Mradi wa LNG: Tukicheza Vizuri wakati huu ni hakika Umasikini tutausahau Tanzania na Samia anaweza kuwa Rais Bora zaidi kuwahi kutokea Tanzania

Hiyo gas unayojivunia life time yake wakiamua kuichimba yote ni miaka mingapi? Na je ikiisha hiyo LNG plant itabaki na kazi Gani?
 
Hiyo gas unayojivunia life time yake wakiamua kuichimba yote ni miaka mingapi? Na je ikiisha hiyo LNG plant itabaki na kazi Gani?
Miaka ya kutosha tuu na pia uvumbuzi unaendelea Hali kadhalika Nchi ya Mozambique kuna uvumbuzi kwa hiyo italetwa Tzn.
 
Kama kawaida ya wabongo mwekezani 87% tz 3% kuendelea kusikieni bombani ndugu.
 
Kama kawaida ya wabongo mwekezani 87% tz 3% kuendelea kusikieni bombani ndugu.
Ndio hivyo unataka upate kingi wakati hujatafiti na hujaweka chochote hapo kwenye mradi.

Ukiacha hiyo share ila kuna ajira,Kodi na faida zingine mtambuka.

Kumbuka til.70 hizo sio pesa ya serikali ni ya investors.
 
Unadhani tatizo la marehemu lilikuwa ni nini haswa?. Kutaka ionekane watangulizi wake kwamba hawajafanya kitu na ni madalali wa mabeberu? Ubishi tu na ukaidi?. Au kuna alichokijua ambacho sisi hatukijui?.
 
Ila wabongo dah! Kuna watu hadi bado wanamlaumu Nyerere na wengine hadi sasa bado wanamlaumu Magufuli kana kwamba bado anaongoza nchi.
 
Unadhani tatizo la marehemu lilikuwa ni nini haswa?. Kutaka ionekane watangulizi wake kwamba hawajafanya kitu na ni madalali wa mabeberu? Ubishi tu na ukaidi?. Au kuna alichokijua ambacho sisi hatukijui?.
Hoja zao zinahoja kwa upande fulani
 
Kwa iyo unapingana na wachambuzi mahiri The African Report?

Unaonekana hata Elimu yako ni mashaka, kuna uhusiano gani kati ya LNG na Umeme au Bwawa la Nyerere?

Nani kakwambia LNG inatumia pesa za serikali?
Hilo African report ni kati ya majarida yasiyoamika duniani,lipo kisiasa zaidi.Na pia hiyo LNG unayoiongelea hujui kuwa ina wamiliki wake tofauti kabisa na sirikali ?Sasa sisi tutanufaika vipi zaid ya kuingizwa mjini kwa mara nyingine na wapigaji kwa kuwajengea miundombinu?
Tatu,sie wenyewe tumeshindwa kuileta Dar kwa matumizi ya kawaida tutaweza kuipeleka ulaya?
Na mwisho epuka propaganda za west ndugu
 
Tupe uthibitisho wa kutoaminika kwa jarida la The African Report, tupe pia uthibitisho wa wamiliki wa Gesi ambao ni tofauti na Serikali
 
Ndio hivyo unataka upate kingi wakati hujatafiti na hujaweka chochote hapo kwenye mradi.

Ukiacha hiyo share ila kuna ajira,Kodi na faida zingine mtambuka.

Kumbuka til.70 hizo sio pesa ya serikali ni ya investors.
Mawazo finyu sijawahi kuona

Utafiti gani ? Nani hajui kwamba hapo kuna Gas ?
Mikataba mibovu inafanywa kutokana na kukosa uzalendo, uroho na 10% na kuwa shortsighted...

Unaongelea ajira ?, Ajira kwa vizazi vingapi ? hio ni non renewable energy siku ikiisha na ajira zinapotea..., tungekuwa na busara madini ni mengi kwenye faida ya huku tungewekeza itusaidia na kule..., Tunawaza tu kuuza kwa bei ya kutoa zawadi badala ya kuwaza pia hio natural gas angalau kuwa piped iwasaidia wananchi kuondokana na gharama za cooking fuel (now that is thinking long term)

By the way ni lazima kila maliasili ichimbwe na imalizike kwenye hiki kizazi chetu (and what can we show for it) ? Ni kama mlevi kutumia kiinua mgongo chake kununua bling bling
 
Wewe ni mpumbavu,uliamka tuu ukajua kwamba kuna gas? Wewe ndio ulitafiti hii gas? Unadhani ni mkojo huo kwamba utakuta unavuja kama unavyojikojoleaga kitandani?

