Mradi wa Bagamoyo: Hujuma Tanzania na ushindi kwa Kenya na Rwanda

Mradi wa Bagamoyo: Hujuma Tanzania na ushindi kwa Kenya na Rwanda

Hii mada sio hadhi ya wale wapambe wa vyama ,hii ni mada ya kisomi inayopaswa kujadiliwa watu wenye uelewa mkubwa katika uchumi na diplomasia ya kiuchumi.

Wasomi acheni woga, jitokezeni kudadavua hii mada kitaalamu bila kuegemea mrengo wa kiasiasa.
 
ZZK hebu acha tamaa ya 10% yako ambayo uliitegemea kutoka kwa wachina bali waonee huruma watanzania na kizazi kijacho mbona umekuwa msakatoge mpaka kupitiliza ? Watu mkataba tumeuona unataka kuaminisha watanzania kuwa sie hamnazo. Unataka tutawaliwe na wachina hivi huoni kinachoendelea Zambia na nchi zingine zilizofanyiwa mbaya na wachina .Tafadhali baba najua hapo nyuma ulikula sana sasa umebanwa vumilia tunataka maendeleo ya nchi na uache kutumika sana mbona tunakujua sana mpenda hela wewe.
 
[imejaribu kukuelewa lakin kwa taabu sana, hizo sheria zilipitushwa bungeni, Maguful alikuwako, unaweza kutuletea record moja hapa ya maguful kupinga hzo sheria?

Angalau ZK twaweza kupata, leo unamlaumi ZK kuwa ndi waliopitisha sheria mbovu za madin enzi za mkapa wakt ambao huyo ZK wala hakuwepo bungeni?
Mkuu umetumia akili gani kuandika huu ujumbe? plz jaribu kuu edit Basi ndo uutume Tena maana unatusumbua Sana kuuelewa.
Harafu ulichokiandika na mwandiko wako unasadifu akili yako uliyonayo bila shaka kwahiyo siwezi kukushangaa Zaidi ya kukuhurumia.
 
Gerald .M Magembe,


Kuhusu eneo wewe umedanganya Mmlingotini, Kiromo, Kitopeni na Zinga zingetosha sana na baadhi kungebaki ndio maana Mlingotini watu walishalipwa)
 
Hii Bandari ya Bagamoyo ingekuwa Chato ingeshajengwa siku nyingi.

Subirini muone Chato inavyojengwa bandari kubwa kushinda ile ya Mwanza
 
Bandari ijengwe na Wachina halafu waitumie kwa miaka 100 Rais Magufuli anataka miaka 33

Kafanye nyumbani kwako biashara kichaa hiyo
 
Huelewi!
Nauliza kabla ya kudandia kujenga hiyo bandari kwa nini tusiboreshe kwanza hizi zilizopo?

Mkuu kwa uelewa wangu nayafahamu haya:

Unapofufua Bandari au kuwekeza kwenye Bandari lazima uwe na sababu ya kufanya hivyo, Mkoloni alipojenga Bandari zote hizi na kujenga reli alikuwa tayari ameshajiandalia mizigo na yakusafirisha na kuleta.. Mkoloni aliwekeza sana kwenye uzarishaji hasa kilimo kwa maana ya Katani, Ngano, Kahawa, Ngozi, Matunda,Korosho nk. Kifupi mkoloni alifanya set up ya uzarishaji kwanza halafu akajiwekea uhakika wa masoko huko ughaibuni hapo ndio akalink bandari zote na reli.
Ukipitia uzarishaji alioufanya mkoloni pia alihitaji malighafi na vipuli kutoka sehemu mbalimbali za maana uzarishaji ulikuwa kwenye kiwango cha juu na mahitaji ya vipuli na baadhi ya malighafi zilihitajika.

Kwa sasa uzarishaji wetu bado ni mdogo kiasi cha kuweza kulisha bandari zote, Tanga na Eneo lote la kaskazini hakuna uzarishaji wa kuleta kontena hata 1000 kwa mwezi na hivyo hivyo uwezo wa kuexport kiasi hicho pia haupo kwa tafsiri nzuri ni kuwepo na uzarishaji wa kiwango cha chini. Kimkakati Mtwara port ipo karibu na Nacala na Beira port za Msumbiji ambazo tayari pia hutumiwa na Zambia, Malawi na DRC.. Tanga port iko Karibu na Mombasa port na jirani hapo hakuna nchi yeyote iliyo karibu unaweza kusema inaweza kutumia hiyo bandari zaidi ya kutegemea mizigo ya Ndani. Kontena 500-1000 hizo ni meli Ndogo ambazo bado zinaweza kuhudumiwa na hizo Bandari za Tanga na Mtwara, la msingi nikuongeza uzarishaji wa ndani ili tuwe na uwezo wa kusafirisha na kuagiza mizigo mingi sehemu mbalimbali za nchi na hapa ndipo tutaweza na kuwa na pakusimamia.

