Eric Cartman
JF-Expert Member
- May 21, 2009
- 11,966
- 11,218
Kwenye hiyo miradi kabla ya kuwalaumu wachina tatizo ni uchoyo wa raisi aliekuwa madarakani muda huo kwa kupeleka miradi nyumbani kwao kijijini badala ya kufanya mambo kwa maslahi ya nchi.
China bila ya kujali ya kuwa watakuwa hawana uwezo wa kulipa kutokana na demand ndogo ya mizigo given the location of the port na na demand ndogo ya abiria kwenye uwanja wa ndege kutokana na kwamba sehemu yenyewe ni remote bado wakawajengea hiyo miradi.
Why so? waki default wanaendesha wao hasa bandari ambayo waliiweka kama mtego kwa strategy zao za logistic and apparently militarily wanaweza paki manowari zao in the future.
Ndio ujue hiyo port ya Bagamoyo hawafikirii sana sisi ni maslahi yao ndio swala la msingi, je sisi tunajua ina maslahi gani kwetu au ina impact gani za kiuchumi.
Wanaojua ni watu wale wale waliosaini mikataba mibovu na ndio hao hao leo walishindwa kupata better deal na ACCACIA na wanaotoa ushauri wa investment za ovyo; bila ya kuutoa huo mkataba kujadiliwa hili kupata mtazamo wa wengi. Kwa kudra za mungu hii investment inaweza kuwa blessing or a very bad one yenye manufaa kwa China tu.