Mradi wa Bagamoyo: Hujuma Tanzania na ushindi kwa Kenya na Rwanda


Magufuli yupo na Lamu ya kenya haitaki Bandari ya Bagamoyo, kama kweli angekuwa anaitaka hiyo Bandari angeshakaa na Wachina na hao waarabu wakarekebisha mikataba na kufikia mwafaka Bandari ikaanza kujengwa
 
Watu wanajibu kishabiki badala wapinge kwa hoja ili tujue upande wa pili wa shilingi kwa kina.
Hata maandishi yake yamekaa kishabiki! Hakuna na hoja zozote za kuonyesha kuwa huo mradi utakuwa na manufaa kwa nchi yetu. Kusema tu kuwa watajenga badari kubwa siyo fact. Angeonyesha jinsi hiyo bandari itakuvyokuwa na manufaa.
 
Mheshimiwa, wewe ulikuwa mmoja wa wale walionanga serikali kuhusu makemikia na ukatoa sababu mbalimbali za kisheria na uchumi kuhusu hilo. Mwisho wa siku mmebaki midomo wazi.

Wewe endelea na ACT na ubunge wako ila hadhi yako kitaifa inautata kiasi wengine tunaanza kuamini pengine wewe siyo mwenzetu.
 
embu tuambie serikali ingepata nini? kupokea meli kubwa ni jambo moja kunafaika ni jambo lingine kabisa.. kikwete alisita kusaini, magufuli anasita. unadhani hawana akili kichwani?
 
Magufuli yupo na Lamu ya kenya haitaki Bandari ya Bagamoyo, kama kweli angekuwa anaitaka hiyo Bandari angeshakaa na Wachina na hao waarabu wakarekebisha mikataba na kufikia mwafaka Bandari ikaanza kujengwa
Kurekebisha siyo tatizo. Tatizo ni marekebisho ya aina gani yatakubalika.
 
Bungeni hata uongee vizuri namna gani maadam ni mpinzani halitafanyiwa kazi mifano ni mingi sana hv unaishi Tanzania wewe?
 
Kwani Panama na Suez canals nazo zinaupana gani kuita malango wetu uchochoro?
 
Majasusi gani? Ndo hao walio mshauri kwamba Serikali ikanunue korosho kwa kutumia Jeshi? Kama ndo hao basi tuna shida kubwa na majasusi wetu.
Mkuu, shida yetu wala siyo majasusi. shida kubwa ya Tanzania hivi sasa ni kwamba tuna Rais ambaye ana muono mfupi kuliko maelezo.
 
Kujenga kwa fedha zao nayo ni hoja? Hoja ni uendeshaji wa nchi itanufaikaje? Wanaweza kujenga kwa fedha zao tukajikuta kama tumewauzia hiyo sehemu moja kwa moja. Umenikumbusha mwanamke anayenywesha pombe Bar halafu anaamua kumeza kama rejeta mbovu akidai eti hatumii fedha yake.
 
Pale tu tutakapojifunza kufanya kazi pamoja badala ya kuweka ubinafsi mbele ndipo tutakapopata uhuru kamili wa kiuchumi. East Africa.
Tunashindana sisi kwa sisi, nguvu nyingi inapotea kwa hila na faida ya muda mfupi. Mabeberu wanafurahi na kunemeekea hapo hapo.
 
Hoja zako zitto huwa zimekaa kinafiki na kipambe Sana huwa haziangalii side effects kwa Taifa. Tatizo huko bungeni siku hizi mmekuwa mkipoteza mda mwingi kubishana ujinga na kutishiana Mambo ya uchawi kuliko kujadili vitu ambavyo vina masirahi kwa Wananchi.
Ko wewe unaona Ni halali muwekezaji kumiliki bandari kwa karne moja serikali bila kupata faida kubwa kisa aliijenga yeye.