Ukiangalia Ujenzi wa hii Bandari ya Bagamoyo, wahusika wenyewe ndio waliichagua na si kuchaguliwa na plani yao ilikuwa ujenzi uende sambamba na chain ya viwanda vingi, ukiangalia hapa utaona waliamua hivyo ili kuwezesha bandari iwe na mizigo ya kuingia na kutoka na kama kuna mingine itakuja basi itavutwa na idadi ya meli zinazoingia na kutoka kwenye bandari maana wingi wa meli ndio huleta mizigo. Flow ya meli ikiwa kubwa mahala fulani maana yake waleta mizigo huwa wengi ili kupata uharaka wa kufikisha mizigo.
 
Freddie Matuja,

Kweli mku ZZK atupe data za kisomi sio blabla. Siku hizi tuko makini na uchambuzi wao. Yeye na TL. Wanataka kuwapa sapoti au marks bila kufanya juhudi darasani. Atwambie within 5 Years or 10 Years tungepata kiasi gani?
 
Kwakweli Zitto amewandika mazito ila tu sio mtu wakuaminika... lazima kuna kitu nyuma sio kwa maandalizi ya maandishi hayo, Zitto asingekua mnafiki angekua the best presidential material wa nchi hi, anaupeo mwingi
Jama ni mzuri lakini hayuko stable sana kimawazo. Unaweza kuta kesho anakuja na bandiko la kupinga huu mradi kwasababu ameona wengi hatujamusapoti.
 
Labda ulikuwa hufahamu tuu ila ujenzi wa sasa wa bandari ya Dar utajumuisha kuongezwa kwa kina, hivyo hizo generation 4 zitaweza kutia nanga.

Jamaa yangu hakuna namna unaweza kutanua ile Bandari ya Dar es salaam kufikia viwango vya bandari kubwa zinazozungumziwa.. Kulia Kigamboni na kushoto Posta katikati ni njia, hakuna namna unaweza kuzuia sand deposit pale na kila siku utakuwa unachimba kina tu kuongeza kina.. Kana inawezekana ibomolewe kigamboni au Posta pawe open sea na sio mlango na hii ni moja ya sababu iliyofanya wale jamaa wakaacha bandari zote wakaitaka Bagamoyo.. Bandari zote za Tanzania zina mlango wakuingilia port maji kupwa na maji kujaa huondoa maji kabisa na kujaza mchanga mara kwa mara na kwa muda fulani itakulazimu kuchimba kuongeza kina..

Lingine pale ni storage na miundo mbinu ya kuingi na kutoka bandarini hasa kwa heavy loads, ukileta heavy loads nyingi lazima kuwe na foleni kubwa sana maeneo mengi ya Dar hasa njia zinazolink na bandari, Huwa likishuka NYK pale na kuanza kushusha magari lazima uone msongomano wa hatari pale.. Storage bado ndogo sana kwa meli kubwa tatu za kontena 10000 kushusha mzigo pale hapo bado roro kubwa hazijashuka na kuanza kupakua..

Kuendelea kuijenga Dar es salaam port ni kupoteza fedha tu, ni eneo ambalo tayari sio rafiki labda tuamua DAR ES SALAAM PORT IWE NI KWA RORO TU, MTWARA PORT IWE NI KONTENA PORT, NA TANGA PORT IWE FOR TANKERS.
 
Tutaendelea sana kuumiza vichwa na hivi vitu kiasi cha kuparuana wenyewe kwa wenyewe, kuna vitu viwili bado hatujaweza kuvimaliza kama basic, msingi imara huleta nyumba imara, zege juu ya mabua ni kupoteza muda tu..

UMASIKINI; Jamaa yetu Tanzania bado masikini sana, tuikwamue kwanza na vidogo tulivyonavyo ili ikijikwamua hayo makubwa kubwa itakuwa kama kumsukuma mlevi, masikini anawaza kula, kulala, kuvaa, kujitibu, tutatue kwanza.

UZARISHAJI MALI MDOGO ; Bado shughuli za uzarishaji mali ni ndogo sana Tanzania, tunazarisha kiasi kidogo sana na mwisho wa siku uzarishaji mdogo hupelekea kushidwa kwenye mambo mengi mfano, ndege, meli, reli, bandari nk.
 
Kama swala ni kujenga bandari yenye kina kirefu kwanini tusiijenge ya Mtwara ambayo kiasili kina chake ni kikubwa pia imekaa sehemu nzuri ya kuweza kuhudumia nchi ambazo hazina bandari, kama wapinzani wenyewe ndio hawa waliomtukanaa JK anauza nchi, miswada inaletwa kwa hati ya dharula waendelee kuwa wapinzani milele wala wasipewe nafasi.

Tayari ilishafafanuliwa ni jinsi gani bandari ya Bagamoyo ingeua bandari nyingine na huku nchi ikipoteza mapato ya kodi kama tunataka kushindana na Kenya kuhusu bandri ya Lamu sehemu sahihi ingekuwa ni kujenga bandari ya Tanga na sio kwenda bagamoyo kwa kifupi Zitto anatumika kama alivyotumika kwenye maswala ya madini
 
Jiwe kawasamehe ACACIA dola bilion 190 (Trilion 424)walizotuibia kwenye madini.
yaani kwa gharama za hiyo bandari ya bagamoyo kuwa ni Dola bilion 10, maana yake Tumewasamehe ACACIA pesa yenye uwezo wa kujenga bandari kama hizo 19.

