneo na wengi wakaacha kuyaendeleza kwa kuishi kwa wasiwasi wakiwa hawajui chochote juu ya Bandari mpya, Tambueni kuwa nyakati hizi siyo za kuwahadaa watu ni vyema kuwambia ukweli.
 
Kuna Meli gani kubwa duniani kwa sasa ambayo haziwezi kutia nanga kwenye bandari ya Dar?

Sikiliza hiyo video, kina cha bandari ya Dar Ni kikubwa zaidi na kinao uwezo wa kuhudumia meli ya ukubwa wowote duniani
Nyingine hii hapa

 
Zitto nilitaka nikwambie kuwa wewe ni m,s.e.n,g.e lakini nimekumbuka kuwa wana Jf hatutumii lugha chafu.
Usikute wewe ndiyo wale waliolipwa bilion 56 fidia kuhama Bagamoyo kupisha Bandari ndiyo maana una uchungu na Zitto kisa hutaki kuhama na umeuza baadhi ya maeneo yako kwa watu wengine wasiojua ujio wa Bandari.
 
Wako mbele kwa kila kitu yaani hadi ufisadi
Soma vizuri mkuu, kuna maeneo nimekutajia amabayo kenya ipo mbele ya nchi zote za EA.
labda kwa faida yako Kenya ipo mbele katika maeneo yafuatayo:-

kwanza, Mentally,(ina watu ambao ni very smart upstairs),

Pili, Politically( Kenya inathamini sana democrasia kuliko nchi yoyote EA mfano kumbuka kipindi cha uchaguzi wa kenya),

Tatu, economically( uchumi wa kenya ni mkubwa sana kuliko nchi zingine za EA).

Nne, Socially( Kuna huduma nzuri hospitalini na kuna experts wa kutosha mfano ishu na tatizo la ommy dimpoz hospitali iliyogundua tatizo lake ipo nchini Kenya wakati nchini kwake alisema ana cancer wakati siyo kweli, TL alitibiwa nchini kenya kabla ya kwenda Beligium, n. k.)
 

Wasome wakenya wenye akili wanavyouona huo ni mradi wa kipumbavu kuwahi kutokea Kenya, mimi Siwezi kushabikia huyu zumbukuku anaetaka tuuze nchi yetu kisa kushindana na Kenya, huyu hafai kabisa kuwa kiongozi sababu atafanya maamuzi kimihemko badala ya kutumia weledi
Post ya 2010 lkn alionya vema pengine maoni yake yamezingatiwa
 
Nilichoelewa ni Kwamba Odinga amechangia kukwamisha mradi wa bandari ya Bagamoyo.

Kwamba zile tripu Za Odinga Dar na Chato alikuwa anatumwa na nchi yake kumlisha sumu Rais wetu kuhusu mradi wa Bagamoyo.

Kama kweli Odinga alipewa na tuzo kwa kazi hiyo, kama nchi inabidi tujitathimini.

Kifupi Odinga alikuwa jasusi wa kiuchumi kwa nchi yake kwa mjibu wa Zitto.
Yaani mnamchukulia poa sana Magufuli. Haya na zawadi ya tausi tumewapa
 
Kibandari hicho cha Dar es salaam kilichojengwa na mkoloni eti ndo kitufanye tusijenge libandari likubwa la kuwezesha mimeli mikubwa mikubwa kushusha mzigo!- Jiwe na serikali yake wana vision fupi kwelikweli

Siku hizi kuna mimeli inabeba mafuta tani Milioni 4, Hii bandari ya Dar inaweza kuhudumia dude kama hilo?

Siku nchi ikiwa vitani na ikawa inahitaji mafuta ya kutosha kwa ajili ya mavyombo ya kijeshi huko msitari wa mbele na mengine kutumika nchini, tuna uwezo wa kuagiza mimeli mikubwa ikaweza kutia nanga kwenye kibandari cha Dar?

Population ya nchi yetu inazidi kuongezeka , leo tuko watu milion 50,miaka 99 ijayo tunaweza kuwa watu milion 200, sasa kama hatuna vision ya kuwa na Libandari lenye kuweza kubeba ma Super Tankers itakuwaje?.

Ukitaka kula lazima uliwe, Miaka 99 kwa nchi ni kitu gani?, Hongkong si hiyo hapo walipewa waingereza waiendeshe miaka 100,mbona imerudi kwa wachina, na wachina wakaamua waiongezee miaka mingine 50 ijiendeshee mambo ya ndani, sasa miaka 50 si inaisha keshokutwa tu?