Nina muunga mkono Rais magufuli kwa maamuzi yake Kwani Ni maamuzi yanayomuhurumia mtanzania na Wala siyo mawazo yako yanayomupa muwekezaji ulaji. Kauli Kama hii hii ya magufuli aliwahi kusema mwalimu wakati wa uhai wake lakini nyie wabungu na Rais wenu mkapa hamkumusikiliza mkapitisha sheria za ajabu ambazo mpaka leo watanzania tunajutia..
Nanukuu "Madini na rasilimali zote zilizomo nchini zisianze kutumika mpaka pale Watanzania watakapo pata uwezo wa kutumia wenyewe"(By j.k nyerere)

Likewise kukubali kusaini mkataba huo wa kinyonyaji Ni sawa na kurudia makosa yaleyale ya kusain mikataba ya Madini mliyoipitisha nyie wenyewe bungeni kwa kutumika na Mabeberu.
Viva Rais Magufuli Endelea kututea Sisi wananchi Achana na kelele za Hawa kina zitto wachumia matumbo wa mabeberu.
 
[imejaribu kukuelewa lakin kwa taabu sana, hizo sheria zilipitushwa bungeni, Maguful alikuwako, unaweza kutuletea record moja hapa ya maguful kupinga hzo sheria?

Angalau ZK twaweza kupata, leo unamlaumi ZK kuwa ndi waliopitisha sheria mbovu za madin enzi za mkapa wakt ambao huyo ZK wala hakuwepo bungeni?
 
Weka huo mkataba tuone sio kuleta propaganda eti kodi tutapangiwa na mchina
 

Tundu Lisu alianza kupiga kelele tokea 1998 mapema kabsa na Magufuli alikuwa waziri kwa nini hawakumaliza matatizo mapema? Zitto na wapinzani wamesaidia vingi kuwazindua ndipo wakaja na ya sasa ingawa na yenyewe yana makandokando yake utayasikia baadae hapo mbeleni.
 
Huwezi kuongeleea mambo makubwa kiasi hiki bila kuonyesha numerical analysis ya huo mradi kuanzia gharama za utekelezaji wa huo mradi na return yake itachukua muda gani kubreak even na pia mkataba hu upone (nani anafadika na ninik na kwa jinsi gani).

Hizo porojo za Zitto hata mimi ninaweza kuzipiga tu vizuri na nikaeleweka. Uchumi hauendi kwa porojo. Alete analyisis inayo support hiyo hoja yake vinginevyo bado naona anatafuta kick (cheap popularity). Kakaosa hoja sasa anapalamia mpaka visivyo na tija!

HIVI KWELI SERIKALINI AU TANZANIA KWA UJUMLA HAKUNA WACHUMI WAZURI MZURI NI ZITTO TU NA NDIO ANAJUA KILA KITU?
 
Kagame aliwahi kumwambie Kikwete yafuatayo:-

" I will Just Wait For You At the Right Place And I will Hit You, "

MWISHO WA KUNUKUU.


Mkuu ebu tuwekee hyo clip....kuna sehemu niliionaga (kwenye social network) ila nimesahau
 
Nimesoma mara tatu hii makala ya Zitto,bila kujali itikadi ya memaji dhidi ya Rais Magufuli.
Serikali ipitie upya mkataba, yale yenye ukakasi yawekwe sawa,Mradi uanze haraka.

Kuhusu Reli kwenda Rwanda vs Burundi,binafsi natamani HUB iwe uvinza kwakuwa uvinza bado ni Tanzania,yapo mengi watanzania watanufaika kupitia HUB ya uvinza kuliko kupeleka ajira Rwanda wakati tuna maelfu ya vijana wasio kuwa na ajira.

Hizi siasa zisitufanye kutelekeza maslahi ya taifa na watu wetu.

Zitto leo umetufungua macho wengi,tunaomba uje na makala nyingine ya mradi huo ukituonesha serikali itapata nini kwa kila mwaka ambacho kwa kutelekeza mradi huo tutakuwa tumewaachia wakenya wanufaike nacho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…