Jiwe ni mhujumu uchumi!
 
Tumepoteza fursa ya nchi kwa sababu za kitoto, zisizo na maana na za kipropaganda tu. Kuendesha bandari miaka 99 mara tunataka miaka 33 haiwezi kuwa sababu kwa mtu mwenye akili timamu wakati Mradi ni Joint Venture na Serikali ni mbia mwenye hisa zinazotokana na ardhi yake. Kuna mwekezaji atabeba ardhi ya Tanzania kuipeleka China au Oman? Eti Bagamoyo itaua Bandari ya Dar es Salaam, kwa hiyo Ujenzi wa Bandari ya Lamu utaua Bandari ya Mombasa? Nasubiri kuona Bandari ya Dar ikifa kwa sababu ya ujenzi wa Bandari ya Lamu.

*********************
Mwami tafadhali sema sababu zote alizosema Mh. Magufuli acha kuchagua vipande vinavyobeba hoja zako za kizushi.

Nakumbuka vizuri Rais alielezea sababu nyingine kwamba haitaruhusiwa kuendeleza bandari nyingine yeyote, moja na pili TRA au mamlaka za serikali hazitaruhusiwa kuingia kufanya ukaguzi ndani ya bandari.

Aidha alisema hata TRA hawataruhusiwa kukagua uhalisia bali kile walicholetewa mezani.

Naruhusu kukosolewa au nyongeza katika hili.
 
Kama swala ni kujenga bandari yenye kina kirefu kwanini tusiijenge ya Mtwara ambayo kiasili kina chake ni kikubwa pia imekaa sehemu nzuri ya kuweza kuhudumia nchi ambazo hazina bandari, kama wapinzani wenyewe ndio hawa waliomtukanaa JK anauza nchi, miswada inaletwa kwa hati ya dharula waendelee kuwa wapinzani milele wala wasipewe nafasi.
Tayari ilishafafanuliwa ni jinsi gani bandari ya Bagamoyo ingeua bandari nyingine na huku nchi ikipoteza mapato ya kodi kama tunataka kushindana na Kenya kuhusu bandri ya Lamu sehemu sahihi ingekuwa ni kujenga bandari ya Tanga na sio kwenda bagamoyo kwa kifupi Zitto anatumika kama alivyotumika kwenye maswala ya madini

Katika bandari Mtwara ni bandari au dimbwi, bandari unaijua wewe?
 
Kwa hiyo ni kweli? Bagamoyo tukabithi kwa miaka 99 bila ya sisi kupata chochote au siyo. Unapenda
Huyu Mwami kuna kipindi Mzee Dr. Harrison Mwakyembe alisema sikutegemea mtu makini Kama Zitto Kabwe anasema serikali inunue mitambo ya IPTL wakati alijua sheria ya Manunuzi PPRA inahitaka kununua vifaa, mali mpya ba si second hand.

Aidha aliongeza kwamba kununua kwa mitambo ile bado sio mwarobaini kwakua uzalishaji wa umeme wa mafuta Ni ghali na maintenance costs yake ni kubwa.

Badala ya kuipunguzia serikali mzigo itakua inauobgeza maradufu.

MH. ZITTO UNAKWAMA WAPI KAKA YANGU WEWE NI MTU SMART SANA KUJIINGIZA KWENYE SIASA UCHWARA KAMA HIZI. UNAITUMIA ELIMU YAKO VIBAYA.
 
ZZK anatueleza mkakati wa Bandari ya Bagamoyo kuwa ni gateway ya imports.

Kwa mchumi yeyote ningetegemea angekuwa na in-depth analysis ya how do we strengthen production ya mazao ghafi na processing ili kuwa na certain ya exports.

JK toka 2013 mpaka 2015 anatoka madarakani alisita kusaini a go ahead. Unadhani kwanini year 1 imepita hakusaini,
Year 2 imepita hakusaini.

Year 3 anatoka madarakani early November bila kusaini. Nini alikiona kama sio favourable clauses ya mkataba mpaka 3 years zikakatika hakutia mkono.

Dr. Mpango waziri wa Fedha alikuwa mkuu wa Tume ya Mipango wakati wa JK; bila shaka alikuwa sehemu ya walimshauro JK asiwe "fasta" kusaini.

ZZK uliponda sana initiative za JPM na Prof. Kabudi kukaa na Barick na kushikilia makanikia in the name of tutashitakiwa. Leo hii uongo wako umeonekana wazi mchana peupe.

By the way; show by numerical projections namna gani Bagamoyo port could make a difference kwenye kuongeza revenues ambapo Mtwara, Tanga na Dar zime-fail ili ku-justify hoja yako
Very learned way of sending across good ideas. Tunatanua bandari zote tulizonazo kwa wakati mmoja, ili uchumi unaotegemea bahari uweze kukua.
 
Back
Top Bottom