Mambo ya nchi yanahitaji long vision, siyo sifa sifa tu
Sasa Bandari ya LAMU hiyo hapo, na inajengwa na wachina hao hao, sisi tumembwelambwela.

Hiyo SGR tunayojenga kama haitakuwa na mzigo mkubwa wa kutosha wa kubeba itakuwa Underutilized!

Kwa taarifa zenu, Mchina anataka kufungua front ya kibaishara na Afrika, Alitaka Tanzania iwe gateway ya kuingilia kwa sababu ya historia nzuri na uhusiano wetu mzuri na wao na pia kwa sababu wana reli ya TAZARA waliyotusaidia kujenga miaka 50 iliyopita. Sasa kwa kuwa sisi tunajivutavuta watakwenda kuangusha kitu cha maana hapo LAMU, Then Kenya wataiongezea urefu SGR yao ifike Uganda na South Sudan, Ikshafika Uganda naamina Kagame atataka link ya SGR ya Uganda pia iende kwake na wakati huohuo atakuwa na Link ya SGR kutoka Tanzania.

Kagame akifanikiwa kuwa na SGR mbili moja kutoka Kenya na nyingine kutoka Tanzania atakuwa na leverage kubwa mno katika east Afrika, kwa sababu akikosana na nchi moja atatishia kupitishia mzigo wake nchi nyingine, kwa hiyo atakuwa na bargaining chip kubwa ndani ya East Africa.

Mradi wa Bagamoyo ulikuwa unaandamana na viwanda kibao kwenye Economic Zone hiyo, sasa hivyo vitu vimeyeyuka!


Wanasiasa wetu wabinafsi sana hawaangalii vitu beyond their life time. Wamejawa na ubinafsi mwanzo mwisho.
 
Una chuki na Magufuli. Fuatilia harakati za mkinga na ufafanuzi wa mkurugenzi TPA, kisha njoo
Moja ya mambo ambayo nimeandika hadi vidole vimegoma kuandika ni suala la bandari!!! Na eneo ambalo Magufuli nimeamini ni muongo wa kupindukia ni suala la Bandari ya Bagamoyo!!

Eti serikali haitapata chochote na mazuzu wanamshangilia!!!

Eti hata kodi hatutakusanya wakati duniani kote inafahamika kodi ni mali ya serikali!!!

Na kama alivyosema Zitto, hoja ya ardhi ni hoja ya kijinga!! Sheria ya ardhi inatamka wazi kwamba hati miliki inaweza kutolewa kwa miaka 33, au miaka 66 au 99!!!

Sasa mradi mkubwa kama wa bandari na economic zone hau-qualify hatimiliki ya miaka 99, ni mradi gani tena unaoweza ku-qualify?! Kama mradi mkubwa kama Bandari ya Bagamoyo stahili yake ni miaka 33, ni miradi ya aina gani tena itakayokuwa na sifa ya kuwa na hati miliki ya angalau miaka 66?!!

Ukweli ni kwamba, Magufuli anapenda sifa... angependa sana aonekane yeye ndie mwanzilishi wa ule mradi! Na hicho ndicho kinachomfanya akimbilie miradi mingi mikubwa ili apate hiyo status kwamba kama isingekuwa Magu, basi xyz usingekuwepo kama ambavyo amekuwa akitamba kwamba kama sisi yeye, ATCL isingekuwa na ndege!!!
 
Moja ya mambo ambayo nimeandika hadi vidole vimegoma kuandika ni suala la bandari!!! Na eneo ambalo Magufuli nimeamini ni muongo wa kupindukia ni suala la Bandari ya Bagamoyo!!

Eti serikali haitapata chochote na mazuzu wanamshangilia!!!

Eti hata kodi hatutakusanya wakati duniani kote inafahamika kodi ni mali ya serikali!!!

Na kama alivyosema Zitto, hoja ya ardhi ni hoja ya kijinga!! Sheria ya ardhi inatamka wazi kwamba hati miliki inaweza kutolewa kwa miaka 33, au miaka 66 au 99!!!