Eti kwani ni lazima ichimbwe kizazi chenu,kwa hiyo ukiacha na hujaandaa mazingira ya hicho kizazi kingine kitazaliwa kina akili automatically? Una akili timamu? Is technology waiting your kizazi? Saizi tuna maelfu ya Tani za fossil fuels unfortunately 30 years to come Dunia inapiga marufuku matumizi ya makaa,kwa hiyo kizazi kitafaidia makaa sio? Mega fool wewe.

Una hoja za kitoto na za kijinga, mnawaza ujinga mara 10% and such nonsense.Faida tutakazopata kama Taifa hizi hapa πŸ‘‡

Tupe uthibitisho wa kutoaminika kwa jarida la The African Report, tupe pia uthibitisho wa wamiliki wa Gesi ambao ni tofauti na Serikali
Huu Mchakato ulianza tangia 2016 na Stakeholder wa Kujenga hio Plant ni kama ifuatavyo

Stakeholders[edit]​

Talks between the government of Tanzania and the six oil companies involved in the project began in earnest in September 2016. The oil companies involved include:[11]

  • Equinor ASA (formerly Statoil ASA)
  • ExxonMobil
  • BG Group
  • Royal Dutch Shell Plc
  • Ophir Energy Plc
  • Pavilion Energy Private Limited
Also participating in the talks are the following parastatal agencies of the Tanzanian government.[11]

Wanajitoa ufahamu kutokana na chuki zao tu! Hawana lolote la maana zaidi ya kujawa na chuki tu

Hawajui pia kuwa sasa Umoja wa Ulaya umeamua kutambua Gesi kuwa moja ya renewable energy kwa iyo uhakika wa uchumi wa Gesi upo sana kwa miaka mingi ijayo

Kwa hali inavyoendelea sasa Ulaya wanahamia Afrika Kama sehemu yao ya kutegemea nishati na Chakula na wala sio Urusi tena. Hivyo ni fursa Kubwa sana kwetu kiuchumi
 
Wewe ni mpumbavu,uliamka tuu ukajua kwamba kuna gas? Wewe ndio ulitafiti hii gas? Unadhani ni mkojo huo kwamba utakuta unavuja kama unavyojikojoleaga kitandani?
Akili ya mtu na fikra potofu ni ku-attack personality na sio hoja; Mimi nimekwambia hayo mawazo ni potofu kuliko..., hao stakeholders sita walioingia mkataba leo ndio walifanya research, na hizo research walifanya kwa hisani? Gas huko iligunduliwa lini na nani na wanaosign mkataba leo ni kina nani ?
Again rudia nilichoandika ni lazima natural resources zote zimalizwe katika kizazi chetu ?, Kwa matumizi mazuri tungeweza kuchimba baadhi na kutumia hio faida kuwekeza kwenye migodi mingine kwa stake nzuri zaidi.., Mfano Mkataba wa Diamond Botswana ni sawa na wa kwetu ? Je Dunia pia itapiga marufuku matumizi ya Diamond na Gold ?

Una hoja za kitoto na za kijinga, mnawaza ujinga mara 10% and such nonsense.Faida tutakazopata kama Taifa hizi hapa πŸ‘‡

View attachment 2129410
Unajua maana ya faida ? Tunapata percent ngapi kwa huo uwekezaji ? Alafu usiamishe mjadala hapa umeongelea kwamba wacha tupate stake kidogo sababu hatukufanya research na hatuna uwezo ili tupate faida ya ajira na Kodi....

Kweli Akili ni Nywele....
 
Wanajitoa ufahamu kutokana na chuki zao tu! Hawana lolote la maana zaidi ya kujawa na chuki tu

Hawajui pia kuwa sasa Umoja wa Ulaya umeamua kutambua Gesi kuwa moja ya renewable energy kwa iyo uhakika wa uchumi wa Gesi upo sana kwa miaka mingi ijayo
Aisee !!!!!
Kwa hali inavyoendelea sasa Ulaya wanahamia Afrika Kama sehemu yao ya kutegemea nishati na Chakula na wala sio Urusi tena. Hivyo ni fursa Kubwa sana kwetu kiuchumi
Hivi ni lini Tanzania au Afrika imekuwa na uhaba wa Natural Resources ? Tuna Dhahabu, Diamond, Tanzanite, Tourist Attractions n.k. (kuwa na vitu vyenye thamani haijawahi kuwa tatizo tatizo ni kwenye mikataba ya kinyonyaji na kipuuzi tunayoingia)

Pili hata bila ulaya soko la LNG lipo kubwa tu hata huko China, Japan n.k. Ndio maana USA analionea Potential na hata Canada na yeye anataka kuingia kwenye uwanja....

Mambo ya Russia mwisho wa siku yatakuwa solved its cheaper kutumia Natural Gas ikiwa Piped kuliko hio Natural Gas kuwa liqufied (its costly kufanya hivyo na storage yake ni expensive)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…