Sasa mradi mkubwa kama wa bandari na economic zone hau-qualify hatimiliki ya miaka 99, ni mradi gani tena unaoweza ku-qualify?! Kama mradi mkubwa kama Bandari ya Bagamoyo stahili yake ni miaka 33, ni miradi ya aina gani tena itakayokuwa na sifa ya kuwa na hati miliki ya angalau miaka 66?!!

Ukweli ni kwamba, Magufuli anapenda sifa... angependa sana aonekane yeye ndie mwanzilishi wa ule mradi! Na hicho ndicho kinachomfanya akimbilie miradi mingi mikubwa ili apate hiyo status kwamba kama isingekuwa Magu, basi xyz usingekuwepo kama ambavyo amekuwa akitamba kwamba kama sisi yeye, ATCL isingekuwa na ndege!!!
Nimefika eneo la tukio.
Nasema nimefika.
 
Nimesoma bandiko lako Zitto, lakini umeshindwa kumuelewa Rais Magufuli.

Ni kwamba Mh Magufuli hajakataa maradi wa bandari ya Bagamoyo. Alichokikataa Magufuli ni mkataba haujakaa kwa maslahi ya watanzania. Umekaa kwa maslahi ya wanaoujenga. Kitu ambacho hata sisi watanzania tunamuunga mkono kama mkataba umekaa kiunyonyaji hauna maslahi kwetu kuna haja gani kuendelea nao?

Mradi gani huo ambao serikali haitapata kodi, mradi gani huo ambao kama nchi haturuhusiwi kuendeleza au kujenga bandari nyingine yoyote kwa karne nzima hivi tumelogwa au?

Hapana tuendeleze tu bandari yetu ya Dar, Tanga na nyinginezo taratibu kwa maslahi yetu, badala ya kuwa na miradi feki isiyo na tija kwa nchi.

Huu ni ukoloni kama ukoloni mwingine tu, kama tutauza nchi kirahisi hivi. Kwa hili tumuunge mkono Rais Magufuli kwa maslahi ya nchi yetu. Huu ukoloni mamboleo tuukatae, chochote ambacho hakina maslahi kwetu tukatae.., hivyo hivyo watatuelewa tu.

Mambo ya kuuza rasilimali zetu tunajikuta tu watumwa hapana, hatutaki ya Zambia hapa..

Zitto kwa hii hoja yako itakushushia heshima na malengo yako ya mbeleni. Washauri wenye huo mradi uwe kwa maslahi ya wote. Kama haipo win win hiyo siyo biashara tena ni unyonyaji.
Mkuu nadhani na ww hujamuelewa zitto..... Anachosema hapa Kulikua na competition kati ya TZ na Kenya hivyo kama Bandari ya bagamoyo ingekuwa developed wakati huu tungeliwahi soko la melo kubwa kabla ya Kenya.
Shida anayosema hapa ni kwamba Kenya wamegeuka monopoly hivyo bandari ya TZ itamalizwa nguvu hata bila ya "unyonyaji" wa bagamoyo.

Kwa kusummarise tu anadai Bandari ya bagamoyo hta kama sio viable kwetu ni "better than nothing". Mara 10 hayo mabilioni yaishie bagamoyo tunaponyonywa kuliko yaishie Lamu tukose vyote.

Kingine faida ya bandari haipimwi kwa kodi na mapato ya moja kwa moja ila kuna multiplier effect zinazokuja mfano ajira,tender, makampuni mfano ya logistics,Yard za bandari,warehousing, Tax consultants, taasisi za fedha, real estates, Clearing & forwarding n.k kuweka kambi hapa nchini ambayo yatalipa kodi pia n.k hivyo hta kama tusipopata mapato mwanzoni spillover effect yake inaweza kuwa kubwa kuliko hata mapato ya TPA kwa Dar es salaam.

Ni hayo tu
 
Nina wasi wasi mkubwa Na Zitto kuhusu Bandari ya Bagamoyo! Inaelekea alikuwa Ni Wakala wa kusaidia kuwapumbaza watanzania ili wasione uuzwaji wa nchi kupitia mkataba wa Hivyo wa Bandari ya Bagamoyo Na Inaelekea alikuwa ameahidiwa donge nono! Inamuuma Sana!!!

Hivi Zitto anaamua kufumbia macho masharti magumu yaliyokuwepo kwenye mkataba unadhani Ni bure? Hivi Zitto mshipa wako wa Aibu umeupotezea wapi? Unajidhalilisha!!! Hatukuamini tena!
 
Back
Top Bottom